Mtalamu wa maswala ya uzazi Tafadhali nisaidie hili

iryn

Member
Joined
May 31, 2010
Posts
58
Reaction score
26
Nina ujauzito ambao kulingana na wataalamu niko wiki ya 33. Leo nimeshituka kidogo, nikiwa natembea kama moja ya mazoezi ghafla tumbo lilibana kwa chini ya kitovu na nikahisi maumivu kweli.

Baada ya muda nikahisi maumivu yakiongezeka hadi kwenye nyonga . nimejikaza na kuingia ndani kujilaza lakini nikawa na hofu kweli.

Je , inawezekana MTU kupata maumivu ya labour wakati huu au yaweza kuwa tatizo jingine? Naona walau maumivu sasa yanapungua ila naomba kufahamiahwa chanzo yaweza kuwa Ni nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…