Mtaala mpya wa ufugaji wazinduliwa

Mrs Gudman

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2015
Posts
613
Reaction score
1,297
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe leo tarehe 21 Machi, 2019 amezindua rasmi mtaala wa Kilimo uliohuishwa baada ya ule wa zamani uliofahamika kama mtaala wa kilimo mseto kuboreshwa

Akihutubia mamia ya wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Morena iliyopo Jiji la Dodoma, Mhandisi Mtigumwe amesema Mtaala huo ni matokeo ya mahitaji ya soko la ajira (Labour Market Need Assessment) yaliyofanywa na wataalamu waelekezi toka Chuo Kikuu Cha Iringa na kubaini umuhimu kwa jamii

Aidha Katibu Mkuu huyo amebainisha kwamba kulingana na maendeleo ya teknolojia kumekuwa na mahitaji makubwa ya wanafunzi wa Vyuo vya Kilimo kuwezeshwa kubobea katika fani au taaluma zao (field of specialization) hivyo mtaala huo umekuja wakati muafaka
Aidha Mtaala huo umehuishwa na kuingiza taaluma na moduli mpya katika nyanja za Ushirika katika Kilimo, Hisabati katika Kilimo, Mawasiliano, Mabadiliko ya tabianchi, Jinsia na Kilimo Endelevu; ili kuwajengea uwezo na umahiri wahitimu katika sekta ya Kilimo (Agriculture Production)

“Napenda kuwajulisha kuwa mtaala huu umezingatia kanuni za NACTE, hivyo ninayo furaha kusema kuwa tumefanikiwa kupata sio tu Mtaala Uliohuishwa bali pia ni Mtaala wenye moduli mpya sita zilizojaza nafasi ya moduli za Mifugo” alisistiza Mhandisi Methew Mtigumwe

Hata hivyo Mhandisi Mathew Mtigumwe alibainisha kwamba Mtaala mpya wa Kilimo (Agriculture Production) umehusisha moduli mpya zilizoingizwa katika tuzo ya taifa ya ufundi daraja la nne NTA Level 4: mbinu za msingi za mawasiliano Basic Communication Skills na hisabati katika kilimo Basic Mathematics in Agriculture; tuzo ya taifa ya ufundi daraja la tano NTA Level 5: menejimenti ya mazingira Environment Menagement na Kanuni bora za Ushirika katika kilimo Principles of Cooperatives in Agriculture; na tuzo ya taifa ya ufundi daraja la sita NTA Level 6: kilimo hai/endelevu Organic Farming na jinsia katika kilimo Gender in Agriculture

Mtaala uliohuishwa unalenga kutoa wagani tarajali wenye umahiri katika uzalishaji mazao kwa tija na hivyo kuchangia katika sera ya uchumi wa viwanda alisisitiza Mhandisi Mtigumwe

Awali Katibu Mkuu huyo alishukuru Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Shirika la LWR, Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania (SAT), Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi NACTE, Wakala wa uzalishaji na usambazaji wa mbegu za kilimo (ASA), Taasis ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanznia (TOSCI), Halmashauri za Wilaya, Makampuni Binafsi, Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Wizara ya Kilimo kwa kufanikisha upatikanaji wa mtaala huo

Aidha, Wakufunzi wetu wanahitaji kupata mbinu bora katika kutekeleza Mtaala mpya, mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia; haya ni maeneo mengine ya mashirikiano, nasi tuko tayari kushirikiana na wadau mliopo na wadau wengine alimalizia Mhandisi Mtigumwe.
MWISHO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…