Riseforchange
New Member
- Sep 1, 2022
- 1
- 0
Napenda kumshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema pia kukupa nafasi ya kufuatilia matini yangu kikamilifu
Pia shukran zangu za dhati nazielekeza kwa waasisi wa dawati la jamii forum stories of change
baada ya hapo twende pamoja katika mada yetu ya ukoo wa babu...
LEO TUNAGALIE KATIKA NYANJA ZIFUATAZO
1; UKOO WA BABU
2; KWANINI NI UKOO WA BABU
3; UTUMWA NA UKOLONI WA KIFIKRA UTOKANAO NA UKOO WA BABU
4; CHANGAMOTO KUBWA ZITOKANAZO NA UKOO WA BABU.
5; NINI KIFANYIKE ILI KULETA UKOMBOZI KWA WAHANGA WA UKOO WA BABU.
1; UKOO WA BABU ni mfuatano wa taratibu na kanuni za kimila na desturi ambazo alizifanya babu kama misingi asili yenye kuongoza kizazi hadi kizazi kilichopo chini ya ukoo huo.
MTAALA WA ELIMU YA TANZANIA NI UKOO WA BABU.
2; ZIFUATAZO NI SABABU ZA ELIMU YA TANZANIA KUONEKANA KAMA UKOO WA BABU
i) Mfumo wa elimu ya Tanzania ipo katika milolongo ya sheria za kale, hii inaamanisha kwamba mwanafunzi lazima asome madarasa kumi na mbili (12) mpaka kumi na nne (14) ndio aweze kupata elimu ya watu wazima yenye ufanisi wa kujitegemea yaani vyuoni.
ii) Elimu ya msingi na sekondari haitofautiani zaidi ya mabadiliko ya lugha hii ikiwa ni mfano dhahiri kwamba babu alifanya kitu fulani katika umri fulani na ikawa desturi kwamba lazima katika umri huo yeyote kwenye ukoo wake lazima afanye vivyo hivyo katika mitaala ya elimu yetu inaturejesha katika kilekile nilichojifunza msingi na kukifanyia marudio sekondari
iii) Mifumo ya vipimo vya uelewa na uthubutu ama viwango vya uelewa wa wanafunzi yaani mitihani, hapa pia pamejikita sana katika ukale mwanafunzi wa msingi anajifunza miaka saba masomo saba hadi tisa kwa sasa na zamani ilikuwa ni masomo matano, licha ya kujifunza masomo mengi hivyo tena kwa kipindi kirefu cha miaka saba au nane bado mwanafunzi anapimwa uwezo wake wa kukumbuka kwa maswali hamsini tuu bila kuzingatia somo moja amejifunza mambo mangapi; kibaya zaidi amesoma miaka saba anapimwa ndani ya masaa mawili na nusu tuu kwa somo na sikumbili tuu kwa miaka saba
iv) Vilevile kwa wale ambao wapo sekondari pia hupimwa hivyo kwa kwanzia masomo saba hadi kumi na moja au kumi na mbili nao pia ni miaka minne kwa masaa mawili na nusu hadi matatu
V) Kukariri madarasa; hii pia ni sifa ya ukoo wa BABU kwa yaliowahi kuwepo lazima yaendelezwe
vi) Kusoma anachokitaka mzazi na sio kipaumbele cha mtoto mwenyewe

Mtaala wa elimu umewafanya wanufaika kuwa watumwa na elimu waliopokea kuwa bwana wao
i) vijana wengi kwa sasa walio na elimu ya juu na vyuo imekua kilio chetu kwani taaluma waliyonayo haijawasaidia kuchanganua changamoto zao za maisha
ii) vigezo vya ajira kuzingatia uzoefu wa kutosha kazini kua kigezo muhimu katika udahili wa vijana umekua msumari wenye kutu kudunga vidonda vyao wakati ambapo wao wapo na uhitaji wa kunusuru majereha waliyonayo ndipo wanapotoneshwa na kuambiwa awe na uzoefu wa zaidi ya miaka kadhaa katika tasinia aliyoomba wakati huo mhanga hajawahi pata mahala popote pale pa kupata uzoefu huo
iii) elimu yao imewafanya baadhi ya vijana kuwa vipofu wasioweza kuona fursa zilizopo mafichoni zaidi ya zile zilizo wazi zenye upinzani mkubwa
iv) elimu ya sasa inajikita sana katika kuwapa sifa ya ufanisi wa makalatasi yaani vyeti vya ufaulu pasipo kuwapa ufanisi wa ubunifu katika vipaji ili kuendana na soko la dunia

