Mtaala Mpya wa Elimu ya Msingi uko Tayari. Wizara ya Elimu mbona haitaji Lugha rasmi ya kujifunzia?

Kama unaijua Kiswahili pekee utakosa maarifa na connection nyingi zama hizi.

Nitajie connection tano za maana ambazo umezipata kwenye maisha yako kwa sababu ya kiingereza( be honest) na Mimi nitakutajia ambazo nimezipata kwa nguvu ya lugha ya kiswahili
 
Write your reply...hapo bora kiarabu tupate kazi dp world
 
Nitajie connection tano za maana ambazo umezipata kwenye maisha yako kwa sababu ya kiingereza( be honest) na Mimi nitakutajia ambazo nimezipata kwa nguvu ya lugha ya kiswahili
Connection niliyoipata ni kuwa na uwezo wa kusoma na kujifunza vitu ambavyo havipatikani kwa Kiswahili na ningekuwa najua Kiswahili pekee ningekuwa mjinga sana wa vitu hivyo ambavyo ni muhimu kwangu.

Hata JF the bold amepata umaarufu na anapiga pesa hadi sasa kwa kuwa anatoa contents ,documentary na madini kwenye site za kingereza yeye anapangilia vizuri na kutafsiri kwa Kiswahili kisha anapiga pesa kwa watu.

Kwa kumalizia kitu ambacho mimi kikiwa hakijanipa connection nyingi zaidi haimaanishi kuwa hakina connection wala manufaa mengi na kiuhalisia ukiweka kwenye mzani lugha ya Kiswahili na Kingereza ipi ukijua sana ni dili na inakupa manufaa mengi Kingereza kinashinda hili jambo liko wazi hapingi mtu isipokuwa mpaka awe mjinga.
 
Umejitetea sana wacha nikuache tu
 
Jamani kuna utofauti mkubwa sana Kati ya kujifunza kwa kingereza na kujifunza kingereza. Niwazi kuwa kutumia lugha kufundishia haisababishi kujua hiyo lugha kwani hata kiswahili chenyewe watoto wanajua kuongea tu ila kujieleza Ni shida. Nafikiri msisitizo uwepo jinsi ya kufundisha lugha ya kingereza kama lugha sio somo. Miaka sita ya kusoma kwa kingereza mbona haisaidii wanafunzi kujua kingereza Huko mavyuoni kuna ushahidi. Hii inamaana kuwa shida sio matumizi ya lugha ..shida Ni ufundishaji wa lugha yenyewe. Walimu wenzangu mtanisaidia hili. Kuna watoto wanaofanya vizur sana sana elimu ya awali kwakuwa wanatumia lugha wanayoijua lakini wakifika secondary watoto hawahawa hufeli..sasa Tanzania imewaandaa vipi Hawa watoto kujifunza kwa lugha ya geni. Walimu wanaofundisha kingereza primary wanafundisha kuhusu kingereza na sio kingereza chenyewe. Watoto humaliza la Saba wakijua the rules of the language lakini application hakuna. Walimu wa lugha hawana maandalizi mazuri ya kufundisha multilingual classrooms. Halafu pia sekondari swala la lugha limeachiwa mwalimu wa kingereza....so funny maana mwalimu wa kingereza pia hawezi fundisha all the content knowledge. Kama tunataka tatua hili tatizo tuanze na walimu wa lugha vyuoni. Infact Ingependeza walimu wa lugha kufanya mtihani wa lesseni kabisa sababu kingereza sio biology na kufundisha kwa kiingereza ni ujuzi mara mbili, kwanza lugha yenyewe pili kutumia lugha yenyewe.
Hapa sijazungumzia juu ya watoto wa vijijini ambao kiswahili tu Ni changamoto... sasa kingereza si ndo watakimbia shule kabisa. Wachina wanajua kingereza sababu wanafundishwa kingereza kama lugha sio Kama somo. Let's not sacrifice primary education for the sake of learning a foreign language. Wale wa English medium wanaweza sababu kuna factors nyingi ikiwamo resources available quality za walimu, ukubwa wa madarasa, pia support kutoka kwa wazazi. Hata hivyo Hawa waenglish medium pia Ni juhudi za mwanafunzi mwenyewe... it's a struggle to teach and learn in a foreign language during the early years of school. Tafiti zinaonesha hivo na walimu hapa mtakubaliana na Mimi.
Key point to take
Kutumia lugha kufundishia sio kufundisha lugha yenyewe. Nakufundisha lugha Kama somo sio kufundisha lugha yenyewe. Kujifunza lugha ni kujifunza lugha yenyewe Kama ilivyo kuendesha gari ...kujua juu ya magari haimaanishi unaweza endesha gari. Unahitaji kujifunza kuendesha gari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…