Mtaji si kigezo cha kuanza biashara bali bongo lako - jadili

Mtaji si kigezo cha kuanza biashara bali bongo lako - jadili

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
19c1e616-d24c-4d77-842f-7253b2962a69_145.jpg
0d5d4a0356d6ed920f04471ea2f05060.jpg
85tkY16670.jpg
quickfire_lime.jpg

Asilimia 95 ya watu wanasema kuanza biashara lazima uwe na mtaji, labda asilimia 5 zilizobaki wataleta hoja tofauti na hiyo ambayo wataweza kuunga mkono hoja yangu. Kwa ufahamu wangu kuanza biashara mtaji si kiegezo na wenzo wa kusimamisha biashara.

  • Kuna waliofanikiwa kupata utajiri wa pesa na kuwa mamilionea kwa mamilionea kwa ghafla, lakini wengi wao wameishia bankrupt.
  • Kuna waliokuwa maskini wameishia kuogelea kwenye utajiri kutokana na mipango mathubuti iliyotokana na ubunifu wao.

Mara kadhaa nimejaribu kuwashauri wengi namna ya kuweza kusimamisha biashara hata kama hana mtaji hata kidogo na kwamba inawezekana, jibu walilonipa ni kwamba bila mtaji haiwezekani, hata ukijaribu kumwelimisha tatizo wamejengeka na hili kwamba kuanza biashara au mradi lazima uwe na mtaji.

images
images
images

  • Picha ya kwanza barbashop ya Mzee Vernon Winfrey ambayo amefanya maisha yake yote na ndiyo iliyosaidia kumsomesha Oprah kufikia alipo.
  • Picha ya pili Baba mzazi Oprah mzee Vernon Winfrey akiwa na binti yake Opral Winfrey alipofungua barbashop mpya miaka 3-4 hivi iliyopita baada ya kuibomoa ya zamani na kuijenga mpya eneo hilo hilo la uswahilini. Mpaka leo hii anaendelea kufanya kazi hiyo ya kinyozi.
  • Picha ya tatu Mzee Vernon Winfrey akiwa kazini kama kinyozi.
Tujifunze toka kwa Oprah Winfrey
Namkumbuka mama mmoja tajiri sana nchini Marekani ambaye ni Oprah Vernon Winfrey, binti ya mzee Vernon Winfrey mwenye barbashop ambaye kwa kipindi fulani alikuwa kinyozi wangu nilipokuwa nchini humo. Barbashop ya babake ndiyo iliyomsomesha Oprah na kisha kuamua kutumia akili yake kwa kulonga kwenye maonyesho ya TV hadi kufikia alipo kuogelea kwenye utajiri. Nyumba alimokulia ambayo imepangishwa kwa wakuja toka Afrika eneo la watu wa daraja ya chini ndipo anayeogelea katika utajiri alimokulia na kusoma shule za watoto maskini.

Wasomi hawana fikra za kujiari bali kuajiriwa
Wahitimu wengi vyuoni wanakazania kuzunguka huku na kule kutafuta kazi, ni dalili za wazi kuwa hawakufundishwa na kufundwa namna na misingi ya kusimama wenyewe ila tu kutegemea ajira. Wengi wanataka njia ya mkato kuwa mamilionea kwa siku moja badala ya subira ya kujenga misingi imara ya kuwawekea dhana ya kukuza uchumi.

Hata tuta la mchicha na viazi ukiwadokezea wanaona kama unafanya utani vile, wakati wangefikiria tuta moja au mawili ya viazi vikikomaa ambavyo huchukua muda mfupi mavuno yake anaweza kupata mtaji wa kuanzisha kiosk cha kusukuma kwa tololi cha kuuza vocha za simu. Mchicha ndio kabisa maana ni wiki mbili hadi tatu unahesabu kitu mkononi, na kwa kuwa ni wasomi wana mbinu za kutafuta soko sehemu zanye pesa kama mahotelini na restaurant, lakini wao wanaona bora kuchakaza kandambili kutembeza Resume kutafuta ajira.

Tujadili namna gani watu wanaweza kutumia elimu yao kusimama wenyewe hasa siku hizi ambapo ajira zinazidi kuwa haba kutokana na wingi wa vyuo na job openings kuwa kama chanda cha dhahabu kwenye kisahani kikikodolewa na maelfu, nani atakipata? Mwenye kukipata itamgharibu zaidi ya kuamua kusimama mwenyewe.
 
