Nasri A Kulemba
Member
- Oct 16, 2015
- 20
- 56
MTAMBO WA MABAO NDANI YA WANYAMA MAN CITY ,KARIBU UINGEREZA ERLING HALLAND. [emoji460]️
Imeandikwa na Nasri Kulemba[emoji3578]
Kuna namna ya kukubaliana juu uwezo,maamuzi na kipaji ,kisha tukapa jibu ya kuwa huyu ni mchezaji mahili juu ya vigezo hivyo, lakini pia tunaweza kukubaliana kuwa unakipaji lakini usiwe mahili kwasababu umechukua neno kipaji pekee na kutelekeza misamiati ya maamuzi na uwezo.
Kipaji ni kudra kutoka kwa muumba huzaliwa nayo mwadamu,uwezo hutokana na kile ambacho ulichojifunza na pia maamuzi ni akili inayofanya kazi kwa wakati,usahihi ili kutekelaza yale ambayo yanatokana na Kipaji na uwezo. Hapa unafikia anga la umahili na ndio maana suala la kukubaliana linachukua nafasi yake.
Bila shaka dunia imekubaliana juu ya uwezo na umahili alionao Erling Haaland kwenye suala la kufumania nyavu ,ametua kwenye ligi ya bi mkubwa kule uingereza [emoji2527],kwa mbwembwe kweli kweli.
Ametua akiwa anatabasamu,akiangalia kulia na kushoto anaona mabegi yake yalivyojaa takwimu zake kuliko mavazi, inafurahisha sana maana uwezo kipaji na maamuzi siku zote itakujenga kwenye kujiamini na kufanya kazi yako kwa ufanisi.
Haaland ameshinda tuzo kadhaa za kibinafsi na kuvunja rekodi mbalimbali. Wakati wa msimu wa 2019-20 akiwa na Salzburg, alikua kijana wa kwanza kufunga katika mechi tano mfululizo za UEFA Champions League.
Alikuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa msimu uliofuata. Mnamo 2020, Haaland alishinda tuzo ya Golden Boy, wakati mnamo 2021 alipewa Mchezaji Bora wa Msimu wa Bundesliga na alijumuishwa kwenye FIFA FIFPro World11 mnamo 2021.
Namba pekee ni alama tosha zinazokuonyesha Manchester City wameleta balaa la namna gani katika ligi kuu ya uingereza ,ametoka ujerumani akiwa amecheza michezo 89 na kufunga mabao 86,juzi ametoka. kufikisha mabao 20 kati ya michezo 21 akiwa na timu yake ya taifa ya Norway.
Kwasasa jamaa anamiaka 21 ,bado kinda kabisa anaeanza ,lakini takwimu zake ni kama mchezaji mkomavu mwenye miaka 27 aliye juu ya kilele cha ubora wake.
Nyota njema huonekana asubuhi; wasawahili wanasema. Halland akiwa na umri wa miaka 18 tayari ameshaonesha makeke yake katika suala la kusalimiana na walinda mlango, kwani aliwahi kufunga mabao 9 ndani ya mchezo mmoja dhidi ya honduras kwenye ushindi wa mabao 12 .
Bika shaka sidhani kama kuna mtu anashaka juu ya ubora wa huyu jamaa katika suala la kufunga ,kwake ni jambo rahisi sana kama kula chakula. Siwezi kupepesa macho Halland sio mbahatishaji.
Amekamilika kweli kweli ,mshambuliaji aliyekamilika mwenye nguvu ,kasi na ufundi miguuni..ana akili ya mpira na mpambanaji . Unamashaka juu ya kuiweza ligi ya uingeraza .
Isikupe shida. Halland kiutendaji anacheza ligi ya aiana yeyote duniani kwa namna kipaji chake lilivyojipika. anacheza kwa mtindo wa aina yeyote katika falsafa zote kwenye kandanda.
Soka la uingereza linahitaji nguvu ,kasi na upambanaji, sifa zote hizo halland anazo kama mchezaji ,sio rahisi kumtoa kwenye njia kwasababu mwamba amekamilika sana kwenye utimamamu wa kimwli .. Piili ni mrefu kiasi atawapa shida mabeki wengi kuweza kumdhibiti.
Sio mchezaji mvivu,ana akasi kiasi kwamba hata kwenye mpango wa counter attack bado utaupata ubora wake ,kwa namna alivyo sio rahisi kwa beki mmoja kuweza kumkaba binafsi .
Utapata faida zaidi kama endapo utaziba mianya na njia ili mipira iseiweze kumfikia, lakini kumbuka yupo Man city timu yeyenye mafundi wengi wenye uwezo wa kupenyeza mipira.
Bado balaa lipo pale pale ,ni namna gani unavyoweza kuizibiti Man city iliyo na Erling Halland. Tatizo ni Erling Halland yupo na Manchester City iliyo chini ya Pep Gurdiola unaaanzaje kupata wasiwasi juu ya kuendeleza ubora wake .
Msimu ulioisha Manchester city ndio iliyofunga mabao mengi kuliko timu yeyote pale Epl ,na wamecheza bila ya kuwa na mshambuliaji mahili wa kati, mara nyingi Pep amewatumia Rahim Sterling ,Foden na Kervin de bruyne kama washambuliaji wa kati waongo .
Lakini timu yao imemaliza msimu ikiwa na mabao 99, hii inamaanisha kwenye muunganiko wa timu Halland atafunga sana ;na hapa bado hatujaweka uwezo wake kwenye kutungua walinda mlango.
Usiwe na shaka juu ya Halland kuhusu kufanya vizuri, tambua kuwa suala la kufunga kwake Hallland halijawahi kuwa fumbo alafu kumbuka yupo kwenye timu ambayo hata bila kuwa na mshambuliaji inafunga mabao ya kutosha. Mnyama Halland ndani ya wanyama Man city.
Atafunga sana pale Man city, labda apate majeruhi, la sivyo namuona Halland aliyeuwasha moto Dortmund anakuja kuuwasha Uingereza. Ubora wa Manchester City na umahili wa Halland kama tulivyokubaliana ni balaa lingine kwa mabeki wavivu EPL.
#Nskmichezonaburudani.
#nskmichezonaburudani