Mtaji wa Tsh Milioni 3 nataka kuwa mtu wa kati (WINGA)

Mtaji wa Tsh Milioni 3 nataka kuwa mtu wa kati (WINGA)

Sangoma

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2012
Posts
344
Reaction score
165
Habari,

Nahitaji kupambana na utafutaji wa maisha kinamna nyingine hii biashara ya kutegemea kitu kimoja kama chanzo cha mapato naona inafanya maisha yawe magumu na nafuu kwa muda.kwa sasa Namtaji wa 3m niliopata kwenye shughuli zangu zingine za kila siku tena kwa kujinyima sana sasa nahiataji kujiongeza kusogea jijini Dar es Saalam kuwa mkimbiza mwenge mwenye mtaji wa 3m nimefika mitaa ya kariakoo mwezi wa 8 nimeona biashara mbali mbali za nguo, viatu, electronics na zinginezo nyingi nimeona wajanja ni wengi na wanyonge ni wengi pia.

Wakimbiza mwenge wa maeneo hayo niliobahatika kuwa ona ni wababahishaji na hiyo inatokana na kutokuwa na cash wanamaneno mengi ila mifuko haina kitu inakuwa hata ngumu kuaminika kwa wateja na kwa maboss wenye maduka pia sasa nahitaji kutumia nafasi hii kuwa mkimbiza mwenye cash ya 3m kama bond yangu yakujichanganyia kila kichochoro kutafuta riziki.

Ushauri wenu kuhusu hii habari nayo hitaji kupambana kuifanya kwa sasa ila biashara yangu ya awali itaendelea kuwa pale pale nahitaji tu kutafuta chanzo kipya cha mapato nisije uwa watoto na njaa. CONTROLA
 
Mkuu wazo Zuri sana, ila nakushauri Kama wewe ni mgeni Kariakoo tunza pesa yako kwanza, njoo kkoo chagua unataka kupambana na biashara gani.. tengeneza connection na mawinga wa biashara hiyo, ukishaisoma vizuri ndio uweka pesa yako. Ushauri wangu ni huo tu mkuu. Hicho kiasi ni kikubwa sana mkuu. Na vilevile kinaweza kidogo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wazo Zuri sana, ila nakushauri Kama wewe ni mgeni kariakoo tunza pesa yako kwanza, njoo kkoo chagua unataka kupambana na biashara gani.. tengeneza connection na mawinga wa biashara hiyo, ukishaisoma vzr ndio uweka pesa yako.. ushauri wangu ni huo tu mkuu. Hicho kiasi ni kikubwa sana mkuu. Na vilevile kinaweza kidogo..

Sent using Jamii Forums mobile app

Nashukuru sana kwa ushauri wako bro, ushauri mzuri sana.
 
Hiyo biashara una uzoefu nao au umeshawahi kuifatilia kwa ukaribu mkuu
 
Leo March 21st ndio naona hii thread na mwisho kumbe ulinitag ila ukakosea ID yangu ikaingia kama "msg" ndio mana sikuona.

Acha leo nigeuke kama smart911 niseme ile kauli yake pendwa,kwakua uzi ni wa 2020 "Natumai mtoa thread ulipata mwongozo"
 
Back
Top Bottom