Mafanikio huja kidogo kidogo! Ni kweli mtaji sio kigezo cha kuanzisha biashara! Kwangu mimi kigezo kikubwa cha biashara ni kutambua nini unatakiwa kuuza na na wapi!

Wajasiliamali wengi hawakai chini na kufikiri biashara gani wanatakwa wafanye, Ukimwona jiarani yako kanunua bajaji na kesho na wewe! Huna msimamizi wala mwendeshaji matokeo yake ni nini??

Pili hatutumii washauri na wataalam wa mambo haya! Kama hauna ufahamu wa kitu unataka kuuza utamshawishi vipi mnunuzi

Tatu tuiangalie dunia inavyobadilika tutumie fusa za mapinduzi ya tech kufanya biashara, sio za kufuga kuku tu na kuuza mayai matangazo kwenye mageti. Kuna wanaijeria kibao na waethiopia China siku moja niliona TBC wanafanya biashara huko
 
Ni kweli kabisa, Ila ishu ni kwamba si kweli kabia kwamba unaweza kuruni biashara bila mtaji kwa sababu hata servise business ambzo inasemekana unaweza anza bila mtaji still lazima uwe na hata Tsh 500 ya kununua kalamu au karatasi na kazalika,

So ishu ni kwamba Kama Mjasiriamali unatakiwa kuumiza kichwa jinsi ya ku grow, huwezi ukajiita Mjasirimali halafu ukaanza kulia kwamba huna mtaji,The real Entreprener hasubirii mapka serikali ilete miradi ya Ujasirimali ndo aanze,

Ni kweli Iadea ni Primary capital na kutokea hapo ndo unaweza wewe kama wewe kuumiza kichwa jinsi ya kuweza kusonga mbele na wazo lako, watu wasiishie kusema wana mawazo ya Biashara ni lazima Uonyeshe bidii katika wazo, Wazo kama wazo si ishu kabisa na watu hawawezi kukuona mjanja kisa un wazo bali utapimwa kwa jitihada zako,

Hivyo Basi, swala la Mitaji ni juhudu za Mtu bianafisi, nazani ukisoma story za watu wali fanikiwa, kuna story zinazungumzia walivyo grow up, so ni wewe kama mjasiriamali kuhangaika kwa kila njia ya kupata pesa za kuanza projet yako

Kwa Bongo Tunatatizo kubwa sana katika hilo, Mtaji umegeuzwa kuwa Ngao ya Kuharalisha mtu kuto kujiajiri, kila utakaye muuliza ni mtaji,

Ukiwa na Spirit ya Ujasiriamali utaona kwamba mtaji si ishu kabisa, Bali kinacho takiwa ni Jitihada binafisi, unaweza kuta mtu ni mfanya kazi naanalipwa freshi tu ila swala la Kujiajiri atakuambia hana pesa, ishu ambayo sio kweli,

SO KWA WAFANYA BIASHARA MTAJI KWELI NI TATIZO KUBWA SANA, ILA KWA MJASIRIAMALI MTAJI SI TATIZO,
 
Kuna makampuni kadhaa yameanzishwa nchini ambayo yanaonekana kumilikiwa na wazawa, lakini huwezi kuamini amefanikiwaje kuwa na mtaji wa kuwa na mradi mkubwa kama wa kuwa na shirika la ndege, nk. Ukweli wengi hatujui kujifunza na wanaojua hawapendi kutufunza wengine ndio tatizo si kwa Tanzania tu ila kwa dunia, wachache wenye mbinu hizo hawako tayari kushirikisha fikra na waoni.

Biashara duniani ni kushirikisha na kushirikiana bila hivyo mafanikio ni haba. Kuna walioneemeka kutokana na kushirikishwa katika biashara na wanaonekana mamilionea, lakini ukiangalia background you walikuwa maskini kama wengi tulivyo.

Nakubaliana nawe mdau
Eliphaz the Temanite wengi wetu kuwa biashara ni kuiga kwa vile fulani anafuga kuku basi nami naandaa banda la kuku, hatima bidhaa ya aina moja kuishia kwenye supply kuwa kubwa kuliko demand. Hapa ndio tatizo.

