KERO Mtaala mpya wa Kidato cha Kwanza 2025, masomo yanahimiza ICT lakini shule nyingi hakuna ICT ROOM na Watoto hawana msingi

KERO Mtaala mpya wa Kidato cha Kwanza 2025, masomo yanahimiza ICT lakini shule nyingi hakuna ICT ROOM na Watoto hawana msingi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Serikali ina haja ya kutazama mpya juu ya suala la mtaala ulioboreshwa wa kidato cha kwanza 2025, kwa hakika mtaala huo haukidhi vigezo kwa mtoto wa kidato husika kwa sababu baadhi ya mada mfano Baiolojia alikuwa anajifunza kidato cha pili hadi cha nne lakini zimerudishwa form one.

Masomo mengi hata English Language yanahimiza kutumia ICT lakini shule nyingi hakuna ICT ROOM pia hata watoto hawana msingi na uelewa wowote kuhusu ICT hivyo contents za form one hazieleweki kwa mwanafunzi na ni ngumu kuzi masta.

Kwanini Serikali imeharakisha sana kulazimisha mtaala utumike wakati hilo jambo lilitakiwa lichukue hata miaka mitano au kumi ili lianze kutekelezwa.

Shida iliyopelekea mtaala wa kidato cha tano mwaka 2024 kusitishwa ni zilezile zinazotakiwa zitumike ili na huu usitishwe maana hawajatatua zile changamoto.

Elimu ni msingi kwa taifa lakini sasa hivi inachezewa sana kama haja ilikuwa ni mtoto akimaliza ajiajiri kwanini masomo ya KILIMO na KOMPYUTA hayakuwa ya lazima tofauti na Kiswahili na Geografia eti ni ya lazima.

NIOMBE JAMIIFORUMS JUKWAA LA HABARI MPAZE SAUTI JUU YA HUU MTAALA MPYA MAANA HAKUNA HATA VITENDEA KAZI KTK SHULE NYINGI SANA NCHINI.
 
Tukisema tuna wasiwasi na elimu ya tanzania na ufaulu mnasema tuna wivu.
 
serikali inahaja ya kutazama mpya juu ya suala la mtaala ulioboreshwa wa kidato cha kwanza 2025, kwa hakika mtaala huo haukidhi vigezo kwa mtoto wa kidato husika kwasababu baadhi ya mada mfano Baiolojia alikua anajifunza kidato cha pili hadi cha nne lakini zimerudishwa form one.

Masomo mengi hata English Language yanahimiza kutumia ICT lakini shule nyingi hakuna ICT ROOM pia hata watoto hawana msingi na uelewa wowote kuhusu ICT hivyo contents za form one hazieleweki kwa mwanafunzi na ni ngumu kuzi masta.

Kwanini serikali imeharakisha sana kulazimisha mtaala utumike wakati hilo jambo lilitakiwa lichukue hata miaka mitano au kumi ili lianze kutekelezwa.

Shida iliyopelekea mtaala wa kidato cha tano mwaka jana kusitishwa ni zilezile zinazotakiwa zitumike ili na huu usitishwe maana hawajatatua zile changamoto.

Elimu ni msingi kwa taifa lakini sasa hv inachezewa sana km haja ilikua ni mtoto akimaliza ajiajiri kwanini masomo ya KILIMO na KOMPYUTA hayakuwa ya lazima tofauti na Kiswahili na Geografia eti ni ya lazima.

NIOMBE JAMIIFOROMS JUKWAA LA HABARI MPAZE SAUTI JUU YA HUU MTAALA MPYA MAANA HAKUNA HATA VITENDEA KAZI KTK SHULE NYINGI SANA NCHINI.
Ndiyo maana nasema huu mtaala ni mzuri kwenye makaratasi ila utekelezaji utakuwa 0. Wewe kama miaka yote kuna shule kibao wanasoma alternative to practical, leo uniambie watoto wote wataweza kusoma yale yaliyomo kwenye mtaala huu ambayo mengine yanahitaji tool boxes, na computers n.k.
 
Niliongea haya pia, huu mtaala umewekwa kwa kukurupuka. Wamejifangia maamuzi wakahisi mtaala utakuwa sahihi
Honestly, sioni haja ya jufundisha coding kuanzia shule ya msingi. Mwanzo tulikuwa naTEHAMA wangeweka tu mipango mkakati mizuri katika somo la TEHAMA walau mtoto awe na uelewa na ICT lakini sio walichofanya sasa. Haya mambo yanahitaji muda sio kukurupuka tu
 
Serikali ina haja ya kutazama mpya juu ya suala la mtaala ulioboreshwa wa kidato cha kwanza 2025, kwa hakika mtaala huo haukidhi vigezo kwa mtoto wa kidato husika kwa sababu baadhi ya mada mfano Baiolojia alikuwa anajifunza kidato cha pili hadi cha nne lakini zimerudishwa form one.

Masomo mengi hata English Language yanahimiza kutumia ICT lakini shule nyingi hakuna ICT ROOM pia hata watoto hawana msingi na uelewa wowote kuhusu ICT hivyo contents za form one hazieleweki kwa mwanafunzi na ni ngumu kuzi masta.

Kwanini Serikali imeharakisha sana kulazimisha mtaala utumike wakati hilo jambo lilitakiwa lichukue hata miaka mitano au kumi ili lianze kutekelezwa.

Shida iliyopelekea mtaala wa kidato cha tano mwaka 2024 kusitishwa ni zilezile zinazotakiwa zitumike ili na huu usitishwe maana hawajatatua zile changamoto.

Elimu ni msingi kwa taifa lakini sasa hv inachezewa sana km haja ilikua ni mtoto akimaliza ajiajiri kwanini masomo ya KILIMO na KOMPYUTA hayakuwa ya lazima tofauti na Kiswahili na Geografia eti ni ya lazima.

NIOMBE JAMIIFORUMS JUKWAA LA HABARI MPAZE SAUTI JUU YA HUU MTAALA MPYA MAANA HAKUNA HATA VITENDEA KAZI KTK SHULE NYINGI SANA NCHINI.
Hivi vyama vya walimu ni basi tu lakini vilistahili vyote vifutwe!! Nimeona sehemu watu wanaicheka kada ya ualimu kwa kupewa semina ya mtaala mpya huku malipo ni elfu 3 tu tena inaenda kucover gharama za chai. Hakuna chama hata kimoja kilichopaza sauti kuhoji sababu ni nini hadi walimu kutopata stahiki zao kama sheria na kanuni za kazi zinavyotaka. Ila fanya mapenzi na mwanafunzi ndo utajua haki zinavyotafutwa.
 
Tumieni Vishkwambi..
Punguza kulialia..
 
Back
Top Bottom