Mtaji wa 10 Millions Tshs

COTANGENT

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2012
Posts
444
Reaction score
243
Habari za majukumu, niko na hiyo pesa ningependa mawazo yenu ya biashara ipi hususa ya uchuuzi- yaani kutoa bidhaa point A kwenda kuuza point B kwa faida
Siko interested sana na Kilimo wala ufugaji, hivyo mawazo yenu yasijikite huko kabisa.
Zaidi ni taarifa za bidhaa fulani kuitoa sehemu fulani na kwenda kuiuza sehemu nyingine. Nataraji ushirikiano toka kwenu, naomba kuwasilisha.
 
Biashara za uchuuzi ni biashara za kijinga, ni biashara za watu wasio na uwezo wa kufikiri au ambao wana uwezo wa kufikiri lakini wanaona uvivu kufikiri. Kubwa zaidi, ni biashara za watu wavivu wavivu tu na watu wenye akili za kipuuzi kama za wachuuzi ndio wameifikisha hii nchi hapa ilipo. Nchi inashindwa kuzalisha vitu kwakuwa kila mwananchi anafikiria kuchukua vitu mbele ya nyumba yake then anaenda kuuza nyuma ya nyumba yake. Ukisoma tu hiyo thread utagundua mtoa maada ni mtu wa namna wa namna gani. WAKATI CHINA KILA MWANANCHI ANAFIKIRIA KUPRODUCE NA KUUZA HIVYO VITU VINAKOSA WANUNUAJI KWAKUWA KILA MTU ANATAKA KUZALISHA NI KINYUME NA TANZANIA AMBAPO EVERY TOM&JERRY WANT TO BUY AND NOT TO PRODUCE. HUWA NACHUKIA SANA NAPOKUTANA NA WATANZANIA KAMA MTOA MAADA HII.
 


Pamoja na hayo mkuu.
sasa watu wote wakizalisha ni nani atakua mnunuaji.?.Ukizingatia soko la Africa lilivyo bovu.

Mtanzania hawezi kuzalisha mali na kupata wanunuaji ili hali bado Mali nyingi zinatokea nje ya nchi. Hivyo kwa tanzania kufanya kitu kama hiko ni lazima Serikali pia ifanye mageuzi ya sera ya Uwekezaji humu nchini.
 
Mkuu Chips Mayai, kwenye maisha kila kitu ni hobby sijawahi penda kilimo wala ufugaji japokuwa nazungukwa na watu wanaofanya hizo shughuli na hata humu JF kuna ushauri mwingi tu juu ya kilimo na ufugaji.
Next time jaribu kuja positive zaidi hata kama unakosoa kitu. Hio China uliyotolea mfano mazingira ya kiuwezeshwaje yapo tofauti sana na hapa kwetu... ndio maana sitaki kuji involve kabisa kwenye production activities, kwa ushauri zaidi karibu.
 
Ndio mbona mie kiduka changu mtaji wake ilikuwa milioni 8 na kinadunda babu yangu Asprin!!

Duka la vifaa vya ujenzi???

Hiyo kodi ya pango tu kwa mwaka ni shingapi kwa mfano??
 
Last edited by a moderator:
Duka la vifaa vya ujenzi???

Hiyo kodi ya pango tu kwa mwaka ni shingapi kwa mfano??

Shilingi laki mbili na arobaini kila mwezi elfu 20.....si unajua mambo ya kijijini babu???
 
Shilingi laki mbili na arobaini kila mwezi elfu 20.....si unajua mambo ya kijijini babu???

Oh... kwa kijijini sawa. Hapa mjini utasubiri sana. Hiyo unayolipa kwa mwaka hapa Dar kuna sehemu haitoshi hata kwa mwezi!!
 
Oh... kwa kijijini sawa. Hapa mjini utasubiri sana. Hiyo unayolipa kwa mwaka hapa Dar kuna sehemu haitoshi hata kwa mwezi!!

Duhhh!!sasa kwa dar nikisema nifungue duka la ujenzi natakiwa niwe na kiasi gani?
 
Hv Luchelele ni Rock city Mwanza...? Ok kwa mkoa hio kodi ya pango ni possible ila mjini hapana, ok nimechukua wazo lako best.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…