Pengine wengine wengi wetu hatuoni faida ya moja kwa moja na kubwa inayoweza patikana kutokana na kilimo ingawa ni cha msimu, ila tunaangalia mavuno hayo na soko lake badala ya kufikiria kilimo cha mazao ambayo unaweza kuyaingiza kwenye mfumo wa industrialization kuwa processed na hivyo kuuza producs zake.
 
Ni kweli kabisa, Ila ishu ni kwamba si kweli kabia kwamba unaweza kuruni biashara bila mtaji kwa sababu hata servise business ambzo inasemekana unaweza anza bila mtaji still lazima uwe na hata Tsh 500 ya kununua kalamu au karatasi na kazalika,

So ishu ni kwamba Kama Mjasiriamali unatakiwa kuumiza kichwa jinsi ya ku grow, huwezi ukajiita Mjasirimali halafu ukaanza kulia kwamba huna mtaji,The real Entreprener hasubirii mapka serikali ilete miradi ya Ujasirimali ndo aanze,

Ni kweli Iadea ni Primary capital na kutokea hapo ndo unaweza wewe kama wewe kuumiza kichwa jinsi ya kuweza kusonga mbele na wazo lako, watu wasiishie kusema wana mawazo ya Biashara ni lazima Uonyeshe bidii katika wazo, Wazo kama wazo si ishu kabisa na watu hawawezi kukuona mjanja kisa un wazo bali utapimwa kwa jitihada zako,

Hivyo Basi, swala la Mitaji ni juhudu za Mtu bianafisi, nazani ukisoma story za watu wali fanikiwa, kuna story zinazungumzia walivyo grow up, so ni wewe kama mjasiriamali kuhangaika kwa kila njia ya kupata pesa za kuanza projet yako

Kwa Bongo Tunatatizo kubwa sana katika hilo, Mtaji umegeuzwa kuwa Ngao ya Kuharalisha mtu kuto kujiajiri, kila utakaye muuliza ni mtaji,

Ukiwa na Spirit ya Ujasiriamali utaona kwamba mtaji si ishu kabisa, Bali kinacho takiwa ni Jitihada binafisi, unaweza kuta mtu ni mfanya kazi naanalipwa freshi tu ila swala la Kujiajiri atakuambia hana pesa, ishu ambayo sio kweli,

SO KWA WAFANYA BIASHARA MTAJI KWELI NI TATIZO KUBWA SANA, ILA KWA MJASIRIAMALI MTAJI SI TATIZO,

Umenena hoja ya maana, pengine ni uvivu wetu wa kufikiri umetufikisha hapa kuona mafanikio hutokana na mtaji, wakati mtaji ni dunia yetu ilivyo na Processing unit ni ubongo wetu. Muda amao wasomi wengi wanapoteza kuzunguka kwa miezi kadhaa kunadi RCV zao bila mafanikio wangeamua kutuliza kichwa na kufanya kitu huenda wangeshakwua na kitu kinachowasaidia kupata vitumbua asubuhi.

Mara zote mafanikio si mijini tu, kwani mijini kila kitu ni ghali. Huko vijijini ndiko mali na ardhi vinapatikana kwa ulaini na ukivitumia vizuri vinageuza kabisa maisha ya mtu. La sivyo muijini tutaishia kuchangiana za kulipia ghetto huku tukipishana muda wa kulala ili kupeana nafasi kwa kutotosheleza makazi ya kila mmoja. Vijijini raha tupu hakuna kitu kama hicho.
 
Nazipendaje hizi Thread siku hizi...#Naomba haya mageuzi yadomain in my mind#
 
Mkuu ni kweli kabisa, but tatizo kubwa sana n fear of starting, fear ndo inatuangamiz wote, unshinwa hata kabla yakuanza, yaani kama ni vita unashinwa vita hata kabla yakupeleka majeshi eneo la vita
 
Wahitimu wengi vyuoni wanakazania kuzunguka huku na kule kutafuta kazi, ni dalili za wazi kuwa hawakufundishwa na kufundwa namna na misingi ya kusimama wenyewe ila tu kutegemea ajira. Wengi wanataka njia ya mkato kuwa mamilionea kwa siku moja badala ya subira ya kujenga misingi imara ya kuwawekea dhana ya kukuza uchumi.

