Mtaji wa laki 5, Nifanye biashara au shughuli gani ili kuukuza

Hakuna biashara ya shillingi laki 5 unaweza nitajia biashara mbili za shillingi laki 5?

Unaishi Tanzania au nje ya Tanzania?

Mtu anayeuza tu ishu kama macover ya simu, zile screen protector n.k anaweza akaanza na mtaji huo...

Mtu anayelangua mtumba wa nguo, viatu, mashuka, nguo za ndani n.k anaweza akaanza na mtaji huo...

Mtu anayefanya biashara ya uji, maandazi, chapati, chai, mihogo, alkasusu, kahawa n.k anaweza akaanza na mtaji huo...

Mtu anayeuza kuni, mkaa, mafuta ya taa nk anaweza akaanza na mtaji huo...

Wengine wataweka nyingine...
 
Mtu huyo huyo anaweza anza na biashara tajwa kwa mtaji wa 10000, laki au million. Basi biashara si rahisi kusema hii ya mtaji fulani
 
Mtu huyo huyo anaweza anza na biashara tajwa kwa mtaji wa 10000, laki au million. Basi biashara si rahisi kusema hii ya mtaji fulani

Ni rahisi na inatakiwa kujua mtaji wa biashara, kwa sababu kutokea hapo ndio unaweza fanya hisabati za vitu kama ROI (return of investiment) n.k
 
Naomba Ushauri, Na Wazo la biashara ambalo nitakifanya kukuza uchumi binafsi na kipato ili kuwaangalia watu wamuhimu karibu yangu.
Boss nunua sola w100 na betrii N70 na charger Ware, na charger za solar. Kisha tafuta kijiji chochote nenda panga chumba cha biashara anza kuchaji Sim, Redio na betrii za sim.

Jaribu baada ya miezi 6 njoo hapa utoe ushuhuda wako.
 
Asante Sana ni wazo zuri mno
 
Acha uongo mzee

Hakuna mtaji halisi wa biashara fulani. Wazo linachagizwa na kilichopo mfukoni. Kua na wazo stahiki, analyse resources zako, thrive kufika tamati.

Nakumbuka nilianza biashara yangu kwa kusajili business name nikawa trusted kufika kua na kampuni. Nikaanza kupata hadi kazi zilizojua ya mtaji wangu. Kila nilipotaka kuanza nalionq mtaji hautoshi ata kusajili kampuni hahahahaha.
 
Ni rahisi na inatakiwa kujua mtaji wa biashara, kwa sababu kutokea hapo ndio unaweza fanya hisabati za vitu kama ROI (return of investiment) n.k

Hata mtaji wa 10,000 kwa hiyo biashara ya 500,000 unaweza fanya hizi hisabati “ ni namba”
 
Hakuna biashara ya shillingi laki 5
Unalosema una hakika nalo au kwakua uko jf laki tano unafanya biashara vizuri tu..ila mkitaka biashara za insta fb itakua ngumu ila ukitaka kujutoa na kukuza mtaji laki tano unazungusha
 
unalosema una hakika nalo au kwakua uko jf laki tano unafanya biashara vizuri tu..ila mkitaka biashara za insta fb itakua ngumu ila ukitaka kujutoa na kukuza mtaji laki tano unazungusha

Ni sawa ndio nasema hiyo biashara hata kwa million na mamilion unaweza ifanya. Hata chini ya laki 5 unaweza ifanya. Hakuna biashara ya laki 5
 
Beting mkuu.
Yaani hapo unachukua odds 2 tu unatia mzigo wote.
Baada ya dakika 90 unaingiza 1 milion na zaidi.
Kwa ufupi ndani ya dakika 90 unapata faida ya laki tano.
Ingekuwa hivyo kampuni zingekuwa zishafungwa

Kubeti ni Kamala kubeti ni kubashiri kuna kula na kuliwa 50/50
 
Ingekuwa hivyo kampuni zingekuwa zishafungwa

Kubeti ni Kamala kubeti ni kubashiri kuna kula na kuliwa 50/50
Maisha yote ni kamari mkuu.
Unanunua kuku umfuge akuzalie na upate faida kupitia yeye.
Unaweka muda na fedha kwaa ajili yake, malengo ikiwa ni kupata faida kupitia kwake.
Ajabu unakuja ugonjwa wa mdondo unampitia anakufa.
The same kwenye beting, unachagua odds zako vizuri, unastake mkwanja.
Mwisho wa siku mkeka unachanika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…