i) Ukosefu wa vijana shujaa, shupavu na wenye uwezo wa kujiamini kujenga na kutetea hoja zao
ii) Kuwa na wimbi kubwa la wasaliti wengi wenye kujipendekeza kwa ajili ya masilahi yao binafsi badala ya kulinda maslahi ya taifa
iii) Mfumo huu umetengeneza vijana wasiotaka kuhoji kwanini zaidi ya kuiachia serikali yenyewe; mfano mzuri ni kwenye taasisi zetu utakuta mtu hajishughulishi ipasavyo zaidi ya kusema hii ni kazi ya serikali badala ya kujitoa ili kuweza kutetea maslahi ya serikali na taifa kwa ujumla

i) Serikali ipunguze urefu wa mda wa kusoma kitu kimoja kwa zaidi ya miaka kumi; hapa nazungumzia masomo yale yanayosomwa kwa shule za misingi haina sababu kurudiwa sekondari, ikumbukwe kwamba mtoto mdogo anaouwezo mkubwa wa kujifunza zaidi ya mtu mzima hivyo ikibidi vitu vya sekondari vipelekwe msingi ili kupunguza umri wa kijana ambaye ni nguvu kazi kupotelea kwenye elimu na baada ya hapo kuwa tegemezi badala ya kuwa tegemeo la taifa kwa ujumla.
ii) Ikiwezekana shule ziwe katika migawanyiko yenye kuibua vipaji vya wanafunzi mfano mwanafunzi ni muimbaji au anakipaji cha uandishi wa habari au utangazaji basi kwa elimu ya sekondari mwanafunzi huyo asome masomo ya lugha pekee ikiwezekana asome masomo matatu kiswahili ikiwa ni nguzo muhimu katika masomo yake; halikadhalika iwepo mfumo wa chuo katika ngazi ya sekondari ambayo itapunguza mlolongo wa miaka mitatu ya baadaye kusoma chuo inamaanisha miaka minne ya sekondari na chuo kikuu pia awe amehitimu; hivyo akisoma masomo matatu ndani ya miaka minne ya fani aliyonayo pia asomee fani hiyo hiyo kwa kipindi hicho hicho ili mwanafunzi au kijana aweze kuanza kujitegemea akiwa na miaka kumi na nane hadi ishirini na moja na sio kama leo mpaka miaka 28 bado kijana ni mzigo kwa wazazi serikali na taifa kwa ujumla
ii) Kama hapo juu mwanafunzi mwenye kipaji cha michezo ya mipira pia wafikapo sekondari wasome masomo matatu ya lugha na kujikita katika michezo kwani michezo ni ajira mfano mzuri ni MBWANA SAMATA ambaye mpira unamlipa vizuri zaidi
iii) Elimu ijikite katika mazingira na maisha halisi ya watanzania na Afrika kwa ujumla na sio kusoma historia ya uhuru, ujio wa wakoloni na mengine yanayofanana na hayo
iv) Elimu ya Tanzania iwape uhuru wanafunzi kufanya tafiti za tiba asilia kutokana na mimea (miti pori tuliyonayo kutokana na kuwepo kwa misitu asilia ya kutosha) vilevile utafiti huu uendelee na ufike mbali kwani kwenye kingo za mito na vilele vya milima bado kuna vitu vingi ambavyo havijagunduliwa ambavyo baadhi yao ni vivutio vya utalii na vingine vingi ni rasilimali muhimu katika maendeleo ya taifa letu
Kwa leo naomba niishie hapa kwa heshima na taadhima kubwa naomba kuwashukuru wale wote mlioweza kufuatilia matini yangu pia niwashukuru wote mtakaopokea na kuipenda matini yangu kumbuka kuipenda ndio nguvu kubwa ya kuleta matini nyingine
Mungu awabariki sana mmoja mmoja kwa imani yake 🙏🙏🙏

Upvote
0