Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Rais wa Shirikisho wa riadha nchini Anthony Mtaka amesema nafasi aliyoshika mwanariadha wa Tanzania Alphonce Ferex Simbu katika mashindano ya olimpiki yaliyomalizka jana nchini Brazil imeonyesha kuwa Watanzania kwenye riadha wanaweza kama wakiandaliwa vizuri.
Akiongea na ITV Mtaka amesema Watanzania wasibeze nafasi hiyo kwani tangia mwaka 1964 hakuna Mtanzania ambaye aliwahi kushika nafasi hiyo hivyo mchezaji huyo ameuhisha mchezo wa riadha na kwamba ameonyesha mwanga kuwa Tanzania inaweza kama itawekeza katika riadha.
Aidha Mtaka ameyashukuru mashirika yote ambayo yameonyesha nia ya kutaka kumsaidia mchezaji huyo huku akiwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi tarehe 25,mwezi huu katika uwanja wa ndege ili kumlaki mchezaji huyo.