Mtaalam wa Nyasi asema asema nyasi za Uwanja wa Mkapa zina 'Fangasi' lakini bado zina ubora wa mechi kuchezwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Erick Mpoki ambaye ni mtaalamu wa masuala ya nyasi za uwanjani ambao kitaalamu wanajulikana kwa jina la “Football groundsman” amesema amekuwa akifanya kazi hiyo tangu mwaka 2012

“Elimu hiyo ameipata kwa Wachina na Wazungu kwa vitendo, tukiwa kwenye kazi ndipo tumejifunza hapohapo, hatukufundishwa darasani bali kwa kazi husika.”

Akizungumzia kuhusu majani ya uwanjani hasa yale ya asili ni muhimu kuyafuatilia muda mwingi.

Anasema “Mfano kama hii hali unayoiona hali ya nyasi kukauka si kwasababu ya kukosa maji bali ni ugonjwa wa ‘Fangas’.

“Aina ya majani haya (Uwanja wa Mkapa) yanaitwa ‘tough grass’, hali ya kuzidi kwa maji na kukosa mwanga wa kutosha inaweza kusababisha nyasi zipate magonjwa kama hayo ya ‘Fangas’, hapa ninamaanisha ukungu ambao unakaa kwenye nyasi.”

Akiulizwa kuhusunyazi za Uwanja wa Mkapa ambazo zinaonekana kupoteza ubora wake, amesema:

“Mvua za Januari ndizo ambazo huwa zinakuwa na madhara kwa kuwa zinaweza kunyesha mfululizo kisha kukawa hakuna jua la kutosha.”

Kuhusu matunzo amesema “Kuna dawa ambazo zinatumika kwa ajili ya kuulinda uwanja dhidi ya wadudu na magonjwa mbalimbali.”

Kuhusu Uwanja wa Mkapa kama unaweza kutumika kwenye mechi za wikiendi hii, amesema Uwanja wa Mkapa una ubora mzuri kuliko viwanja vingi vya Afrika.

"Nimeona hata mashabiki wanalalamika kuhusu ubora wa uwanja wetu, wasiwe na hofu, ubora ni mzuri japo ni kweli Uwanja hautakiwi kuchezewa mechi mara kwa mara, mfano ukiangalia nje, wenzetu viwanja vya Taifa havitumiki mara kwa mara."

Chanzo: DAR 24 Media
 
Naona anazungusha zungusha maneno tu, mbona haendi straight. Muonekano ukiwa mbaya unaharibu vibe ya mashabiki. Wanaweza kuharibu zaidi kwa kuumwagia maji mengi siku ya game wachezaji wakawa wanateleza tu kama game ya Simba na Coastal Union.
 
Erick Mpoki ambaye ni mtaalamu wa masuala ya nyasi za uwanjani ambao kitaalamu wanajulikana kwa jina la “Football groundsman” amesema amekuwa akifanya kazi hiyo tangu mwaka 2012

“Elimu hiyo ameipata kwa Wachina na Wazungu kwa vitendo, tukiwa kwenye kazi ndipo tumejifunza hapohapo, hatukufundishwa darasani bali kwa kazi husika.”

Akizungumzia kuhusu majani ya uwanjani hasa yale ya asili ni muhimu kuyafuatilia muda mwingi.

Anasema “Mfano kama hii hali unayoiona hali ya nyasi kukauka si kwasababu ya kukosa maji bali ni ugonjwa wa ‘Fangas’.

“Aina ya majani haya (Uwanja wa Mkapa) yanaitwa ‘tough grass’, hali ya kuzidi kwa maji na kukosa mwanga wa kutosha inaweza kusababisha nyasi zipate magonjwa kama hayo ya ‘Fangas’, hapa ninamaanisha ukungu ambao unakaa kwenye nyasi.”

Akiulizwa kuhusunyazi za Uwanja wa Mkapa ambazo zinaonekana kupoteza ubora wake, amesema:

“Mvua za Januari ndizo ambazo huwa zinakuwa na madhara kwa kuwa zinaweza kunyesha mfululizo kisha kukawa hakuna jua la kutosha.”

Kuhusu matunzo amesema “Wana dawa ambazo zinatumika kwa ajili ya kuulinda uwanja dhidi ya wadudu na magonjwa mbalimbali.”

Kuhusu Uwanja wa Mkapa kama unaweza kutumika kwenye mechi za wikiendi hii, amesema Uwanja wa Mkapa una ubora mzuri kuliko viwanja vingi vya Afrika.

"Nimeona hata mashabiki wanalalamika kuhusu ubora wa uwanja wetu, wasiwe na hofu, ubora ni mzuri japo ni kweli Uwanja hautakiwi kuchezewa mechi mara kwa mara, mfano ukiangalia nje, wenzetu viwanja vya Taifa havitumiki mara kwa mara."

Chanzo: DAR 24 Media
Paragraph ya mwisho ndio kaongea point ya msingi. Shamba la bibi hautumiki kabisa na kuishia matukio yote kuyapeleka Lupaso.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom