Msuva aibuka shujaa huko Morocco

Msuva aibuka shujaa huko Morocco

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Nyota wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva usiku wa jana ameibuka shujaa wa timu yake ya Difaa Hassan El Jadida, baada ya kufunga mabao mawili ambayo yaliisadia kutoa sare ya 3-3 ugenini katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco dhidi ya Olympique de Khouribga.

MSUVA 1.jpg

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya nchini Morocco. Msuva alifunga bao la kwanza katika dakika ya 65 huku bao la pili akifunga dakika ya 90+2, bao ambalo lilikuwa la kusawazisha na kuiokoa timu yake kuondoka na kichapo.

Bao la kwanza la Difaa Hassan El Jadida lilifungwa na Tarik Astati dakika ya 33. Mabao ya Khouribga yamefungwa na Zouhair El Moutaraji mawili dakika za nne na 38 na Adam Nafati dakika ya 55.

Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja Jadida na kushuka kwa nafasi moja hadi ya nne kwenye Ligi ya Morocco yenye timu 16, ikifikisha pointi 38 baada ya kucheza mechi 25.

Msuva amekuwa akifanya vizuri nchini Morocco akiwa kwenye msimu wake wa kwanza ndani ya klabu ya Difaa iliyomsajili majira ya kiangazi akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Yanga SC.

Chanzo: EATV
 
Asante Msuva asante Yanga
 
safiii, kila la kheri kwake aendelee kufanya poa. asiishie kuwapiga mabao tu achukue na mbinu zao chafu wanazotumia kutufunga (ndani na nje ya uwanja) hawa waarabu ili iwe msaada kwetu.
 
Mkuu acha kua na fikra za kizamani,mbinu gani hizo chafu? kwani kwenye mpira hua mnafungwa na waarabu tu eeh? kwahiyo tz ina mpira bali hufungwa kwa mbinu chafu tu? acha kutafuta wakumtupia lawama zisizo na msingi,mjipange.
 
una fikra mpya ila zimefubaa, kuna mbinu za ndani na nje ya uwanja ili kupata ushindi.Tunafungwa na timu tofauti ila mara nyingi waarabu wamekuwa wakitutoa kwenye michuano kwa mbinu chafu (kama kutupulizia dawa za uchovu vyumbani, kutulaza hotel zenye kelele, kutupa msosi wa hovyo, kuchelewa kutupokea ama kutupa malazi) izo no baadhi mkuu.
Kama unafikra kwamba mpira huchezwa bila mbinu chafu ww una fikra zilizo fubaa
 
Hahahaha! eti kutupulizia dawa za uchovu vyumbani! kutupa msosi wa hovyo! hivi mkuu uko serious kweli? kwa dunia ya sasa hivi ufanyiwe hivyo na hatua zisichukuliwe? hizo ni hekaya za kizamani sana tuliaminishwa eti kipa akitaka kudaka anaonyeshwa bastola anauacha mpira linaingia goli! Enzi zile hakuna hata tv,

Anzisheni football academies acheni kutafuta pakutokea,hebu ipeleke Brazil au Ujerumani huko kwa waarabu halafu wafanye huo usanii wao tuone kama watashinda hata gemu moja!
 
Itakuwa umeanza kufatilia soka majuzi, izo fitna mbona sana zinatokea. rejea yanga alipoenda cheza (kama sio botswana basi ni zambia ) niruhusu masahihisho. walipewa basi flani limechoka balaa, uongozi ukashauri watumie usafiri waliopewa na watanzania wa lule.

lile basi lilikuwa limepuliziwa dawa na viongozi waliumwa balaa (walio panda lile basi). umeanza kufatilia mpira 2017 ulipo nunua simu janja bado unaleta ubishi wa mbinu chafu nje ya uwanja
 
Ulichoongea ni sahihi kabisa. Tatizo letu hatutaki kufuata njia sahihi za kupata mafanikio lakini tuna tamani mafanikio. Ila ukiangalia uhalisia wenzetu wamewekeza na ndio maana wanapata mafanikio. Na hili limekuwa tatizo kwenye nyanja nyingi na ndio maana tunafeli na kwa bahati mbaya watu wamesha tengeneza excuse badala ya kuangalia tunapo kosea ili tufanye marekebisho.
 
Nilidhani naongea na mtu mkubwa mwenzangu kumbe naongea na kitoto cha shule! kwani ungetoa tu hayo maoni yako bila hivyo vikejeli vya kitoto nisingekuelewa?
Halafu una akili nzito sana ya uelewa bora nikuache uendelee kubweteka na kuamini kua soka lenu haliendelea na hamfiki popote eti kisa mnafanyiwa mbinu chafu! sasa hizo mbinu chafu nyinyi hamjui kuzifanya? au mmezidiwa mpira mpaka na mbinu chafu?
 
Ulichoongea ni sahihi kabisa. Tatizo letu hatutaki kufuata njia sahihi za kupata mafanikio lakini tuna tamani mafanikio. Ila ukiangalia uhalisia wenzetu wamewekeza na ndio maana wanapata mafanikio. Na hili limekuwa tatizo kwenye nyanja nyingi na ndio maana tunafeli na kwa bahati mbaya watu wamesha tengeneza excuse badala ya kuangalia tunapo kosea ili tufanye marekebisho.
bora hata wewe umenielewa vizuri mkuu.
 
Yusuph muhilu nae miaka miwili ijayo atakua au atamzidi msuva..yule dogo ni balaa mjini hapa
 
una fikra mpya ila zimefubaa, kuna mbinu za ndani na nje ya uwanja ili kupata ushindi.Tunafungwa na timu tofauti ila mara nyingi waarabu wamekuwa wakitutoa kwenye michuano kwa mbinu chafu (kama kutupulizia dawa za uchovu vyumbani, kutulaza hotel zenye kelele, kutupa msosi wa hovyo, kuchelewa kutupokea ama kutupa malazi) izo no baadhi mkuu.
Kama unafikra kwamba mpira huchezwa bila mbinu chafu ww una fikra zilizo fubaa

Dah nimecheka sana aise...yani usithubutu kuongea haya maneno yako ya kupuliziwa dawa kadamnasi...yani watakucheka sana at end of the day watakupuuza. Sisi na mpira wapi na wapi, kwani ndio first time kufungwa??? Mbona Nigeria walipigwa nyingi tu na hao hao Morroco mbona hukusema nao walipuliziwa dawa!!! Mtu anaejuwa mpira hawezi kuongea haya maneno kiongozi....kuna wengine walijitoa ufahamu miaka ya nyuma eti mechi ya France na Brazil 1998...wakaja na maneno kama yako tukawapuuuza tu. So kama hujui mpira kiongozi ni heri ukae kimya ili usiendelee kuaibika. Ni ombi tu wala usinihisi vibaya.
 
Itakuwa umeanza kufatilia soka majuzi, izo fitna mbona sana zinatokea. rejea yanga alipoenda cheza (kama sio botswana basi ni zambia ) niruhusu masahihisho. walipewa basi flani limechoka balaa, uongozi ukashauri watumie usafiri waliopewa na watanzania wa lule.

lile basi lilikuwa limepuliziwa dawa na viongozi waliumwa balaa (walio panda lile basi). umeanza kufatilia mpira 2017 ulipo nunua simu janja bado unaleta ubishi wa mbinu chafu nje ya uwanja

Tukubali waarabu wapo juu kisoka,, wanajuwa wanachokifanya...sisi twendelee na politics zetu. Pembeni birika la kahawa.
 
Mkuu achana nae huyo bado anaishi na fikra za zama za mawe,umfunge Algeria kwa mpira gani ulionao? umfunge Misri,Morocco? au Tunisia? kaeni mjitafakari ni wapi mnakosea kuliko kulia lia na kutoa vilawama visivyoeleweka,kushiriki tu kombe la Africa toka mwaka 1980 mpaka leo hakuna kitu! kushiriki kombe la dunia ni ndoto!! mpira unataka uwekezaji na sio maneno mepesi mepesi.
 
You are absolutely right kiongozi...
 
Back
Top Bottom