Mtaji wa Mil.4

Ihwa jnr

Member
Joined
Feb 4, 2014
Posts
19
Reaction score
14
Wadau nimetafuta ajira imekuwa ngumu ila nimepata mchongo wa kupata kiasi cha mil.4,Niajiendeleza na masomo ya mambo ya IT na ninataka kufanya biashara hiyo hiyo inayohusiana na mambo ya Computer je hiyo biashara inalipa na je naweza kuifanya vipi na vipi mtaji wangu unatosha? Naomba ushauri wenu wadau
 
sijakuelewa mkuu!...unamaanisha ada kugeuzwa mtaji wa biashara?......tambua kulipa na kutolipa kwa biashara , uwe tayari ushaianza sio kuhadaika na propaganda ukaingia kichwakichwa!
 
Mie nafikiria ni mtaji mdogo kwa kuuza hata vifaa vya Computers(Computers accessories).
Maana hiyo ni sawa na Laptop nne tu za maana.

Nakushauri fungua Workshop sehem,maana utaalam unao,kisha Upatengeneze vizuri sana then ajiri mtu mmoja na wewe ukiwa wa pili .Maana ukitoka chuo unapitia kumaliza kazi za watu siku inakuwa imeingia.

Baada ya muda unanunua vifaa vidogovidogo ili kupamba Ofice,na mwisho wa siku unakuta Ofisi imejaa,na inakuwa mtu akileta kimeo chake unahamisha kwenye Pc useless then unaweka huko na siku inakwenda.

Uaminifu ndio silaha ya Biashara hii,na pia inahitaji uvumilivu sana.

Halafu kuwa Mjanja kwenye kutafuta Tenders kwenye Maofisi Binafsi au makampuni na hata serikalini,na hao hao wateja wako ndio watakaokusaidia kama ukiwa muwazi na mkarim kwao na hodari katia kazi zao.
Hata kama utafungua Ofisi ndogo wewe nenda Halmhasuri kaisajili upate Leseni kamili ili ikitokea Tender kama ni ya Ofisi fulani au Kampuni fulani basi unakula Shavu.

Kuna watu humu wana tenders za Maofisi makubwa sana,na ukipelekwa ofisi zao ni zakawaida sana tu.
Na Hata kama huna utaalam wa juu sana unaweza kukodi wazoefu zaidi wakaenda kukupa Company,in three years utakuwa mwingine kabisa kama sio mtu wa madem,pombe na ubishoo.

Mfano mie,nikwamba nilipata Tender ya ku supply baadhi ya viungo kwenye Hotel moja hapo Dar,sasa nilichofanya kwanza ni kusajili kama kampuni kwa Dar ambapo ni rahisi sana na leseni ndio kabisaa ubwete na haichukui muda kabisa.
Maana hawa watu wa Tenders hasa za maofisi hawatakupa kazi zao za Services katika vifaa vyao kama huna kampuni na lazima Cheques zitaandikwa kwa jina la kampuni na sio mtu binafsi.Na ukimuona mtu umafanikiwa kupata Tenders as Private basi jua hana muda kuna wajanja watakupita kama umesimama,mwishowe utaishia kwa Waganga.
 
Kama umesoma chuo maana yake unao marafiki wenye taaluma kama yako then washirikishe wazo lako mjipange wenye mawazo na malengo yanayofanana mjichange mfanye kitu cha maana.

Sababu kwa mtaji huo kiasi
Ni ngumu kulingana na gharama za assets za biashara.

Kutoka sio lazima uwe single.
 

Mi nina business yangu ya Stationery na Video library kwa pamoja (ziko two in one) nauza. Value (thamani) ya biashara ni milioni 7 including bidhaa, mashine, computer, printers, scanner, TV screen, meza/kabati ya aluminium n.k. Maelewano yapo pia. Eneo la biashara ni zuri, Mabibo karibu na shule. Sababu ya kuuza ni kwamba nitakuwa shule hivyo usimamizi siwezi kumudu tena. Picha ya duka imeambatanishwa.... Yaani nakuuzia unaendelea na biashara saa hiyohiyo ukitaka.

Mawasiliano 0758397557, 0718174415.
Attached Thumbnails
 
Turnover per day ni wastani wa kiasi gani

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…