Hata tuta la mchicha na viazi ukiwatokezea wanaona kama unafanya utani vile, wakati wangefikiria tuta moja au mawili ya viazi vikikomaa ambavyo huchukua muda mfupi mavuno yake anaweza kupata mtaji wa kuanzisha kiosk cha kusukuma kwa tololi cha kuuza vocha za simu. Mchicha ndio kabisa maana ni wiki mbili hadi tatu unahesabu kitu mkononi, na kwa kuwa ni wasomi wana mbinu za kutafuta soko sehemu zanye pesa kama mahotelini na restaurant, lakini wao wanaona bora kuchakaza kandambili kutembeza Resume kutafuta ajira.

Tujadili namna gani watu wanaweza kutumia elimu yao kusimama wenyewe hasa siku hizi ambapo ajira zinazidi kuwa hapa kutokana na wingi wa vyuo na job openings kuwa kama chanda cha dhahabu kwenye kisahani kikikodolewa na maelfu, nani atakipata? Mwenye kukipata itamgharibu zaidi ya kuamua kusimama mwenyewe.

Kaka hapo ndio kwenye mzizi wa tatizo, elimu yetu inatuandaa kuajiriwa ndio maana mtu yuko radhi ajitahidi kupata vyeti hata kama hana ujuzi/uzoefu au hajapata uelewa kuhusu anachojifunza kwa sababu ndio vinavyohitajika ili kupata ajira.

Tunafursa nyingi sana hasa kwenye kilimo, ila kwa sababu ya kufungwa na mawazo ya kuamini kwamba kuajiriwa pekee ndio njia ya maisha, tunashindwa kuziona fursa.

Be blessed
 
Fikra za wengi wetu kwamba kusimama hadi uwe na mtaji, siku wakipata mtaji na kisha kufilisika hawawezi kusimama mpaka wapate mtaji, tofauti na yule anayesimama kwa kutegemea zaidi bongo lake kwani kufilisika ni njia ya tahadhari kwa siku atakapoimarisha nguvu za kujiimarisha zaidi.
 
Mada nzuri !!mimi nilikuwa najua udalali pekee ndio biashara pekee unayowezakuifanya bila mtaji,tuelezeeni vizuri ni vipi wawezaanza bila capital,mawazo ya biz tunayo lakini pesa yaitajika...niwekeni sawa
 
Machinga wameweza kuanzia from 0 to capital. Wamekuwa wenzi wa wafanya biashara na retailers wakubwa kwa kwenda kuchukua bidhaa madukani mwao na kuziuza mitaani, akifanikiwa kupata wateja ametia chake mfukono na kumrudishia mhazini wake haki yake. Kwa nini hilo lisiwezekane kwa wasomi?

Msomi una nafasi ya kufanya kile anachofanya machinga kwa mbinu ya juu zaidi maana kuna nafasi na maeneo mengi ukifunguka na kwa weledi unashtukia umetengeneza soko la bongo lako kutumia kujenga mazingira ya kujiajiri.

Ukimwambia msomi fanya utafiti kupata soko la wanaotaka solar kuwekewa majumbani mwao. Badala ya kupoteza muda kutwa kucha kuzungukia maofisi kutafuta kazi bila mafanikio, bora zunguka kutafuta soko hiyo adimu. Ukishapata unamwambia niambie kisha mimi nitakuajiri umsaidie mtaalamu for installation kisha hapo una kitu cha kutia mfukoni, kama msomi huyo kafanikiwa kupata wateja kumi au zaidi hajatia mfukoni zaidi ya zile ambazo angetegemea kupata akipata ajira? Kwa utundu na usomi wake hatachota ujuzi wa solar energy system inavyokuwa-installed na kisha baadaye akaamua kuwa na kampuni yake?

Huu ni mfano mmoja wapo, nimejaribu kuwashawishi vijana hilo, kama wangefanikiwa ni mradi unaweza kumsaidia kijana not just to keep them busy, they can get some cash absolutely, na katika kujishughulisha hivyo akili yao itapanuka na kuibua mengine na nafasi nyingine wanazoweza kujenga mazingira ya kujiajiri.

Tatizo nilionalo ni kasumba ya kwamba kusoma maana yake ukihitimu ni kuajiriwa badala ya kujenga dhana ya kupanuka kifikra katika kujenga maisha ya mtu. Kuwa na maisha mazuri po pote duniani hata nchi zilizopaa juu sana kiuchumi, ajira pekee haitoshelezi kujikimu kimaisha, unatakiwa kuwa na ubunifu wa kuwa na extra income, hapo utaona mambo yanakunyookea vema.
 
