Mtaa wa Pili Kaeni Chonjo: Msiyempenda Anakuja

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Ndani ya wiki mbili zilizopita, Kamati ya Usajili ya Simba SC imekua iki haha huku na kule kuleta washambuliaji mbalimbali kwa ajili ya kuja kufanya majaribio.. ili wakifanikiwa wawe miongoni mwa wachezaji wachache sana waliowahi kuitumikia timu bora kuwahi kutokea ukanda wa CECAFA, Simba SC.
Lengo la zoezi hilo lilikua ni kupata deadly straika [20+ goal's holder] wa kuongeza nguvu kidooogo katika safari yetu ya kuchukua makombe 4 + Ngao 1 ya Hisani msimu ujao.. makombe hayo ni;

1. Vodacom Premier League
2. Kombe La Shirikisho a.k.a FA Cup
3. Mtani Jembe 3
4. Kombe La Muungano
5. Ngao ya Hisani

Kati ya washambuliaji wote ni Kelvin Ndayisenga pekee ndiyo aliweza kuzikonga nyoyo za Benchi la Ufundi, Mashabiki n.k. Hii ilitokana na kiwango cha ajabu saaaana alichokionesha katika mechi ya majaribio.
Kiwango alichokionesha hakikuiacha salama kambi ya mtaa wa pili, kwani kiliwafanya wawe wanapiga dua mchana na usiku ili Kelvin asitue Msimbazi.

Mwanzoni ilionekana ni ngumu kutua, baada ya Kelvin kutaka day zito.. lakini sasa hali imebadilika kwani Uongozi umeamua kuvunja kibubu na kumpa kila anachotaka ili aje kuitumikia Simba SC.. na mda si mrefu atatua Bongo kusaini mkataba.

".. kwa ujio huu wa kelvin a.k.a tormentor nadiriki kusema ile jig-saw puzzle iliyokua ikitusumbua vichwa, sasa imekamilika rasmi.. na 12/09/2015 ifike mapema" ~ sembo

Kwa Matomaso: http://salehjembe.blogspot.nl/2015/08/simba-yaachana-na-wasenegali-yamrudisha.html?m=1
 
..umekuja mbio sn; em tuambie anatokea timu gani huyo? record zake zikoje? tatizo hii mambo yakumwaga misifa kibao kwa mchezaji af akienda uwanjani anaogopa kugusa mpira hamjaanza leo..tuwekee hizo record tujionee mjomba..
 
..hiyo link inanigomea kufunguka..
 
sembo umeanza tena na stor zako za hao mastraika feki...emu weka walau rekod zake tuone
 
..umekuja mbio sn; em tuambie anatokea timu gani huyo? record zake zikoje? tatizo hii mambo yakumwaga misifa kibao kwa mchezaji af akienda uwanjani anaogopa kugusa mpira hamjaanza leo..tuwekee hizo record tujionee mjomba..

Nachojua;
1. Anatoka Burundi
2. Umri miaka 25
3. Rekodi akiwa Tanzania, Mechi 1/Goli 1 [hapa ni kama Ronaldo vile]
4. Player Rating, katika mechi iliyopita 10/10

Alafu, Inaonekana Mkuu hata mpira hufatilii, Siku ya Simba Day 08/08/2015 alitupia goli la kideoni, nadhani litakua goli bora la mwaka la FIFA [asante Azam TV kwa kufanya lionekane dunia mzima]. huku akionesha kiwango cha hali ya juu saaana, tuliokua uwanjani ni mashahidi.
 
sembo umeanza tena na stor zako za hao mastraika feki...emu weka walau rekod zake tuone

Mkuu rekodi zake haziko vizuri saana.. Tangu akiwa na miaka 20 alikua 1st eleven ya AO Bujumbura.. na waligoma kabisa kumuuza.. baada ya kuona pengo lake wanaliziba vipi?! Ni sawa na Barcelona kumuuza Messi.. jambo hilo haliwezekani.. Ila thanks GOD sasa anatua Msimbazi.. Mtaa wa Pili wajipange kisawasawa.
 
Mkuu, Isije kuwa ya Danny Serunkumma. Mchezaji ni mpaka acheze ndio ujue kama mbivu au mbichi.
 
Mikia mtaelimika lini ili kumprove wrong rage kwa kuwaita mbumbumbu!
 

..nahisi utakua kiongozi flani simba,haiwezekani umkubali mtu kwa hilo goli moja alilofunga simba day..hiyo timu aliyotoka inaitwa AO iko burundi au wapi ht sijawai kuiskia.! record zake huna.! yani ww siasa za ccm na chadema ndio unazileta simba...ouh..!
Hakika Tanzania tutasubiri miaka 200 angalau tu kwenda AFCON..by the way mi simba pia ila hii style ya ushabiki kipofu inatakiwa iachwe simba iende mbele,amekuja msenegali mkapiga kelele wee siku imefika hola,naskia tena leo mnamjaribisha mwingine ngoja tuone..
 
