Elections 2010 Mtakaodhulumiwa ccm iongezeeni chadema nguvu

Elections 2010 Mtakaodhulumiwa ccm iongezeeni chadema nguvu

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
18,887
Reaction score
7,673
CCM ni chama cha Dhuluma, hili lipo wazi.
Tumesikia tayari wagombea wa CCM wameshaanza kumwagiwa mchanga wa macho.
Peter Msola (waziri wa mawasiliano) amefanya ghiliba ili awanie kiti cha Ubunge bila kupingwa. Dili limebumburuka.
Dodoma mjini zoezi la kura za maoni limeahirishwa, mbunge anayemaliza muda wake ambaye wakazi wa Dodoma Mjini hawataki hata kumsikia amekula njama na katibu wa wilaya ili kumpitisha. Tayari katibu amehamishiwa Morogoro.
Kyela nako inasemekana Mwakyembe amekaliwa kooni na Mwakipesile na kambi yake na tayari dhuluma ya wazi dhidi ya mpiganaji huyu imeanza kudhihirika.
Shinyanga (Bukombe na Mbongwe) kura za maoni zimeahirishwa. Wagombea 16 wamegomea zoezi maana zipo dalili zisizo na shaka kuwa wagombea fulani wanapendelewa.
Arusha, Felix Mrema na Elisa Mollel wanahujumiwa,
Batilda Buriani na yeye yumo kwenye listi ya kuwahujumu wenzake Arusha.
Ole Sendeka mambo yake sio mazuri sana na tayari amelalamika kuhujumiwa.
Kwa majimbo haya inaonekana kabisa ki ujumla kuwa hali si nzuri ndani ya chama.
Nawaomba, wote watakaodhulumiwa wafanye kama walivyofanya wenzao wa Karatu (kipindi kile Slaa alipopigwa mchanga wa macho CCM), wafanye kama walivyofanya Kigoma kaskazini, Mpanda Kati, Moshi mjini ambako poote hapo upinzani umechukua majimbo baada ya CCM kuhujumiana. Watakao hujumiwa waunganishe kura zao wazielekezee CHADEMA ili tupate sauti ya kutosha Bungeni.
 
Wanang'ang'ania nini CCM? wakati wajua wazi kuwa ni chama cha kale isiyotaka mabadiliko.

Wahamie CHADEMA
 
Back
Top Bottom