Mtaalamu wa maswala ya Uti wa Mgongo na magonjwa ya mfumo wa fahamu kutoka Apollo kutoa huduma Dar

lyzbeth

Member
Joined
Mar 6, 2014
Posts
40
Reaction score
8
Kulingana na upungufu mkubwa wa wataalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu Tanzania, vichanga 1000 kati ya 4000 wanaozalliwa na tatizo la mfumo wa fahamu hupatiwa matibabu. Ina maanisha vichanga vilivyobaki hukua na tatizo la mfumo wa neva.

Kutokana na ongezeko la watanzania kwenda nje kutafuta matibabu yanayohusisha mfumo wa fahamu na uti wa mgongo, na uwepo wa uhitaji wa wataalamu wa magonjwa ya jinsi hii kwa wingi zaidi, ujio wa mkuu wa idara ya upasuaji wa uti wa mgongo na mfumo wa fahamu Dk. Alok Ranjan kutoka Hospitali za Apollo Hyderabad utakuwa na msaada mkubwa sana kwa Watanzania.

Watanzania wanashauriwa kutumia fursa hii kupata msaada wa kimatibabu kutoka kwa mtaalam huyu anayetambulika kimataifa.

Dk. Alok Ranjan kutoka Hospitali za Apollo Hyderabad atawaona wale wagonjwa wake wa awali aliowafanyia upasuaji katika hospitali ya Apollo ya mjini Hyderabad, lakini pia atatoa ushauri kwa wagonjwa wote hapa Tanzania wenye magonjwa yanayohusu mfumo wa fahamu na uti wa mgongo.

Kliniki hii ya siku 3 itaanza tarehe 11, nakuendelea tarehe 12 na 13 mwezi Novemba 2015 kwa muda wa nusu siku pale kwenye hospitali ya Hindu Mandal Dar es Salaam.

Kutokana na takwimu zilizotolewa mwaka 2012, kwa afrika mashariki ndani ya watu milioni 9 kulikuwa na mtaalam mmoja tu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu. Shirika la afya ulimwenguni (WHO) wanashauri kila nchi iwe na walau mtaalam mmoja wa magonjwa ya fahamu kuhudumia watu 100,000, ila kwa Tanzania wastani ulikuwa 1:13,000,000.

Watanzania wengi, hasa maelfu ya watoto, wanafariki kila mwaka kutokana na magonjwa kama kichwa kujaa maji (hydrocephalus), tatizo la kuzaliwa la fuvu (encepheloceles), matatizo ya kichwa yanayoleta shida kwenye uti wa mgongo na magonjwa mengine yanayofanana na hayo.

Kwa sasa Tanzania ina watalam tisa, ambao saba wanafanya kazi hospitali ya taifa ya muhimbili na wengine wawili wapo hospitali ya rufaa ya Bugando.

Kwa uzoefu wa kutibu zaidi ya wagonjwa 1500 wa kitanzania kwa miaka 10 iliyopita katika sekta ya ubongo na viungio vya uti, Dk. Alok Ranjan ni mzoefu mkubwa katika upasuaji wa mfumo wa fahamu kwenye hospitali za Apollo zilizopo Hyderabad. Amefanya zaidi operesheni kubwa 5000.

Amejikita zaidi katika upasuaji wa uti wa mgongo, uvimbe mdogo katika neve za mifumo ya fahamu katika maeneo ya ubongo, fuvu na uti wa mgongo, upasuaji wa uti wa mgongo kwa watoto, na upasuaji katika ateri. Dk. Alok Ranjan ni mwanachama katika kundi la mabingwa wa upasuaji wa mfumo wa fahamu kutoka Hospitali za Apollo na chini ya usimamizi wake ameweza kufanya zaidi ya operesheni 1000 kwa mwaka.

Katika hizo siku 3 za kliniki hiyo, Dk. Alok Ranjan atajikita kwenye maeneo ya msingi yanayohusisha matatizo magumu katika ubongo na mfumo wa uti wa mgongo kwa watoto na watu wazima pia. Upasuaji katika neva za mfumo wa fahamu, upasuaji katika mfumo wa uti wa mgongo, uvimbe, upasuaji mdogo wa mfumo wa fahamu kwa upande wa ubongo na uti wa mgongo, upasuaji katika fuvu,upasuaji kwa watoto kwenye viungio vya uti wa mgongo na ateri.

Hii sio ziara ya kwanza kwa daktari huyu mjini Dar es salaam. Huu ni mwendelezo wa ushirikiano na hospitali za Hindu mandal na unadhihirisha ni jinsi gani hospitali za Apollo zimejikita kwenye kutoa huduma bora za afya kwa watanzania wote ambao hawana uwezo/kipato cha kuwawezesha kwenda India kwa ajili ya matibabu.

Huduma hii ya kliniki, ni fursa ya pekee kwa wagonjwa wote wanaosumbuliwa na magonjwa yanayohusisha mfumo wa fahamu na uti wa mgongo, wenye uhitaji wa matibabu na hawana uwezo wa kusafiri kwenda hospitali za Apollo. Dk. Alok Ranjan atafanya kazi kwa karibu kabisa na timu ya madaktari wa hospitali ya Hindu Mandal kwa kutoka huduma madhubuti na ushauri bora katika afya.

Hivyo Watanzania wanashauriwa kuweka miadi mapema na hospitali ya Hindu mandal kupitia mawasiliano haya; +255 22 2114991 - 4.
 

Attachments

  • dr-alok-ranjan.jpg
    10.5 KB · Views: 122
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…