Msukuma wa Ushirombo na Afisa wa FFU kwenye simu

Msukuma wa Ushirombo na Afisa wa FFU kwenye simu

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Mayaya Jembeulaya – Harooo… hapo ni Ghasia?

Inspekta Marwa – Ndiyo, Fidi Fosi mkoa wa Geita, mimi Inspekta Marwa, una shida gani?

Mayaya Jembeulaya – Nimetoka Dsm nimekuta mtu anahujumu uchumi wa taifa, baghosha!

Inspekta Marwa – Anahujumuje uchumi wa taifa?

Mayaya Jembeulaya – Anaitwa Mangi, anauza haja klubwa kwa shs.300 na haja ndogo kwa shs. 200, tafuta nauli ya wawili nikupeleke umkamate.

Inspekta Marwa – Wewe umenunua?

Mayaya Jembeulaya – Doho… hana iefudii.

Tii tii tii… simu imekatika.

Tukio siyo halisi ni Chit-Chat kuchagiza mabadiliko ya lugha katika sehemu za huduma ya maliwato ya umma.

Majwala
 
Vichekesho vingi kwenye hili jukwaa havichekeshi
Nimetumia sanaa ya lugha kurekebisha wanaochafua lugha ya Kiswahili kwa matangazo yenye maudhui yanayotoka nje ya muktadha hususan kwenye biashara ya huduma ya maliwato mijini.

Iko siku BAKITA itaendesha operesheni ya kamatakamata wanaochafua lugha ya Kiswahili kwa namna yoyote ile sijui kitasalia nini.

Kama kamatakamata hii ingelikuwepo miaka mingi, kwa upande wa viongozi wa kitaifa angesalimika Mwl Nyerere na Ben Mkapa tu.
 
Back
Top Bottom