Mtaa wa wafugaji wa kuku

Mgombezi

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2009
Posts
610
Reaction score
181
Wana JF

Mimi ni mfugaji; nimeanza kufuga kuku wa nyama (broiler) miezi michache iliyopita. Nimeamua kuanzisha thread hii ambayo lengo lake ni kubadilishana uzoefu katika ufugaji bora wa kuku.

Naamini hapa jamvini kutakuwa na wafugaji wenzangu pamoja na wataalamu wa mifugo; ambapo tutaweza kushirikiana na kusadiana katika kutatua changamoto mbalimbali katika sekta hii.

Changamoto mojawapo katika ufugaji wa kuku ni magonjwa yanayoweza kusababisha vifo kwa kuku; ndiyo maana nimeonelea vyema kuleta thread hii kwa JF DOCTOR ili tuweza kuwapata madaktari wa mifugo. Kama itakuwa sio mahala pale basi wadau tunaweza kutoa comments zetu za sehemu husika ya thread hii. Nilishawahi kutoa ombi la kuanzishwa jukwaa la KILIMO na UFUGAJI ili tuweze kulitumia hilo kwa mada husika, ni matumaini yangu kwamba moderators wanalifanyia kazi ombi hilo.

Ni matarajio yangu kwamba kupitia thread hii tutaweza kuwa na SHAMBA DARASA, kwani tunaweza kuleta changamoto tunazokutana nazo na kupata uzoefu wa wngine au ushauri wa kitaalamu katika kutatua tatizo.

Tarehe 27 Feb 2011 - nimeweka Kuku wa Nyama (broiler) 400 bandani. Niliweka maji yenye glucose kwa muda wa takribani masaa 4 pamoja na chakula (starter). Baada ya hayo masaa manne niliweka maji yenye dawa (Hipralona ENRO-S), kutokana na ushauri wa mtaalamu wa mifugo kwamba wakati mwingine vifaranga huanguliwa wakiwa na ugonjwa wa Salmonellosis. Ninaendelea na dawa hii mpaka leo (siku ya 3).

Kwa siku ya leo (siku ya 3), nimepoteza kifaranga kimoja na alikuwa na dalili za ugonjwa kama nilivyoonyesha katika picha. Vifaranga wngine watano wana dalili za ugonjwa huo. Nimekuwa nikiona vifaranga katika siku 5 za mwanzo wanakuwa na ugonjwa wenye dalili hizi na wakati mwingi kupoteza vifaranga vichache. Nimeamua kuleta hapa jamvini ili niweze kusaidiwa;
  • Je huu ni ugonjwa gani
  • chanzo chake
  • tiba au kinga yake.



Ni matumaini yangu kwamba wafugaji pamoja na wataalamu tuliopo hapa JF tutatoa ushirikiano katika kusaidiana kupunguza hasara ambazo zinawezekana kwa kupeana ujuzi na maarifa zaidi. Wakati mwingine upatikanaji wa mtaalamu wa mifugo huwa ni mgumu katika baadhi ya maeneo.

Nawakilisha
 
Mode; naomba hii thread hapa u-delete kwani nimeamua kuhamishia jukwaa la biashara.

Kwa yeyote anayetaka kuchangia naomba uende jukwaa la biashara, kama itakuwa bado haijawa deleted.
 
Asante bwana. Wafugaji tupo. Nami huwa nauona ugonjwa huo. Ila nadhani ukitumia dawa nzuri mwanzoni huwa haupatikani. Jitahidi kupata ushauri wa daktari.
Tuendelee kuwasiliana kwa jonasmpango@yahoo.co.uk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…