Mtaa wa Agrey, mtaa unaokuwa kwa kasi zaidi DSM kwa mishemishe

instagram

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,118
Reaction score
4,863
Kama ilivyokuwa kwa mitaa ya Pemba Kkoo na Samora posta streets enzi za 80's/90's, Azikiwe street(Zero Brain) 2000's, mtaa wa Agrey ndo mtaa unaoukua kwa kasi sana sasa hv kwa mishemishe za town.

Mtaa wa Agrey ndo mtaa ambao ukitaka ishu yoyote ya simu, pc, jeans, shati, electronic, restaurants unapata.

Sasa hv mtaa wa Agrey kuna raia toka kila kona ya Africa wanapiga mishemishe pale, wanaijeria, waganda, wa sudani na ukifika dukani kwao wanaongea kiswahili safi kabisa.

Na ukifika mtaa wa Agrey utakuta ndinga za kila aina zimepaki pale.

Mtaa wa Agrey ni mtaa wa mishemishe na hakuna vibaka ni watu wastaarabu tu tofauti na mtaa wa kongo uliojaa vibaka.

Mtaa wa Agrey umetoka kuwa mtaa wa madimbwi na kuwa mtaa uliopigwa lami na kuwa mtaa wa kijanja mjini ambao uko opposite na klabu namba mbili kubwa zaidi Afrika Simba sports club baada ya Al ahly ya Egypt.

N:B, Mtaa wa Agrey ni mtaa unaoongoza kwa kutembelewa na pisi kali Tanzania. Pia utakuta pisi kali zinaongea ki zambia, ki congo, kimalawi, kiganda, kinyarwanda, kikuyu, kiluhya, kikalenjini cha Kenya etc. yani utakutana na pisi za kila kona ya Africa, yani pale wewe jipozisheni tu vizuri utachukua, utaweka pazuri tu kimataifa.

Kama ukifanikiwa kupata fremu mtaa wa Agrey hujakosea
 
Upande wa pili wa Barabara ya Msimbazi unajenga sana. Ukianzia hapo Bank ya Wakenya pote panajengwa vitu vipya tu
 
Ten ukisogea sogea hapa karibu na hili kanisa la Lutheran ndo kuna kwenda kasi kwa speed ya 4G.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…