Mswahili ukisali kwa kiingereza tunajua hauna matatizo makubwa

Mswahili ukisali kwa kiingereza tunajua hauna matatizo makubwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Umesoma katika hizi shule za "saint Government" miaka yote na unaomba Mungu kwa lugha ya Kiingereza?? Ulianzaje na uliwezaje?

Nilisoma sehemu kwamba, ukiona Mswahili anaomba Mungu kwa lugha ya Kiingereza, basi jua mtu huyo ana SHIDA NDOGO au MATATIZO MACHACHE.

Kwa wanaojua namna Waswahili wanavyotaja mambo mengi kwenye maombi yao wanaelewa kinachomaanishwa hapa.

Eti kuna mtu huko, aliomba huku akisema; " OH LORD, I KNOW YOU ARE NOTHING WITHOUT ME AND YOU NEED MY HELP" mtu aliyekuwa kando yake alipomuuliza maana ya maombi yake akasema, " EEH MWENYEZI MUNGU, MIMI SI KITU BILA WEWE NA NINAHITAJI MSAADA WAKO" JAMANI JAMANI!!!

Huyu mwingine alisikika akiomba, " OH GOD WE PRAY FOR YOU, AND OUR DEAR MOTHER, WE PRAY TO YOU" Akidhani anamwomba Mungu na kumwombea mama yake, kumbe amesema anamwombea Mungu na kumwomba mama yake.

Nakumbuka mwaka ambao niliacha kuomba kwa Kiingereza, ulikuwa muda wa kulala na nikasema, "PLEASE GOD BLESS THIS FOOD" nikashtuka na KUISHIA njiani!! Food my foot!! Food kitandani, tena nipo alone! Which food na si Mchawi!!

TUIPENDE LUGHA YETU INAKIDHI MAHITAJI YAKE YA MSINGI YA MAWASILIANO.
Ujumbe na utani.
 
🤣 Kabisa Yaan! Afu kwanini utumie kiingereza wakati lugha yako unayo? Au ndo kumpi ma Mwenyezi kama anakiweza?
 
Umesoma katika hizi shule za "saint Government" miaka yote na unaomba Mungu kwa lugha ya Kiingereza?? Ulianzaje na my foot!! Food kitandani, tena nipo alone! Which food na si Mchawi!!

TUIPENDE LUGHA YETU INAKIDHI MAHITAJI YAKE YA MSINGI YA MAWASILIANO.
Ujumbe na utani.

Yesu aliagiza maombi hayataki maneno mengi, yakiwa mengi unakuwa unafiki​

Mt 6:5-18 SUV​

Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.] Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
 
Hata mtu AKIKASIRIKA kwa kiingereza hayupo serious!😀
"Please John don't do this...."
 
Huku kwetu Kiingereza ni lugha ya walevi, mtu akiwa tungi ndiyo utamsikia akichomekea maneno mawili mawili.

Hata Maprofesa wengi kimalkia kinawapiga chenga, yaani ikifika taimu ya kuongea hii lugha mbele ya kadamnasi basi lazima awe na kitambaa kwaajili ya kufuta jasho linalotoka hata kama ndani Kuna full AC.

Na siyo kuomba tu, huwezi kwenda kwa mtu kukopa hela halafu uongee hii lugha anaweza sema huna shida.
 
Kuna sista alikuwa akija kututembelea, wakati wa kulala anasali muda mrefu hadi unachoka. Anaingiza na kunena kwa lugha.
 
Back
Top Bottom