Mtaji huu ni wa muhimu kuliko yote kwenye biashara!!

mwanawao

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2010
Posts
3,192
Reaction score
5,743
Watu wengi wakitaka kuanza kufanya biashara huwa wanaanza kufikiria kuwa na mtaji wa mamilioni shilingi. Katika fikra hizi wengi wa wajasiriamali wamekuwa wakijikuta wakizeeka na ndoto zao bila ya kuzifanyia chochote. Lakini kimtazamo ukiangalia kama ni mtu anataka kufungua biashara ya kuuza bidhaa kwa rejareja (retail business) lazima ataenda kwa wanaouza kwa jumla( whole sale). Anayetaka kuuza kwa whole sale lazima ataenda kiwandani kuchukua bidhaa. Sasa katika chain hii hata kama mtu huna mtaji lakini ukiwa na mtaji wa uaminifu ni rahisi sana kupewa bidhaa husika unayohitaji (kwa kukopeshwa) ukafanya biashara ukapata faida yako na hela ya tajiri ukarudisha.

Nina uhakika hata kwa benki tulizo nazo hapa nchini kama watu wangekuwa ni waamnifu kukopa na kurudisha hela na riba ya benki kama inavyotakiwa leo hii kusingekuwa na haya masharti lukuki yaliyowekwa kwa lengo la kumbana mkopaji.

Kwa wenye viwanda wakiwa waaminifu na kuzalisha bidhaa bora ambazo siyo feki, watajijengea uaminifu kwa wateja wao na bidhaa zao zitakuwa na ushindani mzuri kwenye soko na mitaji yao ingeongezeka kwa haraka.

Leo hii miradi mingi ya uwekezaji ndani ya nchi yetu kama uchimbaji wa madini, utalii, viwanda n.k. ingekuwa inafanywa kwa uaminifu, Taifa letu lingekuwa linatisha katika ukanda huu wa Afrika.

Natamani Watanzania tufikie mahali tuwe waaminifu, tuaminiane, tusaidiane, ili tuweze kuondokana na wimbi hili kubwa la umaskini linalotafuna Taifa letu.



 
Ni lazima tukubali kuwa ukweli na uaminifu ndio siri kubwa ya mafanikio si katika biashara tu bali katika kila kitu. Hizo ndizo nguzo kuu za ujenzi wa Social Capital. Na hii ndio siri kuu ya mafanikio waliyonayo watanzania wenzetu wenye asili ya asia. Ni lazima nasi wenye ngozi nyeusi tubadilike jaman
 
Mkuu ni sahihi uaminifu ndo mtaji, ila still kwanza lazima uanze na mtaji wako then baadae ndo waanze kukupa bila pesaa

1. Benki wale wakpaji wenye historia nzuri ndo hukupeshwa bila masharti, lakini mwanzo walipewa mashariti kama watu wengine tu ila baada ya kujenga uaminifu mashariti yakapungua

2. Kuhusu kupewa bidhaa na kiwanda ni hivyo hivyo, mwanzi ni lazima uvulipie ili sasa baadae ndo uanze kujenga uamnifu na wao, huwezi anza tu siku ya kwanza wakakupa bidhaa

3. Ila mwisho kabisa, uaminifu hupotea kwa njia nyingi, Mfano wewe umechukua mzigo vizuri, umefika kwenye eneo lako la kazi mzigo hautoki kabisa, na muda wa wale watu kutaka pesa zao umefika, ukijaribu kuwaambia sababu, ambayo ni ya ukweli hawatakuelewa na hapo ndo uamnifu huanza kupungua

So mara nyingine uaminifu huwa unapotea si kwa kukusudia bali ni kwa bahati mbaya tu
 

Mkuu KOMANDOO, Ni sawa kabisa unachokizungumzia kwamba lazima uwe na mtaji kidogo kwanza ili watu wakuamani, au benki kuwapa masharti nafuu watu wenye historia nzuri n.k., ni kwa nini watu wote hawa wanakuweka kwenye mizani kwanza? Kwa mtazamo wangu ni kwa sababu uaminifu ulishapotezwa na mtu au kundi fulani, ndo maana wanakuwa wagumu kukuamini kabla ya kukuchunguza kwanza. Kungekuwa na uaminifu mtu asingewekwa kwenye mizani kwanza.
 

Kweli kabisa Mkuu, tatizo la wengi ni kwamba wanapenda short cut, kupata hela kwa kutapeli leo bila kuangalia madhara yake kesho itakuwaje?
 
Nina muda tangu nimekuwa member wa JF,,
Lakini mara kadhaa au zote niliishi kwenye nchi yangu bila kujua mkoa wangu...
Sasa hapa ni mahala ambako nilitakiwa kuwepo...
Nitoe pongeze kwa watu wote mlioko humu..
Hata majibizano na kupishana kwenu kumekuwa kwa mantiki na nia ya kusaidiana...
Kwa stail hii 2tajenga taifa lenye watu makini katika Nyanja ya Biashara na Uchumi...
0ngereni sana..
 
Kweli uaminifu ni muhimu ila biashara zina changamoto nyingi sana. Unaweza ukawa mwaminifu ila usiwe na uwezo wa kuovercome hizo challenges za kukufikisha kwenye mafanikio.
Kitendo cha kupewa mkopo tayari ushaaminiwa, kuweka collateral ni ili ujibidiishe zaidi uweze kulipa mkopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…