Mkuu @candid scope, Hebu tutumieni mifano halisi na mazingira halisia ya mtanzania. Hiyo kazi ya mzee Winfrey haujasema aliianza kwa mtaji wa Dollar ngapi, na mpaka sasa ni miaka mingapi na ameingiza kiasi gani cha fedha!!! Mimi bado namuona ni mjasiriamali mdogo tu, na hii inatoka na kuwa hakupangilia vizuri na kuwekeza katika fursa mpya, kusomesha watoto ni wajibu tu si kipimpo cha kipato, hata bongo watu wanasomesha watoto kwa kulima kwa jembe la mkono, kuuza gongo, kuuza vitumbua nk. Point yako ni ya ukweli, lakini mfano wako hauko si halisi, huyo Mzee Winfrey sidhani kama anaweza kuwa role model!

cc: lucky sabasaba, Samaritan, Chasha, IBRAHIM MGAYA
 
Mfano wa mzee Vernon Winfrey unaweza kuchokonoa na kukokotoa tafsiri nyingi, ingawa mleta mada aliamua kushirikisha kile ambacho hata walio matajiri sio wote wamekutokea katika familia zenye kuwapa mitaji ya kuanzia maisha. Tunaweza kujifunza mazingira ya nyumba ambayo babake Winfrey amekuwa anaendesha kijibiashara chake cha barbashop kwa miaka yote. Dhahiri biashara hiyo ni ya kumsaidia kujikimu kimaisha lakini katu si kuchuma mamilioni kwa mtaji wa kuanzia maisha wanawe.

Oprah katokea katika familia hiyo ambayo mazingira yanayofanana na hali ya chini ya maisha ya familia nyingi za kitanzania za kimaskini. Amepambana na maisha magumu licha ya kubakwa na vibaka when she still young girl katika mazingira hayo unayoona jengo la kwanza.

Babake mzazi alinisimulia kwamba alichomsisitizia ni kujiendeleza bintiye kielimu baada ya tukio la kubakwa, amefanikiwa. Oprah hakuwa na mtaji uliomfikisha alipo. Bongo na ulimi mtamu kwenye maonyesho ya TV tu ndilo lililofanyakazi kumfikisha alipo si mtaji.

Nimeleta mfano wa familia hiyo kama kielelezo maana familia yenyewe inajieleza hivyo si kama familia za kiafrika tungeambiwa tumeidhalilisha. Tuna kitu cha kujifunza hapa, licha ya kwamba mazingira ya Tanzania na Marekani ni tofauti, lakini maisha ni yale yale, pangine kwa ufahamu wangu mazingira ya Tanzania yana nafasi na uhuru zaidi wa mtu kusimama mwenyewe kuliko nchi hizo za kibepari, amini usiamini huo ndio ukweli.
 
Mkuu ni kweli kabisa, but tatizo kubwa sana n fear of starting, fear ndo inatuangamiz wote, unshinwa hata kabla yakuanza, yaani kama ni vita unashinwa vita hata kabla yakupeleka majeshi eneo la vita

Tatizo lingine ni kuataka kuonekana nawe ni mfanyabiashara mapema kabla hujawa! Wengi hili huwasumbua
 
ameanzisha barbershop kwa aijli ya kusomesha watoto/mtoto wake na baada ya miaka zaidi ya 40 bado tu yupo kwa babrbershop hiyo tu moja ananyoa, huu nao ni mfano wa role model wa maendeleo???? ungeniambia labda sasa hivi mzee winfrey anamiliki barbershop zaidi ya 1000/= marekani na duniani ningekuelewa!!!! matokeo yake unatuchanganyia na mafanikio ya utajiri wa mwanae oprah!!!
 
Ungejaribu kupitia mabandiko yanayofuata baada ya bandiko kuu ungeona huna haja ya ulichokiandika kwa vile kimeshajibiwa na mleta mata katika bandiko # 13. Nisingependa kurudia hilo, ila nakuletea nukuru ya bandiko hilo ili upate mwanga kwa lengo la mleta mada kielelezo cha familia ya Mzee Vernon Winfrey na bintine tunafunzwaje katika maisha yetu. Mimi mwenyewe babangu alikuwa na mashamba na mifugo, lakini kiwango changu si cha kuiga alivyofanya yeye, nitajaribu kutumia zaidi elimu yangu kufanya vema ndivyo alivyofanya Oprah.

