Mtaji wa pesa huna, Je na mtaji wa nguvu huna?

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Nguvu iwe za akili na za mwili pia ni mtaji. Ukizitumia vyema nguvu hizo na ukidhibiti vyema matumizi yako utaweza kutoboa tu. Kuna watu wapo tayari kukulipa kiasi flani cha pesa kwa kuwasaidia kazi flani.

Bahati mbaya sana watu hawawezi kuziona nguvu zako za kimwili wala kiakili kwa kukutazama haiba yako. Ni sharti uidhihirishe ndipo uweze wafanya watu waanze kukupa kazi.

Hata mcheza mpira haajiriwi kabla hajadhihirisha kipaji chake iweje wewe unataka watu wakupe kazi kwa kuwaonesha haiba, maumbile na makaratasi?

Dhihirisha kipaji chako watu watakuona na watakufungulia fursa. Katika kudhihirisha kipaji lazima uwe na uvumilivu mana huwa inachukua muda mrefu kabla kipaji chako hakijaonekana.

Na kikionekana usibweteke. Wapo waliodhihirisha vipaji vyao wakapewa fursa wakabweteka na kuvimba vichwa wakafulia. Usije nawe ukaangukia katika dhahama hii.

Kwa wale waliobarikiwa wakapata elimu basi watafute hata kazi za kujitolea. Na usiyaamini makaratasi kuwa yatakupatia kazi hata hiyo ya kujitolea. Kama kweli umeamua kujitolea basi hebu jitolee ufanye kazi na ukienda ofisi za hao unaotaka wakupe kazi uwasilishe kazi yako.

Mathalan fani yako ni masuala ya masoko, basi fanya uchunguzi sokoni uone hao unaotaka wakupe kazi wanakabiliwa na changamoto gani ambazo zikitatuliwa itapelekea bidhaa zao zitauzika zaidi? Karibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…