Mtaa wa Mvita, Dar es Salaam

Mtaa wa Mvita, Dar es Salaam

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Mtaa wa Mvita

Hapo nilposimama kupiga picha hii ndipo unapoanza Mtaa wa Mvita ukikutana na Mtaa wa Amani.

Mbele ya mtaa huu na ndiyo mwisho wa mtaa, Mvita unakutana na Mtaa wa Msimbazi.

Miaka hiyo Msimbazi ilikua barabara moja tu. Msimbazi na Mafia kulikuwa na nyumba ya bibi yangu Bi. Asha bint Farijala.

Nyumba hii ilivunjwa miaka ya 1970 na bibi alipewa fidia akanunua nyumba Temeke.

Wakati mimi nakua Dar es Salaam mtu anaweza kusimama Mtaa wa Msimbazi na Kitchwele (Barabara ya Uhuru) na akaona hadi Barabara ya Morogoro. Watu walikuwa wachache na magari hali kadhalika.

Mtaa wa Mvita ni mtaa mdogo lakini udogo wa kuwa na nyumba chache haukuwa kitu kwani mtaa huu umaarufu wake ulitokana na kuwa na tawi kubwa na maarufu la chama cha TANU.

Mtaa wa Amani karibu sana na ilipokuwa ofisi ya TANU hapo Mtaa wa Mvita kulikuwa na Madrasa ya Sheikh Hassan bin Ameir.

Umaarufu wa Madrasa hii katika miaka ile ya 1950 ni kuwa mara kwa mara Nyerere akiongozana na Abdul Sykes na Dossa Aziz walikuwa wakienda pale kwa shauri hili ama lile kutaka kauli ya Sheikh Hassan bin Ameir katika kupgania uhuru na kuisukuma mbele TANU.

Hawa walikuwa wakifika pale katika madrasa basi sheikh atafunga kusomesha na atawaruhusu wanafunzi kwenda nyumbani ili papatikane utulivu katika mazungumzo na wageni wake hawa.

Mitaa hii haikuwa kama unavyoona kwenye hizo picha hapo chini. Barabara hazikuwa na lami wala hapakuwa na magorofa na magari yamaeegeshwa kama hivyo.

Nyumba zilikuwa za chini na zimeezekwa na madebe na nyingine makuti. Nyumba za Kariakoo zilikuwa kama unavyoona kwenye picha ambayo inaonyesha Soko la Karikakoo na Kituo Cha Polisi cha Msimbazi.

Bahati mbaya leo historia hii ya Mtaa wa Mvita na Mtaa wa Amani haifahamiki wala yale yaliyopitika katika mitaa hiyo hayafahamiki.

1663820064866.png
1663820114542.png
 
Hakika Waislamu walichangia 98% kupigania uhuru wa nchi yetu.

Bila wao sijui tungelikua wapi leo.
Mlo...
Uhuru ungepatikana hata bila ya historia hii lakini ungechelewa sana.

Dr. Vedasto Kyaruzi amepata kumwambia Juma Mwapachu kuwa kama si mipango aliyopanga Hamza Mwapachu na Abdul Sykes uhuru usingepatikana mwaka wa 1961.

Mtaa wa Mvita

Hapo nilposimama kupiga picha hii ndipo unapoanza Mtaa wa Mvita ukikutana na Mtaa wa Amani.

Mbele ya mtaa huu na ndiyo mwisho wa mtaa, Mvita unakutana na Mtaa wa Msimbazi.

Miaka hiyo Msimbazi ilikua barabara moja tu. Msimbazi na Mafia kulikuwa na nyumba ya bibi yangu Bi. Asha bint Farijala.

Nyumba hii ilivunjwa miaka ya 1970 na bibi alipewa fidia akanunua nyumba Temeke.

Wakati mimi nakua Dar es Salaam mtu anaweza kusimama Mtaa wa Msimbazi na Kitchwele (Barabara ya Uhuru) na akaona hadi Barabara ya Morogoro. Watu walikuwa wachache na magari hali kadhalika.

Mtaa wa Mvita ni mtaa mdogo lakini udogo wa kuwa na nyumba chache haukuwa kitu kwani mtaa huu umaarufu wake ulitokana na kuwa na tawi kubwa na maarufu la chama cha TANU.

Mtaa wa Amani karibu sana na ilipokuwa ofisi ya TANU hapo Mtaa wa Mvita kulikuwa na Madrasa ya Sheikh Hassan bin Ameir.

Umaarufu wa Madrasa hii katika miaka ile ya 1950 ni kuwa mara kwa mara Nyerere akiongozana na Abdul Sykes na Dossa Aziz walikuwa wakienda pale kwa shauri hili ama lile kutaka kauli ya Sheikh Hassan bin Ameir katika kupgania uhuru na kuisukuma mbele TANU.

Hawa walikuwa wakifika pale katika madrasa basi sheikh atafunga kusomesha na atawaruhusu wanafunzi kwenda nyumbani ili papatikane utulivu katika mazungumzo na wageni wake hawa.

Mitaa hii haikuwa kama unavyoona kwenye hizo picha hapo chini. Barabara hazikuwa na lami wala hapakuwa na magorofa na magari yamaeegeshwa kama hivyo.

Nyumba zilikuwa za chini na zimeezekwa na madebe na nyingine makuti. Nyumba za Kariakoo zilikuwa kama unavyoona kwenye picha ambayo inaonyesha Soko la Karikakoo na Kituo Cha Polisi cha Msimbazi.

Bahati mbaya leo historia hii ya Mtaa wa Mvita na Mtaa wa Amani haifahamiki wala yale yaliyopitika katika mitaa hiyo hayafahamiki.

View attachment 2364218View attachment 2364219
Kwanini uliitwa Mtaa wa Mvita?
 
Back
Top Bottom