Msumbiji imekumbwa na maradhi yapi?

Mwelewa,
Jana rafiki yangu mmoja kanipigia simu baada ya kusoma hii post.
Kanambia nifike Chang'ombe Maduka Mawili nielekee Sigara Club
nitakutana na mtaa unaitwa Maji Maji.

Hapo kuna nyumba ya National Housing ina kibao nje kinasema
kuwa nyumba hiyo akiishi Marcelino Dos Santos.
 
Good analysis ila binafsi naamini Yote hayo yalikua kwenye utashi wa kisiasa (kiutawala kipindi hicho) kwa maana wao walikua first generation being supported

Kadri miaka inaenda na vizazi vipya vinakuja, hua hayo mambo yanasahaulika
Ref: farao na waisrael km Wasoma bible
Pia kizazi cha sasa vs kizazi cha zamani khs ishu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 

Ni kumbukumbu nzuri sana. Ukarimu huo ulikuwa zamani sio sasa
 
Mohamed Said,

..wewe hukwenda kubaingaiza huko Msumbiji ndiyo maana ukawa unaheshimika.

..mimi nakuhakikishia nchi yoyote ile ya dunia ya tatu ukienda kwa mambo ya kubangaiza-bangaiza utapata treatment sawa na waliyoipata ndugu zetu huko Msumbiji.

NB:

..siku nyingi hatujaongea humu ndani. lakini kuna Mzee wetu maarufu Kariakoo na Dsm Mzee MANGARA TABU MANGARA. sijakusikia ukisema chochote kuhusu Mzee huyu. Lakini ni mtu muhimu sana haswa kwa wapenzi wa timu ya Pani Afrika.
 
JokaKuu,
Mtaa wa Swahili huku Narung'ombe na huku Mchikichi ndipi ilipokuwa
nyumba ya Mzee Mangara Tabu.

Nyumba hii inapakana na nyumba ya bibi yangu.
Sisi wadogo tunamuona Mzee Mangara pale nyumbani kwake.

Sijapata sababu ya kumzungumza Mzee Mangara.
Mzee Mangara umaarufu wake ni kwa Young Africans si Pan African.
 

..ha ha ha.

..basi nimeshakusoma.

..wewe utakuwa mtu wa Simba.

..Mangara ni mzee wa Pan African.
 
Kaka Mohamed Said , kweli ni majonzi kwa ndugu zetu wanaoteseka huko Mozambique hasa hasa eneo la Montepuez, lakini je huo msako wa kuwafukuza Watanzania upo nchi nzima ya Msumbiji au hapo Montepuez tu

Shida iko hapa, hayo maeneo ya Montepuez ambayo Watanzania na watu wa mataifa mengine wamefukuzwa ni maeneo maalum yenye madini ya Ruby, na leseni za uchimbaji na utafiti wa madini hayo kwenye hayo maeneo ni zile leseni kubwa (Mining-Prospecting lisences) ambazo unakuta leseni moja inacover eneo kubwa sana, na kwa kisheria eneo kama hilo hakutakiwi kuwe na activities zozote zinazohusiana na mambo ya madini hayo ila kwa idhini ya mwenye hizo leseni akishirikiana na Serikali ya huko

So Watanzania kwa kushirikiana na Askari wa Mozambique walikuwa wanaingizwa illegally kwa kutoa rushwa, na kufanya shughuli za uchimbaji wa madini kwenye hayo maeneo ambayo sio yao, na kama unavyojua shughuli za uchimbaji wa madini unaambatana na uwekezaji wa ma bar, mahotel, Guests nk, hivyo kulikuwa na group la wachimbaji na wafanya biashara lakini wote walikuwa wanategemea uchimbaji haramu na uuzaji wa Ruby

Watu wenye Leseni zao wakatoa malalamiko kwa Serikali ya Msumbiji kuwa wao wanayalipia hayo maeneo lakini kuna uchimbaji unaendelea, ndipo Serikali ikatoa Amri ya kuwatoa wote walioko kwenye hayo maeneo ya Machimbo- Montepuez, Askari wa Mozambique wana tabia moja hata kama anakujua lakini siku ya kukubadirikia hata risasi anakutwanga, Watanzania wachache ndio walikuwa na vibali halali vya kuingia Mozambique lakini sio vya kufanya uchimbaji, wala biashara yoyote so wakikukuta unaangaika na chochote nje ya status yako ya Visa wanakuweka group moja na wasio na vibali na unarudishwa kwenu, so kama uliingia bila kitu huwezi kutoka na kitu kwa sababu viza yako haina status ya kukufanya utoke na chochote ulichozalisha illegally,
Kwa kifupi Watanzania walivunja Sheria za ukaazi wa katika hayo maeneo ya Mozambique

Lakini ukifika maeneo ya Niassa Province kwa kupitia mpaka wa Mbinga kuna uchimbaji wa dhahabu unaendelea kule na wanaMsumbiji wenyewe wamepewa leseni ndogo za mining (Primary Mining Lisence) na wao wamepewa ruhusa ya kuwaita Watanzania na kufanya nao kazi, so Mwana msumbiji anakuchukua na ku-declare kuwa wewe ndio partner wake wa uchimbaji na unapewa kipande (document) za kukuhalalisha kukaa na kufanya kazi kule. Ukifika hayo maeneo utakuta 90% ya wachimbaji kule ni Watanzania na huwezi kusikia wanafukuzwa kama hao wa Montepuez

Tufate Sheria na taratibu za ukaazi tunapokuwa kwenye nchi za ugeni
 
Kituko,
Ahsante kwa hii taarifa.
Vipi kuhusu vipigo na ubakaji?
 
