Mashine ya kutotolea vifaranga unaweza kutumia hiyo transformer simplemind amesema inauzwa elfu 75. Kwa driers, power huwa kubwa kidogo, inabidi uwe na right transformer kufanya ifanye kazi. Hebu soma specifications za bidhaa zako kuhusu kiwango cha power, mara nyingi itakuwa imeandikwa namba ikifuatiwa na W au VA, mfano 1500W. Post hapa, unaweza kupewa ushauri wa transformer inayofaa.
hio transformer ya 75K inapiga mziki? mie niliyooiona ktk maduka ya hapo hapo round-about ya Uhuru + chingaz maximum ilikua 40K kwa mashine ya 1000W.Nunua transformer 220v to 110v zipo madukani bongo . Binafsi nilinunua moja miaka mitatu nyuma kwa ajali ya generator ambayo output 110v. Transformer inaweza kutumika kukuza 110v kwenda 220v au kupunguza 220v kwenda 110v . Bei wakati huo tsh 75000. Mitaa Dar siyafahamu vizuri kwa majina ila ikitoka railway station kuelekea mitaa ya kariakoo duka la vifaa vya umeme lipo kulia baada roundabout ya mwanzo na kabla kufika duka maarufu la kuuza kanga kwa jumla. Hope this will help.
va specification ni kipimo cha "mzigo jumla" transformer inaweza kuhimili. Haina maana mzigo ukiwa kiduchu mfano energy saver 10w itadhurika! Mfano transformer ya 1500 inaweza kuhimili bulb 150 za 10w au pump mbili za 1hp each au tv 20 za 75w au, washing machine 5 za 300w.