Mtandao gani naweza kutumia kwenye Smart Tv hapa Tanzania

Mtandao gani naweza kutumia kwenye Smart Tv hapa Tanzania

mfianchi

Platinum Member
Joined
Jul 1, 2009
Posts
11,904
Reaction score
8,371
Wadau nisipoteze muda wenu, nauliza nje ya mkoa wa Dar Es Salaam ni mtandao wa kampuni ipi ya intaneti/simu ambao naweza kutumia kuangalia netflix au huduma za streaming kwenye smart tv hasa tulio wilayani.

Kwa jiji la Dar Es Salaam najua Zuku ndio wana unafuu kiasi bahati mbaya wilayani hatuna Zuku sana sana ni TTCL lakini bado sijajua ufanisi wao na kwa wale wajuzi na watumiaji wa vifurushi kwenye smart tv ni vifurushi vya aina gani ie GB , speed kwa yule wa matumizi ya kawaida(sio kutwa kukaa kwenye kochi ukiangalia runinga) ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom