Mtake msitake jogoo atawika tu

Mtake msitake jogoo atawika tu

JOSE KASANO

Senior Member
Joined
Apr 23, 2013
Posts
122
Reaction score
95
1.Tanzania nchi yetu, yenye amani na upendo,
umoja mshikamano, watu wenye ukarimu,
ewe ni mwema mlezi, daima tutakulinda,
Tutunza amali zetu, nchi yetu istawi.

2.Jambo la kusikitisha , pia linalotutisha,
Nchi yaanza bomoka, kwa kuliwa nao MCHWA,
MCHWA hawa ni balaa, nchi wanaimaliza,
Wanauma pande zote, tumebakia mifupa.

3.MCHWA washirikiana, kutunyonya mpaka tufe,
Damu imetukauka, mifupa imejinyoosha,
Mwanzo tuliwaamini,kwamba waweza tulinda,
KICHUGUU tukawapa, wakitunze na wakilinde.

4.Wamekula kila kitu, kwenye KUCHUGUU chetu,
Tulikuwa na karanga, maharage na mahindi,
Soya, ulezi mtama na miti yenye fahari,
Nyamapori na kufuga, maziwa pia dhahabu.

5.Wamekula kwa umoja, hadi vyote vikaisha,
Watuanza na sisi, toka kichwa hadi kucha,
Tukilia kwa uchungu, kwao hicho ni kicheko,
Cha kusikitisha sana, MALKIA yuko kimya.

6.MALKIA twamwambia, MCHWA wako waonevu,
Wmekula mali zetu, na damu zetu kunyonya,
Wanatuuma kwa fujo, tena bila ya makosa,
Wenzetu wameuawa, bila hatia yoyote.

7.MALKIA akasema; nyinyi ndio wachokozi,
Ngoja mshughulikiwe, mkajifunze adabu,
Kila siku ninasema, ktulie hamtaki,
Na sasa nawaagiza, waume kwa meno yote.

8.Mimi mnanisumbua, kwa mikelele yenu,
Nina wageni wa mbali, watafuta pa kuishi,
Nimewagawia pale , ambako nyinyi mwaishi,
Mnapaswa kuondoka ,ili tufuge na FARU.

9.KICHUGUU hiki changu, nitagawana na wageni,
Nyinyi tafuta pengine, hapa hamnayo shea,
Nitafanya nitakalo, nyinyi hamna ubavu,
Atakayeziamsha, nitazibomoa zote.

10.Tukauliza KASISI, ni nini twaweza fanya,
KASISI akatujibu; UMOJA WENU NDO NGUVU,
Huyu jamaa hawezi, mkiamua simama,
Muonesheni dalili, ndipo atapozinduka.

11.Tukaanzia ARUSHE, tukiongozwa na LEME,
Kumuonyesha dalili, kwamba tumeshajipanga,
Na yeye akajipanga, kuja kutushambulia,
Tena bila ya kujua, kwamba sisi ni WELEDI.

12.Akamtuma MWIGULE, MWEME pia naye TENDWE,
Kuyarusha makombora, ili yatuangamize,
Kumbe tuna mahandaki, yenye futi NNE chini,
Baada ya kulipua, YAKAWALIPUA WAO.

13.Wakaanza kukimbia, TUNAKUFA! TUNAKUFA!,
Twajilipua wenyewe, wanajililia sana,
MALKIA akasema; MMEFANYA KAZI GANI?
Ninataka maelezo, ya kila mmoja wenu.

14.MWEME AKAJIELEZA; Mkuu samahanini,
Mimi kazi nimefanya, lakini nimezidiwa,
Jamaa wamejipanga, japo hawana silaha,
Wameunganika wote, ikabidi nikimbie.

15.Na kama unakumbuka, nilimwamisha KAMUHANDE,
Baada ya kumuua, MWANGOSE kule NYOLOLE,
Ndugu walichachamaa, ilikuwa ni hatari,
Bado kasheshe ya ULIMBOKE, KIBANDE na BOMU la ARUSHE.

16. TENDWE AKAJIELEZA; Mkuu mimi nashindwa,
Kalamu kuitumia, ninataka kuwafuta,
Ila nawe una KOSA, na tena tangu ZAMANI,
Napaswa anza na WEWE, kisha wao KUFUATIA.

17. Unataka niwafute, kwa aina ya viatu,
Wanavyotaka nunua, wakati wewe unavyo,
WANAHITAJI VYEKUNDU, WAKATI WEWE UNA VYA KIJANI,
MBONA VYOTE NI VIATU, MIMI KOSA SILIONI!!!!!!!!!

18.MWIGULE akadakia, mkuu kazi ni ngumu,
Mimi nimejitahidi, kufungua kesi nyingi,
Ili tuwafunge wote , ila zote wameshinda,
Pesa nyingi zimeisha, mafanikio hakuna.

19.Nimewakimbia sana, kule Arushe nasema,
Njia nimezitafuta, MCHANA kama USIKU,
Ili wasinikamate, Adhabu kuangukia,
Ninachoweza kusema, jamaa wanaye MUNGU.

20.Malkia akachukia, na sasa ahangaika,
Ataka kuwafukuza ila wengine hapati,
Kulia ana KINANE, kushoto anaye NEPI,
PINDE naye ni kikwazo, kwa kauli za kijinga,

21. MALKIA ainama, kichwa akishikilia,
Mimi nikafanye nini, mbona sasa nalemewa,
MCHWA sasa wameshindwa, SISIMIZI WANANGUVU,
WANAGUVU NYINGI KWELI, WANATAKA KUNING'OA.

22.Labda nikawaite, ili tukaridhiane,
Kabla ya kufikia, mwaka 2015,
Ila hawatokubali, niliwapuuza sana,
Na sasa wameamka, au nikawakimbie,

23.Wanaimba nyimbo nyingi, tena za kiukombozi,
Jamii yawakubali, kwamba wanawatetea,
Michango wanachangiwa, nguvu kujiimarisha,
DALILI NINAYOONA, NIKAANZE KUFUNGASHA,

24. Sisimizi wananguvu, alizowatia MUNGU,
Watembea kifua mbele, VIFARU VIKIWAPISHA,
Kama moto wa nyikani, usioweza zimika,
MALKIA NAO MCHWA, WABAKI KUJISHANGAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

T A F A K U R I


N.B. Unaweza kuimba kadri sauti na nyuzi unazoweza na uzipendazo.
 
Back
Top Bottom