MTALAWANDA NI VAO SAHIHI

MTALAWANDA NI VAO SAHIHI

Gota8s

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2014
Posts
201
Reaction score
190
Kipini alipenda pamela, ikavimba pua. Si ujinga kutenda ukitazama wengine, la muhimu kuwaza ni je, umeipata sababu ya kulitenda lile.wanalofanya wenzio?

Nilipata fununu kuwa, nzige wako mbioni kuanguka uwandani kivuli kiwapo kirefu. Nimechungulia anga naona ushwari japo minong'ono imeshamiri. Ila nikitega sikio langu vema, nausikia mvumo wa nzige hawa wakikaribia nyanda zetu. Nimesikia nzige hawa hawatakula majani yote ya mimea, isipokuwa watatafuna shina la mimea ili mmea uanguke na uote upya.

Yamenilevya maneno haya, kwa maana nimeambiwa bua la mmea laweza kuchipua na kuleta tena matunda murua, huenda sijaelewa vema.

Mbega, kima, nyani, tumbili na ngedere huwafanania watu japo tofauti ni weledi, utambuzi, siha, ustaarabu.
Japo wote wanyama, ila sungura hamfanani Nyumbu. sungura si wa kuhama na hutumia janjaye kumghilibu fisi.

Ilisikika kisa cha kasa mwerevu aliyemudu urefu wa kina cha maji ya bahari.. kwamba huwaambia kobe wa nchi kavu wazichome nyumba zao wakaishi mwituni. Akili kumkichwa, ama kweli kobe wanapaswa wainame wakune vema vichwa vyao.

Kama hukuelewa maana yake mwanangu niwie radhi. ila urefu wa njia si hoja, utafika hata kwa kuchechema na wongofu hautakutindia..

Cha kuelewa ni kuwa mpingo ni mti mashuhuri sana mwituni, ila si kwa ajili ya kuponya waja, La!! Ni nkingi na uchongi.

Chonde chonde mwanakwetu njozi si njema siku zote. mpinge anayekuambia utumie vyoo vizuri uvionavyo ndotoni. Matokeo ya uhalisia wake hautaishia huko bali laloni.

Nia njema niliyonayo
[HASHTAG]#FightWhenYouGetReasonTo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#UseYourOwnEyesToSee[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom