Msuva mambo safi Afrika Kusini, Yanga waletewa ofa rasmi ya kumuuza

Msuva mambo safi Afrika Kusini, Yanga waletewa ofa rasmi ya kumuuza

Zatara

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2012
Posts
716
Reaction score
511
attachment.php

MFUNGAJI bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simon Msuva anarejea jioni ya leo Dar es Salaam na tabasamu ‘kuubwa’ baada ya kufaulu majaribio ya kucheza soka ya kulipwa Afrika Kusini.

Winga huyo wa mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC jana amekamilisha majaribio yake ya siku tatu Bidvest Wits ya Ligi Kuu nchini humo na matokeo ni ‘safi’.

BIN ZUBEIRY inafahamu Bidvest Wits wameridhika na uwezo Msuva na sasa wanafungua majadiliano na klabu yake, Yanga SC.

Msuva amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake Yanga SC na Wits iko tayari kutumia si zaidi ya dola za Kimarekani 100,000 (Sh. Milioni 200) kukamilisha dili zima la mchezaji huyo- kwa maana ya malipo ya mchezaji kusaini na ada ya uhamisho kwa klabu yake.

Msuva aliondoka Dar es Salaam Jumatano wiki hii akiwa tayari ameipa Yanga SC ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, huku pia akiwa anaongoza kwa mabao, 17 akifuatiwa na mchezaji mwenzake wa timu hiyo, Amissi Tambwe mabao 14. - Amekosa mechi mbili za mwisho dhidi ya Azam FC Yanga ikilala 2-1 na leo dhidi ya Ndanda ya Mtwara.

Tangu ajiunge na Yanga SC mwaka 2012 akitokea Moro United, Msuva ameifungia timu hiyo mabao 35 jumla katika mechi 102 za mashindano yote.

Chanzo: BinZubeiry Blog
 
Attachments

  • SIMON MSUVA.jpg
    SIMON MSUVA.jpg
    31 KB · Views: 1,156
What next is very clear. Waje Yanga lakini wasijipangie bei wao. Wasikilize Yanga inasema nini.
 
Hakika mkuu, hiyo ni biashara na Msuva ni bidhaa. Ila Yanga wasibane sana katika ada ya uhamisho.

wanaweza pia kutengeneza mkataba ambao utamruhusu aende. Ila iwapo atafanya kweli na kuuzwa team kubwa zaidi basi Yanga nayo iendelee kunufaika
 
Nimemsikiliza katibu yanga anasema wameshatuma barua FIFA sasa hapo labda busara tu ije itumike kama ilivyozoeleka lakn upuuzi wa mazoea si mzuri hata kidogo unarudisha chini professionalism
 
Ninachojua msuva tutazidi kumuona hapa hapa bongo
.Ngassa alifuzu last year,Yanga wakataka hela ndefu,free states wakachimoa.

Miezi kadhaa badae ngasa akaondoka bure
 
Kinachosikitisha wachezaji wetu wana upeo mdogo mambo ya mikataba na hatuna mawakala wa kuwasaidia,Tanzania ina wachezaji wengi wenye uwezo kucheza nchi za nje (Africa ).Angalia wachezaji toka Kongo,Burundi,Rwanda,Kenya wanavyojitahidi kwenda nje ya nchi zao lakini wa kwetu ni wachache sana (Ulimwengu,Samata,Liuzio)
 
Hapa timu yangu pendwa naomba msuva msimletee figisufigisu mwache akaangalie maisha huko bondeni tutapata mchezaji mwingine mzuri zaidi yake,
kwa mfano uondokaji wa Frank Domayo ulinipa shida kweli lakini kaja Salum Telela ambaye ni bora kuliko Domayo.
 
Kweli wamuache akatafute maisha zaidi aisee, wasimbanie
 
pamoja na hayo mkuu kuna wasiwasi wa timu yetu kuyumba msimu ujao maana kuna wachezaji si chini ya 6 wa kikosi cha kwanza wanaweza kuondoka,hivyo viongozi waliangalie hili mapema ili kupata mibadala yao kabla hawajawaiwa .
 
Kweli wamuache akatafute maisha zaidi aisee, wasimbanie

Hapa sijui, unajui viongozi wa mpira Yz, ni magumashi tu, usije shangaaa hiyo Milion 200,wakaiona ndogo, wao wakalopoka 800m!!!ili abaki tu, then mwakani anaondoka free!!! hapa tz labda azamu ndio hawana mambo hayo, ila hizi timu chakavu, ni shida
 
Mi kuamini ni mpka nimuone anacheza,vyombo vya habari vya tz ni ovyo kwa kurukia mambo wasoyajua.!
 
Mi kuamini mpaka nimuone yuko uwanjani na jezi yake imeandikwa jina lake ndo nitaamini tofauti na hapo yaleyale ya Ngasa
 
Mi kuamini ni mpka nimuone anacheza,vyombo vya habari vya tz ni ovyo kwa kurukia mambo wasoyajua.!
wewe jamaa upo sahihi kabisa. Vyombo vyetu vya habari hasa magazeti na mtandao ya kijamii huwa wanaandika mawazo yao tu. Yaani wakidaka moja tu tena sio kutoka kwenye reliable source basi wao wataliboresha kama taftari la kura.
 
Yanga msubiri milioni 700 so mlisema Ana thamani hyo!!
 
Yanga msubiri milioni 700 so mlisema Ana thamani hyo!!

Hiyo ni thamani ya Saimon Msuva endapo Klabu yoyote ile ndani ya ligi Kuu Tanzania bara itamuhitaji..

Endapo Klabu yoyote nje ya Tanzania itamuhitaji basi Maelewano yatafanyika.

Umeelewa....?

Yanga kwa jinsi walivyo na roho mb.....hawawezi kumuuza. Hawapo tayari kumuona mchezaji wa timu yao ananufaika hata mara moja. Tusubiri tuone, watajaza visingizio kama wanampenda kumbe wapi!
 
Back
Top Bottom