Mtaji wa m1.5 unatosha kuhudumia heka moja ya vitunguu/ matikiti maji?

mapipando

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
2,922
Reaction score
3,559
Habari wanajf,nimekuwa na ndoto kubwa juu ya kilimo hasa cha umwagiliaji,na nimekuwa nikiamini kuwa kilimo ni moja kati ya miradi ambayo itaniwezesha kuzifikia ndoto zangu. Mazao ambayo nahitaji kudeal nayo ni kama vile vitunguu, matikiti maji, pilipili mbuzi, karoti na mihogo japo mihogo haihitaji umwagiliaji.

Lakini kwa kuwa sina mtaji wa kutosha,kati ya heka moja ya vitunguu au ya matikiti maji kiasi cha m1.5 kinatosha kuhudumia mpaka hatua ya kuvuna? Na je mazao hayo yanachukua muda gani hadi kuvunwa na lipi lenye faida zaidi, pia ni maeneo gani yanafaa kwa kilimo cha zao husika?

Wenye utaalamu na hili naomba mnisaidie.
Natanguliza shukrani.
 
imekuwa zikitolewa mida ya kukomaa na kuvuna ikitofautiana aidha kutokana na hali ya hewa au utunzaji wa kumbukumbu ila kwa wastan nyanya, vitunguu, matikiti, hoho,bilinganya, nyanya chungu, karrot zinachukua miezi mitatu hadi kuvuna, hapa namaanisha kwa mazao yakuotesha kwanza hesabu baada ya kutawanya shambani, ingawa mda unaweza pungua au kuongezeka. mihogo zipo aina nyingi, zipo za miezi 6,12,18 na 24. chaguo lako
 
Mkuu bab-D jitahidi kusoma mada kwanza uielewe kisha uchangie kile unachoelewa. Sasa nakuomba urudi hapa utupe darasa baada ya kusoma na kuelewa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mapipando kwanza hongera kwa kutambua kuwa kilimo ni fursa ambayo ukiikamatia kwa nia na kimalengo kwakweli upo uwezekano mkubwa sana kukutoa kimaisha!

Bajeti yako ni nzuri na inajitosheleza ikiwa utakuwa umetimiza mahitaji yote ya lazima kwenye kilimo cha umwagiliaji.
Yafuatayo ni mhimu na lazima uwe na uhakika wa kuwa nayo katika shughuri nzima ya kilimo hiki;
1. Uwe na uhakika wa maji
msimu mzima wa mradi.
2. Uwe na nyenzo zote zitakazo
fanikisha umwagiliaji.
Hapa namaanisha water pump na viambata vyake
3. Uwe na shamba ambalo lina chanzo cha maji na liwe linafikika kirahisi kuruhusu kutoa mzigo.
4. Uwe na utayari wa kusimamia na uelewa wa kutosha kuhusu kilimo cha bustani. Upate wasaidizi wa uhakika na waaminifu wenye uelewa na wepesi wa kujifunza.
5. Uwe very knowledgeable na misimu ya zao lipi la kulima kwa wakati huo ili kuepuka hasara zisizo za lazima.
6. Uwe na uhakika na washauri wako wa kilimo na jitahidi kupanua uelewa wako kila kukicha hasa kipindi unapojihusisha na zao lililopo shambani tayari; hii itakujengea uelewa wa nini ufanyacho na kukuepusha na makosa huko mbele maana utakuwa ushasoma mchezo.
7. Jihakikishie soko la kile unacholima ili kuepuka kufanya kitu usicho na uhakika nacho.

Mkuu, ukitekeleza yote hayo hakika utafanikiwa na hutajutia kujihusisha na kilimo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu bab-D jitahidi kusoma mada kwanza uielewe kisha uchangie kile unachoelewa.
Sasa nakuomba urudi hapa utupe darasa baada ya kusoma na kuelewa.

Umeuliza maswali kazaa mi nimekujibu swali la "nimdagani mazao hayo yanachukua hadi kukomaa" au nimekosea?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mapipando kwanza hongera kwa kutambua kuwa kilimo ni fursa ambayo ukiikamatia kwa nia na kimalengo kwakweli upo uwezekano mkubwa sana kukutoa kimaisha!

Bajeti yako ni nzuri na inajitosheleza ikiwa utakuwa umetimiza mahitaji yote ya lazima kwenye kilimo cha umwagiliaji.
Yafuatayo ni mhimu na lazima uwe na uhakika wa kuwa nayo katika shughuri nzima ya kilimo hiki;
1. Uwe na uhakika wa maji
msimu mzima wa mradi.
2. Uwe na nyenzo zote zitakazo
fanikisha umwagiliaji.
Hapa namaanisha water pump na viambata vyake
3. Uwe na shamba ambalo lina chanzo cha maji na liwe linafikika kirahisi kuruhusu kutoa mzigo.
4. Uwe na utayari wa kusimamia na uelewa wa kutosha kuhusu kilimo cha bustani. Upate wasaidizi wa uhakika na waaminifu wenye uelewa na wepesi wa kujifunza.
5. Uwe very knowledgeable na misimu ya zao lipi la kulima kwa wakati huo ili kuepuka hasara zisizo za lazima.
6. Uwe na uhakika na washauri wako wa kilimo na jitahidi kupanua uelewa wako kila kukicha hasa kipindi unapojihusisha na zao lililopo shambani tayari; hii itakujengea uelewa wa nini ufanyacho na kukuepusha na makosa huko mbele maana utakuwa ushasoma mchezo.
7. Jihakikishie soko la kile unacholima ili kuepuka kufanya kitu usicho na uhakika nacho.

Mkuu, ukitekeleza yote hayo hakika utafanikiwa na hutajutia kujihusisha na kilimo.
Mkuu,nakushukuru sana kwa maelezo yako mazuri,nimekulewa na pengine changamoto ambayo huenda ikanikabili ni kupata wasaidizi wa namna ambayo wanatakiwa.Ila kwa kuwa nitausimamia mradi kwa karibu zaidi nafikiri huenda kila kitu kitaenda sawa.

Many thanks.
 
imekuwa zikitolewa mida ya kukomaa na kuvuna ikitofautiana aidha kutokana na hali ya hewa au utunzaji wa kumbukumbu ila kwa wastan nyanya, vitunguu, matikiti, hoho,bilinganya, nyanya chungu, karrot zinachukua miezi mitatu hadi kuvuna, hapa namaanisha kwa mazao yakuotesha kwanza hesabu baada ya kutawanya shambani, ingawa mda unaweza pungua au kuongezeka. mihogo zipo aina nyingi, zipo za miezi 6,12,18 na 24. chaguo lako
Nashukuru mkuu kwa ufafanuzi,lakini bado hujaniambia kama mtaji nilionao utatosha kuhudumia aidha heka moja ya matikiti maji ama vitunguu na pia ni maeneo gani yanafaa kwa zao husika.Ahsante.
 
Mkuu,nakushukuru sana kwa maelezo yako mazuri,nimekulewa na pengine changamoto ambayo huenda ikanikabili ni kupata wasaidizi wa namna ambayo wanatakiwa.Ila kwa kuwa nitausimamia mradi kwa karibu zaidi nafikiri huenda kila kitu kitaenda sawa.
Many thanks.

Hapo penye wasaidizi wazuri ndiyo moyo wa mradi wenyewe. Epuka kuchukua vijana wa hovyo hovyo kiukweli watakuangusha na kukufanya uchukie kilimo hiki.
Wewe ulioanga pengine uanze lini huo mradi wako? kuna namna nataka nikusaidie ikiwa una mtaji tayari.
 
Back
Top Bottom