Mtafutaji hachoki usife moyo

Mtafutaji hachoki usife moyo

Bolotoba

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
3,424
Reaction score
7,706
Maisha ni foleni na siku zinasogea pole pole Muamini MUNGU ipo siku utafanikiwa

Ata kama sio Leo "NDUGU" yangu Ila amini ipo siku utafanikiwa

Mungu wetu halali wala hasinzii "anasikia maombi yetu"

VUMILIA shida "Ila NB usivumilie dharau unaemmudu deal nae perpendicular" 🤣ukiendekeza unyonge ipo siku watakunyonga kabisa.

Biashara yako kuna siku inapata wateja kuna siku wateja wachache(tambua biashara nayo Ina kupanda na kushuka USIFE moyo).

Haupandi cheo we piga kazi tu. "USIFE moyo" uwezo wako ipo siku utaonekana kwa boss wako haina haja ya kujipendekeza kwa boss.

Unamadai mahakamani na bado kesi inazungushwa kama Unahaki (USIFE Moyo) haki itatendeka simu moja

Ni mwaka wa Tatu Huyo mwana dada unamfatilia Ila bado anakukatalia na Kila siku anakula hela zako🤣(USIFE Moyo) acha ujinga wewe(kwa jambo kama hili kukata tamaa ni mafanikio makubwa)

Mwisho, amini kabisa kwenye haya maisha kuna mwenzio mmoja mahali fulani anafanikiwa juu ya jambo ya Hilo hilo jambo unalolikatia tamaa. JIPE IMANI, PIGA MOYO Konde, endelea kutafuta.
 
Back
Top Bottom