Kituko,
Ahsante kwa hii taarifa.
Vipi kuhusu vipigo na ubakaji?

Kama nilivyosema Askari wa Mozambique anakuwa rafiki yako na akikubadirikia na kukuita Bandidu "Bandit" basi hapo anakuwa juu ya sheria, so hao wote (Watanzania) walikuwa kwenye hilo group la Mabandidu,

Vipigo na unyanyasi ulitokana na
1: kundi la Askari maalum lililoletwa kwa ajili ya hiyo operation, so wao walichokuwa wanajua ni kuwatoa Foreigner (tresspasser) kwenye maeneo yasiyowahusu.
2: Baadhi ya Watanzania kukataa kuondoka bila mali zao walizozichuma kwa miaka kadhaa, say 3-5yrs, uanche magari, mitaji nk, lakini wanaambiwa Huna Visa inayokuruhusu kuchuma mali, so ondoka kama ulivyoingia
3: Baadhi walikuwa wanagoma kuondoka kutokana na visa halali au residence permit walizokiwa nazo, shida inakuja wewe una Visitor Visa, lakini unaendesha Bar, au unanunua Ruby, au unachimba Ruby, so una visa ya halali lakini upo kwenye eneo usilostahiki kuwepo wala kutumika
 

Umerefusha mada kwa kuleta hadith zingine ziszona sabbu bila sababu.

Hivyo unvyoshangaa, ndivyo hata mataifa mengine wanachangaa wakiona Tanzania ya vingozi wengine baada ya Nyerere. Tanzania ya wauza madawa ya kulevya, Tanzania ilyojaa rushwa na ufisadi, tanzania isyojali haki za binadmau, Tanzania isiyojali watu wake, nchi yenye matabaka na ubaguzi. Ni tatizo la utawala mmoja kubinafisha nchi, hakkuna ukosoaji, hakuna ukweli,, hakuna uwejibikaji ni ubabe, ubinfsi na unafiki.
 
Ninachofikiria Mimi
Wananchi wa Msumbiji wamekutana na maisha magumu, maisha yenye changamoto nyingi, wamekata tamaa, na mwanzo bila shaka waliamini serikali yao itawafikisha pazuri( ndo mtazamo wa wananchi wengi hata Tanzania), lakini kwa bahati mbaya bado hiyo ndoto haijatimia.

Tusiende mbali hapahapa kwetu Tanzania watu wamekata tamaa, wameshajua serikali si kwa ajili ya wanyonge.
Sasa na huko Msumbiji wananchi wanayoyafanya yanatokana na maisha magumu ambayo hutengeneza stress na kupelekea kua na hasira juu ya watu wengine.
Katika kutazama nani anawakwamisha wakaona pengine wageni (Watanzania) wanachangia hali yetu kua ngumu, wao wanafanya biashara na kufanikiwa sisi mbona hakuna kitu sasa basi cha kwanza tuwaondoe hawa watanzania kwanza.

Hata sisi hapa hua tunawashutumu raia wa kigeni mfano wachina, utasikia wachina wanapewa migodi, tenda za ujenzi n.k mbona sisi tunanyimwa wazawa? It means hata sisi tumeanza kupata hiyo mentality ya Msumbiji na kadri hali inavyozidi kua ngumu na serikali inazidi kuwakatisha watu tamaa, siombei mabaya ila mbele naona giza wakuu.

Mungu atupe uvumilivu.
 
Tabby uandishi ni sanaa. Uandishi huu si sawa na kuandika dondoo za mkutano. Unaweza wewe ukaona kuna yasiyo na maana lakini kuna wengine katika hayo unayoona hayakuwa na umuhimu wanajifunza mengi.
 
Mzee Mohammed usihuzunike sana Mwanadamu hubadilika, Wana usalama wetu wapo kazini kuangalia the main source Muda utatoa majibu sahihi Tuwe na subira tu japo ni Sad sana
 
Pamoja na kutahadharisha kuwa kile kilikuwa ni kizazi kilichoshuhudia na hiki ni kizazi kinachosimuliwa (ndo maana kuna mmoja kasema ni hadithi) nakuwekea picha ya shemeji yako niliyoichukua na kisimu changu cha mchina tarehe 17 january 2017 cape town. Uzee haupigi hod
 
Kampelewele,
Kuna kitu nataka nikugusie.
Kaka yangu aliniahidi kuwa nikenda Cape Town tutakwenda kumuona Chaka Chaka.
2006 nilikwenda kumtembelea lakini sikukumbuka tena habari ya Chaka Chaka.
Ndugu yangu mbona vitu vingi siku hizi vinatoka China?
Ahsante sana kwa picha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…