Mtaalam wa Saikolojia: Wapiga 'Kura' wengi hupenda Kuwapigia Kura wale wa Kwanza Kwanza 'Pichani' na wale wa Mwisho Mwisho 'huwaboa' katika Kuwapigia

Mtaalam wa Saikolojia: Wapiga 'Kura' wengi hupenda Kuwapigia Kura wale wa Kwanza Kwanza 'Pichani' na wale wa Mwisho Mwisho 'huwaboa' katika Kuwapigia

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
"GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE asikudanganye Mtu 'Kisaikolojia' Mpiga Kura yoyote yule Siku ile ya Kupiga Kura huwa na 'mwamko' mkubwa wa 'Kuwapigia' wale ambao 'Picha' zao ni za Kwanza Kwanza na hasa kwa Namba 1 mpaka 3 tu na kwa 'Mazingira' ya Siku husika wengi Wao huwa hawataki wala hawapendi 'Kujichosha' na 'Kujiboa' kuwapigia wale wa Mwisho Mwisho hasa Namba 12 hadi 14" Mtaalam wa Saikolojia.
 
Kama hakuna mabadiliko ni elimu tu ndo itolewe kwamba mgombea wako ni namba.
 
Hao ni wapiga kura wa zamani, wale vichwa vya kuku (wajinga), ambao hawajui wamchague nani mpaka wanaingia kituoni.

Siku hizi wananchi walio wengi wanayo elimu ya uraia, wameshafanya maamuzi mapema kabisa, ukiingia kituoni hata mgombea anayemtaka awe ukurasa wa tatu atatafutwa tu.

Kwahiyo NEC kama walidhani kumweka joni awe wa kwanza kutasaidia wamaulamba wa chuya.
 
Isikutishe Hawa jamaa dhamira zao mbaya tumeshuhudia zikiwarudia wenyewe, kila walifanyalo linabuma
Hapo unaposema kuwa dhamira yao mbaya sina uhakika napo hasa ukizingatia kuwa 'Kiitikadi' unaonekana ni Mpinzani uliyejazwa Sumu nyingi pia.
 
Hao ni wapiga kura wa zamani, wale vichwa vya kuku (wajinga), ambao hawajui wamchague nani mpaka wanaingia kituoni.

Siku hizi wananchi walio wengi wanayo elimu ya uraia, wameshafanya maamuzi mapema kabisa, ukiingia kituoni hata mgombea anayemtaka awe ukurasa wa tatu atatafutwa tu.

Kwahiyo NEC kama walidhani kumweka joni awe wa kwanza kutasaidia wamaulamba wa chuya.
Kwahiyo Mkuu unapingana na Mwanasaikolojia Mwandamizi (kama siyo Mbobezi) juu ya huu 'Utaalam' wake katika Saikolojia ya Picha na Kura?
 
Hii ngoma Lumumba nzima hawalali itakuwa huyo mwana saikologia.

Watu wameshaamua .... na ogopa sana watu wakishasema sasaa basiii!! CCM walijisahau sana ndani ya hii maika mitano wakajiona wapo juu ya kila kitu....

Sasa wenye nchi yao wameshastuka...

Kifupi CCM is no more!! Poleni kama nitawakera ila huo ndio ukweli wenyewe.
 
Hayo majina ya wagombea urais yamepangwa kimkakati, lakini ingekuwepo tume huru ya uchaguzi ule msemo wa wamwisho ndio mshindi ungekuwa na maana sana.
 
Kura haipigwi kama fasheni, kura inapigwa kwa mpangilio maalum, ukiwa na wazo lako kabla, then wakati ukifika unaenda kukamilisha/kutekeleza hilo wazo lako.

Hilo la kusema unaenda kumpigia wa kwanza huo ni mchezo wa kuigiza tu.
 
"GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE asikudanganye Mtu 'Kisaikolojia' Mpiga Kura yoyote yule Siku ile ya Kupiga Kura huwa na 'mwamko' mkubwa wa 'Kuwapigia' wale ambao 'Picha' zao ni za Kwanza Kwanza na hasa kwa Namba 1 mpaka 3 tu na kwa 'Mazingira' ya Siku husika wengi Wao huwa hawataki wala hawapendi 'Kujichosha' na 'Kujiboa' kuwapigia wale wa Mwisho Mwisho hasa Namba 12 hadi 14" Mtaalam wa Saikolojia.
Sasa kama mtu unapiga kura kwa jina moja tu unaboreka vipi? Hebu tarehe 28 ifike nikamtwange mtu nyundo ya kichwani haraka.

Kwanza nikiingia ndani ya chumba natolea macho jina la kwanza kisha nalisindikiza na bonge la tusi halafu naelekea mwishoni napiga tiki yangu halafu narudi tena kwenye jina la kwanza natukana kisha nakunja kura yangu naweka kwenye box.
 
Back
Top Bottom