Mkuu, Isije kuwa ya Danny Serunkumma. Mchezaji ni mpaka acheze ndio ujue kama mbivu au mbichi.

Uko sawa Mkuu.. Ila nadhani mchezaji wa kupewa mkataba ni yule ambae anakuja kufanya majaribio Benchi la Ufundi linalidhika nae, mnampa mechi ya majaribio anafanya mambo.. Na Kevin ni mchezaji wa aina hiyo.
 

Dah.. kumbe Mkuu ni Mwana Msimbazi mwenzangu?! Mbona unakua mgumu sana kuelewa.
Sasa sijui mfanyiwe nini wana msimbazi wenzangu mridhike.. Danny Serunkuma alisajiliwa bila kufanyiwa majaribio, yaliyotokea wote tunajua.. mkaanza kupiga kelele kua usajili unafanyika kwa kuangalia rekodi.
Uongozi ukaona isiwe inshu, msimu huu mchezaji kwanza unafanyiwa majaribio ndo unasajiliwa.. Kevin kaja, kafanya vyema mazoezini na katika mechi.. Kwanini asisajiliwe?! Hivi nyie binadamu mfanyiwe nini ndo mridhike.
12/09/2015 ligi kuu inaanza, Kevin akichemsha una haki ya kunyoosha kidole.. ila kwa sasa Kevin is innocent until proven guilty.
Kuhusu timu yake ingia Google, andika Athletic Olympic FC, inashiriki Bujumbura Premier League.
 

..umekiri mwenyewe rekodi zake sio nzuri, ss ww huoni unatujaza matumaini ambayo hayapo.? anyway,let's wait..
 
..umekiri mwenyewe rekodi zake sio nzuri, ss ww huoni unatujaza matumaini ambayo hayapo.? anyway,let's wait..

Niliposema sio nzuri nilimaanisha.. Hakuna rekodi sahihi katika mitandao.. mfano, nikikuambia nipatie rekodi za Busungu misimu mitatu iliyopita.. Jibu lake litakua sio nzuri.. Kwa maana kua hazipatikani, japo ni Bonge la Straika.
 
Nyie mnaanza ligi zikibaki mechi 3 za kumalizia ligi,mkuu ai utasubiri sana

Haha.. Mkuu tunaanza na spidi ya kasi katika mechi 4 za mwanzo, katika mechi ya 5 ambayo tunakutana na mtani, tunabadili giaa angani na kuweka super sonic speed ambayo ndio tutamaliza nayo ligi mwakani.. Pia kumbuka kabla hatujamaliza ligi tutakua tushakomba Mtani Jembe 3, Kombe la Muungano na Kombe la FA.
 
Kwa mamlaka niliyojipa mwenyewe nakuteua rasmi Sembo kuwa msemaji rasmi wa Simba ktk mitandao na social media zote. Majukumu yako yatahusisha kutoa taarifa, ufafanuzi na maelezo kuhusiana na bidhaa zote za Simba kwa maana ya timu zote na huduma mbalimbali zitolewazo na Simba. Umekuwa ukifanya kwa kuilezea timu kuu lakni kwa uteuzi huu utapaswa kuijulisha dunia kuwa Simba ni Klabu ya Michezo mmbalimbali sio kama hizi timu nyingine ambazo zimeshindwa hata kuwa na timu moja ya maana ya vijana kwa ajili ya kuendeleza vipaji.

Aidha maaandalizi yanaendelea kufanywa ili uweze pia kuwa Admin. wa social media kadha wa kadha zitakazoanzishwa.

Angalizo: Kwa kuwa utakuwa msemaji rasmi wa mitandaoni, unatakiwa kuacha mara moja kutoa taarifa ambazo hazijathibitishwa au mbwembe zilizopitiliza zenye lengo ya kuongeza chumvi ili kupotosha, kuhadaa, kutokusema ukweli.

Kazi hii ni ya kujitolea na inaanza mara moja!!!
 

Haji manara walikosea sana kumweka pale kuwa msemaji wa mikia fc...ulistahili uwepo wew pale,,,lait wangetumia mfumo wanao tumia sasa kiwafanyia wachezaji majaribio ndo wasajiliwe wangefanya hivyo na kwawasemaj wa klabu walah wew usingukuwa na mpinzan


By the way matokeo ya leo,,wazanzibar 2 mikia fc 0
 
yule ni straika ila anahitaji mazoezi sana
 

watu kama hawa usihangaike nao sembo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…