Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Raia wa kigeni kutoka Ufaransa, Nakar Fszman (51), amepatikana akiwa hai baada ya kupotea katika Bahari ya Hindi, eneo la Kisiwa cha Songosongo, Wilaya ya Kilwa.
Fszman alipotea Februari 23, 2025, wakati akifanya utalii kwa kutumia Boti aina ya Kayati maarufu kama Kidau, inayotumia kasia. Mtalii huyo aliwasili nchini Februari 16, 2025, akiwa na mkewe na watoto wawili.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Lindi, Fszman alipatikana Februari 24, 2025, saa tatu asubuhi, katika pwani ya Kilwa Kivinje, umbali wa maili nane za baharini (takriban kilometa 12.9) kutoka alikopotea. Alikuwa hai na mwenye afya njema baada ya juhudi za kikosi cha wanamaji cha Jeshi la Polisi (Marine), kilichofanya msako mkali baharini.