Mtama yatoa zaidi yamilioni 300 mikopo ya asilimia 10

Mtama yatoa zaidi yamilioni 300 mikopo ya asilimia 10

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mkuu wa Wilaya ya Lindi VICTORIA MWANZIVA amezindua zoezi la utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa halmashauri ya Mtama ikiwa ni fedha za mapato ya ndani ya halmashauri na kutoa Hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni Mia tatu sitini, laki tano na thelathini na tisa Elfu.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatatu tarehe 10 Februari, 2025 katika Ukumbi wa halmashauri hiyo ambapo vikundi 52 kati ya 172 vilivyokidhi vigezo katika uhakiki vimepata mikopo hiyo.

Soma Pia: Waziri Mchengerwa: Fedha za mikopo za asilimia 10 ni za moto, tusisikie vikundi hewa


Akizungumza katika hafla hiyo, licha ya kuvipongeza vikundi vyote, MWANZIVA amewataka kwenda kuzitumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kufanya marejesho kwa wakati.
 
Back
Top Bottom