Mtaji kianzio wa M-PESA. Naomba kufahamishwa!

Mtaji kianzio wa M-PESA. Naomba kufahamishwa!

Down To Earth

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
21,940
Reaction score
16,643
Wapendwa, habari za jioni?
Ni matumaini yangu wote mu wazima wa afya!
Naombeni msaada wenu wa kimawazo. Naomba kufahamishwa minimal capital for establishing m-pesa is how much?
Naomba pia nielekezwe potential suitable areas for this business.
Binafsi nina tshs laki 4 na elfu 60:
natanguliza shukurani!
 
Wapendwa, habari za jioni?
Ni matumaini yangu wote mu wazima wa afya!
Naombeni msaada wenu wa kimawazo. Naomba kufahamishwa minimal capital for establishing m-pesa is how much?
Naomba pia nielekezwe potential suitable areas for this business.
Binafsi nina tshs laki 4 na elfu 60:
natanguliza shukurani!

Swali kwako kabla hujajibiwa,usahapata till?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
kama umeshapata till kwani nayo wameishaifanya dili,huipati hivi hivi mpaka kona nyingi!mtaji unategemea na eneo utakalo fanyia kazi,ila ni vizuri kuwa angalau na 1.5m,ili angalau milion1,iwe kama float inakuwa kwenye simu kwa ajili ya wanaoweka,na laki 5,kwa ajili ya wanaotoa,kwani,hiyo laki 4 na 60,itakuwa ngumu kuigawa,kwani we wakija wateja 2 tu float imekwisha!ila kibishi bishi unaweza ila haitakuwa na ufanisi!kwani wateja wengi watakuwa wanakosa huduma kwako,na wakishajua kuwa mtaji wako ni kuunga unga kama homa za vipindi!watakuwa hawaji kwani wanajua kuwa pale hatapata huduma.ikishindikana sana anza angalau na milioni.
 
Mpesa ili upewe till ni lazima uwe na mtaji wa shilingi milioni moja i.e 1Milion.
 
Guys may please be informed about till.

Ok!till ni zile line mbili,ni kama line za simu za kawaida kimuonekano,ambayo unaposajiliwa na kuwa wakala,hizo ndio zinakuwa utambulisho wako ambazo ni namba ya wakala.moja inakuwa ni ya kibenki,unapokwenda bank kununua float wanakuwekea kwenye namba hiyo,kisha we ndio utahamisha hiyo float kwenye till yako ya pili ambayo ndio namba yako ya uwakala,na ndio line ya kazi,ambayo utai2mia kwenye ofic yako,hiyo till ya ki bank ndio kamisheni zako zote watakuwa wanakuwekea humo,na hiyo unakaa nayo wewe sio kumpa mfanyakazi wako akae nayo kama uta2mia mfanyakazi lakini.Hiyo inakuwezesha ku control biashara yako kama unaona mfanyakazi wako anakuletea magumashi unauwezo wa kuihamisha float yote kutoka kwenye till yake ,nadhani utakuwa umeelewa nini maana ya till.
 
Mpesa ili upewe till ni lazima uwe na mtaji wa shilingi milioni moja i.e 1Milion.

Kaka upo wapi wewe!cku hizi hata ukiwa na elfu 20!au kumi unapata till! Uhuni wanaoufanya ni kwamba ukiwaendea oficn kuwa unataka uwakala wanakwambia zoezi hilo tumeishalisimamisha!ila kwa njia za panya hao hao ndio wanataka cha juu,ukiwapa tu cku hiyo hiyo tu wanakupa kila ki2,float ni juu yako unakianzio bei gani kaanze!tz ni zaidi ya uijuavyo.
 
Je,unapataje hiyo kamishen kwa mwez ukiwa na mtaji wa milion moja? naomba maelezo kwa anaejua.
 
nami napenda jua wakuu iyo til bei gani,na je kuhusu licen na tin lazma zisome majina ya kwenye line ya uwakala?
 
Ukifuata procedure lazma uwe na leseni ya biashara,mtaji 1m na kitambulsho chako,ila unaweza kununua ya mtu aliyesajiliwa uwakala aidha ukaendelea kuitumia kwa jina lake au mkaenda kubadili jina ukaweka lako kama unayo leseni,ukihitaji iliyosajiliwa tayar bei ni maelewano kama unahtaji till ya m-pessa unaweza kuni pm nikakuunganisha na wadau
 
Mkuu NDESSA (na wengine) kama una wadau wa tili ya tigopesa naomba uniunganishe
 
Back
Top Bottom