MTANANGE Simba V/S Coastal Union direct report

Status
Not open for further replies.

youngsharo

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
2,491
Reaction score
500
Mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Simba Sports Club na Coastal Union ya jijini Tanga utakaofanyika hapo kesho umekuwa ni mchezo unaosubiriwa kwa hamu hasa kwa upande wa Simba,
ukizingatia kwamba mahasimu wao Dar_es Salaam Young Africa Sc Juzi Walifanya vizuri, hivyo hawana budi kukaza buti ili kuepukana na makelele ya mahasimu wao endapo watafungwa.

Simba ipo katika harakati za kujinasua dhidi ya kushuka daraja kwa kupoteza mwelekeo kwenye mzunguko wa kwanza, wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu nzuri ya mchezo uliopita baada ya kujinyakulia pointi 3 muhimu kutoka kwa Ruvu Shooting,

Aidha katika mechi ya juzi ya watani wao Yanga waliibuka na ushindi wa bao moja kwa mtungi dhidi ya hao Coastal Union goli lililofungwa na beki mahiri Nadri Haroub Al Maarufu (Canavaro) katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Hivyo Coastal Union hawatokuwa tayari kupoteza mechi mbili mfululizo nyumbani kwake.
 

Acha Dharau Wewe Eti Simba Ipo Ktk Harakati Za Kujinasua Kushuka Daraja. Nani Kakuambia? Hivi Wewe Unajua Mpira Kweli? Hebu Nipe Tofauti Ya Points Kati Ya Anayeongoza Ligi Na Nafasi Iliyopo Simba. Mkiwa Mmekunywa Viroba Vyenu Na Kushindiliwa Mitalimbo Kunako Tigo Msiwe Mnakurupuka Namna Hii. Huyo Baba Yako Mwenyewe Rais Malinzi Kwenda Kwake MSALANI a.k.a Chooni ( Kutoa Haja Big ) Kunaitegemea Simba Sports Club. Simba Ikishuka Daraja Na Tanzania Nayo Inapotea ktk Ramani Ya Dunia.
 

hahaaa!
mbona umepanic broh, habari ndo iyo utake usitake hapa mwaka huu muombe mungu msishuke daraja lkn ubingwa bwiiiii! Alaf Huyo Malinzi Wako Mi Namjulia Wapi?
N last wakushindiliwa ni ww sio mm.
 
mi ntakuwa mkwakwani kuangalia mkia ukishikwashikwa
 
Ndala kubahatisha kigori kimoja ndo kafanya vizuri mpaka unashangaa.

Ama kweli wewe ndo wale mnaoona kichuguu mnashangaa.. Ngoja kesho tukuoneshe mlima ili uzimie kabisa.
 
Ahsante kwa kuanzisha uzi siku moja kabla ya mchezo kwani mikia ilianzisha uzi siku moja kabla ya mchezo kati ya COASTAL UNION vs YANGA huku yakitumia maneno ya dharau.

halafu fanya editing mkuu iwe MIKIA na simba kama ulivyoweka.
 
Mwana SIMBA mwenzangu umetumia maneno mazito sana.........
 
Ndala kubahatisha kigori kimoja ndo kafanya vizuri mpaka unashangaa.

Ama kweli wewe ndo wale mnaoona kichuguu mnashangaa.. Ngoja kesho tukuoneshe mlima ili uzimie kabisa.

ahsante ila chungeni maneno yenu kesho sio mbali.
 
Ndala wana bahati walicheza na refa.....kwa kuyakataa yale magoli mawili ya wazi...vinginevyo mkubwa angeumbuka..........
 
Ahsante kwa kuanzisha uzi siku moja kabla ya mchezo kwani mikia ilianzisha uzi siku moja kabla ya mchezo kati ya COASTAL UNION vs YANGA huku yakitumia maneno ya dharau.

halafu fanya editing mkuu iwe MIKIA na simba kama ulivyoweka.

poa mkuu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…