KERO Mtaa wa Kitunda - Machimbo tuna kero ya umeme, unakatika zaidi ya mara tatu kwa siku, TANESCO hawatupi majibu ya kueleweka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Huku mtaani kwetu Machimbo, Kitunda hapa Dar es Salaam tuna kero ya umeme, unakatika takribani kila siku, kuna wakati unakatika na kurejea ndani ya muda mfupi na kuna muda unakatika muda mrefu.

Tunapata hasara kubwa hasa sisi tunaotegemea biashara zinazohusisha nishati ya umeme, mbali na hapo hali ya hewa ilivyo sasa, joto ni kali, kisha kama hauna umeme basi ndani ya nyumba hakukaliki.

Nimekuwa nikifuatilia kuanzia Novemba 6, 2024 na kuendelea mpaka Desemba hii, mambo ni yaleyale, kata – rudisha, kata rudisha.

Kinachoshangaza upande wa pili wa eneo tulilopo sisi, Kitunda Center wao hawana shida kama ya kwetu, tumekuwa tunapiga simu TANESCO kuripoti, mara zote wanasema kuna tatizo la kiufundi umeme utarejea kama kawaida baada ya muda.

Kibaya zaidi muda mwingine hasa wikiendi wanakata umeme kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Wale wanaohifadhi vyakula kwenye majokofu kama vile nyama na Samaki wamekuwa wakipata tabu ya vyakula kuharibika.

Hivi TANESCO mbona mnatuchukulia poa sana au kwa sababu huku hakuna Viongozi wakubwa wa Serikalini?

Pia soma ~
Naibu Waziri: Poleni Wakazi wa Kitunda kwa changamoto ya umeme, kuna hitilafu zinazojitokeza katika Miundombinu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…