Mtaji milioni 3, biashara ipi itafaa?

Kumbe zaidi ya kuturoga mkuu mshana una mambo mazuri kwetu. Kwa hiyo huuzi kwa grades? Maana ungenitwisha grade one ningekuwa tajiri japo mkuu hapendi tuwe matajiri
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hiyo mali ni nzuri zoom picha uone
 
Kilimo au fungua stationary hapo karibu na chuo
M3 haitoshi kwa stationery
Hebu tuchambue
Kodi ya chini laki 1 kwa miezi 6 laki sita
Photocopy mashine ya kawaida milioni 1
Computer na monitor laki 4
Printer ya kawaida laki 1
Makabati ya kioo mawili laki 5
Viti 2 laki moja
Meza ya computer laki 1
Bidhaa za kuanzia milioni 1
Miscellaneous laki 2
Kwa mahesabu ya haraka na kujibana sana stationery ndogo inahitaji milioni nne hapo ni kama chumba kimekamilika kila kitu
 
Ahsante
 
Kwenye biashara ili ufanikiwe vizuri unahitaji kuwekeza kidogo lakini faida iwe kubwa japo pia kuna status
Ukifungua duka la viatu halina uwekezaji mkubwa na faida inaonekana haraka tofauti na stationery ambayo inahitaji vitu vingi kwa wakati mmoja
 
Kwenye biashara ili ufanikiwe vizuri unahitaji kuwekeza kidogo lakini faida iwe kubwa japo pia kuna status
Ukifungua duka la viatu halina uwekezaji mkubwa na faida inaonekana haraka tofauti na stationery ambayo inahitaji vitu vingi kwa wakati mmoja
Viatu ....?Elekeza vizur mkuu
 
Fanya Mobile business kama tigo pesa, m pesa hapo hapo ulipo, kama haitafaa nenda moro kalime nyanya
 
Viatu ....?Elekeza vizur mkuu
Una kodi fremu kwa laki moja unalipia miezi 6 hiyo ni laki 6
Unanunua viroba 3 vya viatu kwa kuanzia hiyo ni laki 450
Unatumia laki 2 Kwa modification ya fremu usafiri nk
Kwahiyo jumla unakuwa umetumia 1,250,000/=
Unapofungua kiroba fanya hivi
Unachagua pair kumi bora Moja elfu kumi hapo una laki moja
Unachagua kumi nyingine Moja elfu 7 hapo una elfu sabini tayari
Unachagua kumi nyingine unauza Moja elfu 5 hiyo ni elfu hamsini tayari
Zilizobaki 20 unauza kwa Moja elfu 3 hiyo ni elfu 60
Kwahiyo kwa makisio ya chini kabisa unakuwa umeuza kiloba kwa 280000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…