Siku moja Mwaka 1975 mpigapicha na mwandishi wa habari bwana Stanley Forman alinasa tukio ambalo limebaki katika kumbukumbu ya moja ya matukio mabaya zaidi kuwahi kurekodiwa tangu teknolojia ya uvumbuzi wa camera duniani.
Tukio hili alilolinasa bwana Stanley lilikuwa likimuonesha mrembo wa miaka 19 diana Bryant na mwanae msichana wa miaka 2 aliyeitwa tiare jones wakiruka kutoka kwenye dirisha la apartment waliyokuwa wakikaa hadi chini baadaa ya kushika moto.
Picha hiyo aliyonasa ilizua hisia sana wakati huo ndani na nje ya Marekani wakati huo ikionyesha ni kwa jinsi gani kuna mstari mwembamba sana unaotenganisha Uhai na kifo.
Picha hii iliyonaswa na Stanley ilishinda Tuzo ya pullitzer mwaka 1976 na ilikuwa ni moja kati ya picha za kuhuzunisha na vilevile disturbing image huku ikiongea mengi kuwahusu wahusika waliomo ndani ya picha hiyo na hatma yao .
Huyo Diana Bryant alifariki muda mfupi baada ya kuanguka kutokana na majeraha mabaya aliyoyapata ikiwemo kuvunjika ila bintiye huyo mdogo hakufa bali aliangukia juu ya mwili wa mama yake hivyo hakupata majeraha makubwa.
Picha hii ilizua mjadala mpana ndani ya jamii ya wamarekani kuhusiana na maadili ya kuchapisha picha za aina hii kwenye kurasa za magazeti , vilevile uzembe wa hali ya juu ulioonyeshwa na waokoaji ( firefighters)katika kuwanusuru .
Picha hii ilipelekea kutungwa sheria na miongozo katika ujenzi wa exit position chambers kwenye apartment za miji endapo kutatokea ajali kama za moto n.k.