Mtaani kwako Bajaji inalaza bei gani kwa siku?

Upo mkoa gani? Kama upo Dar jichanganye njia ya Kigamboni (Ferry) kwenda Kisiwani hadi Kibada. Huwa naona hii njia bajaji zake huwa hazikai yaani. Zikifika tu ni kujaza na kuondoka. Uzuri wa hii njia pia nadhani bado hakuna daladala. Usichukue ile njia nyingine ya Kibada maana tayari ina daladala, namanisha uchague ile ya kupitia Kisiwani. Sijui sasa wakileta daladala huko mbeleni itakuwaje.
 
Hii ndio maana halisi ya mtu kuwa "Matured'.
Bravo!
 
Upo mkoa gani mkuu
 
Mimi nipo Dar ndugu zangu. Nataka route sehemu yeyote nje au ndani ya mji. Msaada please madereva wanasumbua sana.
 
Mimi nipo Dar ndugu zangu. Nataka route sehemu yeyote nje au ndani ya mji. Msaada please madereva wanasumbua sana.
Mbona hujaeleweka mkuu.. mwanzo umesema umenunua ujikimu na unaendesha mwenyewe ila biashara ngumu then unasema madereva wanasumbua duh ..

Na mbona Dar biashara uhakika tofauti na huku tulipo sisi
 
Wakati unataka kununua bajaji hazikuwa nyingi, ila bajaji zimeongezeka baada ya kununua weye [emoji849][emoji849]

Kweli kazi kukazana
ndio kawaida ya fursa wakati unawaona watu wanapiga pesa unaanza kujipanga ujiingize katika hiyo fursa lakini baada ya kujipanga unakuja kugundua ile fursa si fursa tena.
 
Ashindwe yeye sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…