ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Nchi ya Mozambique imeamua kuteka biashara ya Usafirishaji Kwa njia ya Maji Kwa Nchi zote za Sadc na kuiachia Tanzania maumivu makubwa.
Katika kutekeleza Hilo, Mozambique wameamua kuikodisha Bandari Yao ya Nacala Kwa Nchi ya Malawi na Zambia ambapo wataitumia Kwa kipindi Cha miaka 100 ijayo.
Nchi hizo 3 zinapanga kujenga miundombinu ya reli kutoka Nakala Hadi Mji Mkuu wa Malawi Lilongwe na kisha Hadi Mji Mkuu wa Zambia Lusaka.
Njia hiyo Mpya ya reli itapunguza umbali wa Zambia kuifikia Bandari ya Dar hivyo zaidi ya asilimia 90% ya mzigo wa Zambia utapitia Bandari za Msumbiji za Nakala na Beira.
Kwa hatua hiyo itakuwa ni pigo kubwa sana kwa Tanzania ambayo Bandari ya Dar ilikuwa inategemea zaidi mzigo wa Nchi ya Congo DRC na Zambia kama wateja Wakuu huko Nchi zingine zikiongesea ongezea shehena.
Endapo Zambia itaondoka rasmi kuwa mteja wa Tanzania sio tuu itapunguza mzigo wa Bandari ya Dar Bali itaua kabisa biashara ya Malori ya mizigo Tanzania ambapo Kwa sehemu kubwa yatahamia Nchi hizo za Zambia,Malawi na Msumbiji na zingine za Afrika Ili kuendelea na Biashara ya Usafirishaji.
Pia soma: Bandari za Dar na Mtwara Kuwa Mashakani Kutokana na Nchi za Zambia,Malawi na Mozambique Kuzindua Upanuzi Mkubwa wa Miundombinu ya Nacala Port.
Kwa maelezo zaidi soma hapa Ili Kuongeza Ufanisi wa reli ya TAZARA,Tanzania na Zambia Ziiombe China Wajenge reli Mpya ya Makambako-Mtwara & Kasama-Lubumbashi/Likasi
Ushauri:
Serikali ihakikishe mipango yetu yote Kwa Sasa iwe inalenga kuikumbatia DRC kuanzia Kusini Hadi Kaskazini maana ndio mteja pekee ambae walau jiografia inatupa nafasi.
Serikali ifanye yafuatayo:
1. Lazima tujihusishe na kutafuta amani directly ndani ya DRC Ikibidi Kwa gharama zetu.
2. Lazima Sgr na Barabara zivuke na kuifikia DRC (Bukavu,Goma, Kinshasa, Kindu)
3. Lazima tuwashawishi Zambia na DRC tujenge reli kutoka Tunduma-Kasama-Lubumbashi-Likasi na Kutoka Makambako-Mtwara Port.
4. Lazima Sgr itoke Mpanda-Karema na Kigoma
5. Lazima tutafute pesa za kujenga meli kubwa za mizigo na abiaria ndani ya Ziwa Viktoria na pia tujenge Bandari,Barabara na reli upande wa DRC hata Kwa kuwakomesha pesa
6.Lazima tuwape DRC,Rwanda na Burundi Ardhi za Bure za kumhudumia mizigo Yao Pwani.
My Take
Tusipofanya hayo tunaenda kupoteza hata hiyo DRC Kwa Kenya, Angola na Mozambique na ikizingatiwa DRC inajenga Bandari na reli kuunganisha na Zambia na Angola.
Washindani Wetu wa Kenya wao Wana uhakika na Uganda, South Sudan, Northern DRC na somehow Ethiopia na Rwanda.
Tuachane na Mpango wa kujenga reli ya Mtwara Corridor hiyo Haina maana tena imeshakufa,Nguvu zote zielekezwe Kujenga kioande Cha kutoka Makambako -Mtwara.