Mtaa wa Sheikh Yusuf Badi Lindi

Mtaa wa Shaikh Badi
Moja kati ya mitaa maarufu sana katika mji wa Lindi, wenyeji wanauita pia mtaa wa Himo kwa kuwepo mgahawa wa Himo 1, wa Msomali kutoka Himo, ndugu Yusuf.
Kwa hadhi, juhudi na kazi aliyofanya Shaikh Badi anastahiki kuenziwa na kukumbukwa.
Historia tuliyojifunza leo inatupa wasaa wa kujmua mmoja tu kati ya wasomi wa Kiislamu kutoka Lindi aliyepelekea kubadilika kwa muelekeo wa kisiasa wakati ww ukoloni. Muelekeo ambao ulipelekea mji wa Lindi kuunga mkono harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika.
Katika mtaa huu anaishi pia Salum Barwani, mwanasiasa machachari wa Lindi ambaye alipata kuwa mbunge wa Lindi mjini kutoka chama Cha CUF
Akina Barwan wana historia ndefu ya siasa katika Tanganyika na Zanzibar
Ali Muhsin Barwan aliyapata kuwa waziri wa mambo ya nje kutoka chama Cha Zanzibar nationalist Party alikuwa mmoja wa wanasiasa wenye uwezo wa ajabu.
Kwa upande mwengine Ali Muhsin Barwan ana uhusiano na miji ya kusini -Lindi na Mtwara ambako ndiko walipotoka Bibi zake
Shukran shaikh Muhammad Said kwa historia ya Shaikh Badi.
 
Hivi mwaka 1955 kulikuwa na serikali hasaa yenye nguvu ya kukataza maandamano ya kumpokea Nyerere mjini?

Serikali ipi? Chini ya kiongozi yupi? Hebu fafanua hapo sheikh
Serikali ya kikoloni chini ya gavana Edward Twining.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…