Rejea bandiko
#13 kama ifuatavyo:

Mfano wa mzee Vernon Winfrey unaweza kuchokonoa na kukokotoa tafsiri nyingi, ingawa mleta mada aliamua kushirikisha kile ambacho hata walio matajiri sio wote wamekutokea katika familia zenye kuwapa mitaji ya kuanzia maisha. Tunaweza kujifunza mazingira ya nyumba ambayo babake Winfrey amekuwa anaendesha kijibiashara chake cha barbashop kwa miaka yote. Dhahiri biashara hiyo ni ya kumsaidia kujikimu kimaisha lakini katu si kuchuma mamilioni kwa mtaji wa kuanzia maisha wanawe.

Oprah katokea katika familia hiyo ambayo mazingira yanayofanana na hali ya chini ya maisha ya familia nyingi za kitanzania za kimaskini. Amepambana na maisha magumu licha ya kubakwa na vibaka when she still young girl katika mazingira hayo unayoona jengo la kwanza.

Babake mzazi alinisimulia kwamba alichomsisitizia ni kujiendeleza bintiye kielimu baada ya tukio la kubakwa, amefanikiwa. Oprah hakuwa na mtaji uliomfikisha alipo. Bongo na ulimi mtamu kwenye maonyesho ya TV tu ndilo lililofanyakazi kumfikisha alipo si mtaji.

Nimeleta mfano wa familia hiyo kama kielelezo maana familia yenyewe inajieleza hivyo si kama familia za kiafrika tungeambiwa tumeidhalilisha. Tuna kitu cha kujifunza hapa, licha ya kwamba mazingira ya Tanzania na Marekani ni tofauti, lakini maisha ni yale yale, pangine kwa ufahamu wangu mazingira ya Tanzania yana nafasi na uhuru zaidi wa mtu kusimama mwenyewe kuliko nchi hizo za kibepari, amini usiamini huo ndio ukweli.
 
Mkuu ni kweli kabisa, but tatizo kubwa sana n fear of starting, fear ndo inatuangamiz wote, unshinwa hata kabla yakuanza, yaani kama ni vita unashinwa vita hata kabla yakupeleka majeshi eneo la vita

Umesema kweli mkuu
 
tatizo la vijana wengi ni uvivu wa kufikiri, na uwezo wa kuthubutu. mawazo mgando ya kuona kuwa kuajiriwa serikalini au kwenye afisi za watu binafsi ndio heshima. wengi huona kuwa akijiajiri mwenyewe si kazi, na kwamba hata jamii itamdharau. nioanvyo mimi ipo haja ya elimu ya ujasiriamali kufundishwa kuanzia shule za msingi kama somo kinadharia na kivitendo kama somo la sanaa na ufundi lilivyokuwa zamani wakati tukisoma shule(sijui kama hadi leo lipo). vijana wafunzwe kuyaona maisha katika mapana yake, wajengewe uwezo wa kufikiri na kutatua changamoto, badala ya kujengewa uwezo wa kukariri kama ilivyo sasa.
 
Kweli kabisa na naungana nawe kuwa"MWENYE SPIRIT YA UJASIRIAMALI HAOFII MTAJI" kwani sheria ya kutumia mtaji wa sh. 10000 kutengeneza faida ya sh.5000 katika biashara yeyote ni ile ile inayotumika kutumia mtaji wa sh. 1000000000 kupata faida ya sh. 500000000, kikubwa ni kuwa risk taker kwa kuthubutu kuanzisha biashara yeyote uliyoifikiria na baada ya kuanzisha biashara kazi inayofuata ni KUIHESHIMU PESA nikimaanisha usidharau wala kutumia vibaya fedha hata kama ni sh.50 kwani ukiwa na sh. 499.9 kwenye salio kwenye simu na unataka kujiunga na cheka au huduma nyingine za simu inayogharimu sh.500 haitakubali na itakutaka kuongeza vocha hivyo kuiheshimu pesa katika biasha ndo chachu ya mafanikio! Pamojaa
 
Back
Top Bottom