Mtandao gani naweza kutumia kwenye Smart Tv hapa TZ

mfianchi

Platinum Member
Joined
Jul 1, 2009
Posts
11,904
Reaction score
8,371
Wadau nisipoteze muda wenu, nauliza nje ya mkoa wa Dar Es Salaam ni mtandao wa kampuni ipi ya intaneti/simu ambao naweza kutumia kuangalia netflix au huduma za streaming kwenye smart tv hasa tulio wilayani, kwa jiji la Dar Es Salaam najua Zuku ndio wana unafuu kiasi bahati mbaya wilayani hatuna Zuku sana sana ni TTCL lakini bado sijajua ufanisi wao na kwa wale wajuzi na watumiaji wa vifurushi kwenye smart tv ni vifurushi vya aina gani ie GB , speed kwa yule wa matumizi ya kawaida(sio kutwa kukaa kwenye kochi ukiangalia runinga
 
Vodacom SuperKasi kama upo karibu na mjini , kama upo ndani ndani kuna portable wifi - Voda
 
Achana na mitandao ya simu ina gharama kubwa sana.

Kuna kampuni mpya ya internet imeingia inaitwa Konnect - Satellite internet Tanzania wana offer nzuri sana ya unlimited internet ya satelaiti (yaani unapata popote) 20Mbps shared kwa Tshs. 60,000/- kwa mwezi. King'amuzi chake ni Tshs. 345,000/-

Kama uko serious na kustream au kutumia internet nyumbani (yaani kila mtu nyumbani anatumia) inatakiwa uondoke kabisa kwenye mitandao ya simu na kuhamia kwenye makampuni yanayotoa huduma za unlimited internet. Mambo ya kununua vifurushi vya kupangiwa GB ngapi halafu eti unastream utafilisika, au utapoteza hela nyingi bila sababu.

Na hakuna mtandao wa simu unaoweza ukakupa spidi halisi kama ya kampuni za unlimited. Mitandao ya simu ina watumiaji wengi sana kuliko haya makampuni ya unlimited.
 
Inaonekana nzuri hii
 
Wako vizuri kinomer
Ila kwenye Custer Care ndo tatizo?
 
Wadau nisipoteze muda wenu, nauliza nje ya mkoa wa Dar Es Salaam ni mtandao wa kampuni ipi ya intaneti/simu ambao naweza kutumia kuangalia netflix au huduma za streaming kwenye smart tv hasa tulio wilayani, kwa jiji la Dar Es Salaam najua Zuku ndio wana unafuu kiasi bahati mbaya wilayani hatuna Zuku sana sana ni TTCL lakini bado sijajua ufanisi wao na kwa wale wajuzi na watumiaji wa vifurushi kwenye smart tv ni vifurushi vya aina gani ie GB , speed kwa yule wa matumizi ya kawaida(sio kutwa kukaa kwenye kochi ukiangalia runinga
Ttcl adsl kama ipo ndio best kwa value
4mbps ni 25,000
8mbps ni 50,000

Kwa 4mbps utaangalia youtube na Netflix kwa HD ya kawaida yaani 720p.

Kama unajiweza vodacom superkasi 130,000

Hizo za Satelite hazina uwezo wa ku live stream, kama ni mpenzi wa mpira na vitu vyengine vya kuangalia live hazitafaa, ila youtube na Netflix hazina neno.
 
Asante sana mkuu, umekuwa msaada mkubwa kwetu yanapokuja mambo ya teknolojia, ubarikiwe sana, sasa ngoja niwavae TTCL
 
Achana na mitandao ya simu ina gharama kubwa sana.

Kuna kampuni mpya ya internet imeingia inaitwa Konnect - Satellite internet Tanzania wana offer nzuri sana ya unlimited internet ya satelaiti (yaani unapata popote) 20Mbps shared kwa Tshs. 60,000/- kwa mwezi. King'amuzi chake ni Tshs. 345,000/-

Kama uko serious na kustream au kutumia internet nyumbani (yaani kila mtu nyumbani anatumia) inatakiwa uondoke kabisa kwenye mitandao ya simu na kuhamia kwenye makampuni yanayotoa huduma za unlimited internet. Mambo ya kununua vifurushi vya kupangiwa GB ngapi halafu eti unastream utafilisika, au utapoteza hela nyingi bila sababu.

Na hakuna mtandao wa simu unaoweza ukakupa spidi halisi kama ya kampuni za unlimited. Mitandao ya simu ina watumiaji wengi sana kuliko haya makampuni ya unlimited.
Shukrani sana mkuu
 
shida hizi smart tv recent ni 2k, 4k mpaka 16k..so far streaming services zipo kwenye 2k..utatumia roughly gb 8 kustreem movie ya saa limoja..weka kitu cha voda hapo uone dakika 7 tu unapewa notification gb moja imekata hahaha. tafuta fiber kama uko vzuri.
 
Niliwahi wasiliana nao initial costs ilifika 1.5m nikalala mbele hii ilikuwa last year!

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
Pia internet yao sio unlimited kwa advertised speed, ina terms na condition kuna gb kadhaa ukitumia speed inakua ya kobe

Mfano cha 60,000 unapewa gb 10 tu za speed kubwa, kwa matumizi ya Smart tv hizo ni siku 1 tu zimekata.
 
Ttcl adsl kama ipo ndio best kwa value
4mbps ni 25,000
8mbps ni 50,000

Kwa 4mbps utaangalia youtube na Netflix kwa HD ya kawaida yaani 720p.

Kama unajiweza vodacom superkasi 130,000

Hizo za Satelite hazina uwezo wa ku live stream, kama ni mpenzi wa mpira na vitu vyengine vya kuangalia live hazitafaa, ila youtube na Netflix hazina neno.

mkuu unaweza ukani elimisha kuhusu hii TTcl adsl inakuaje? na je iyo ya 8mbps inaweza kusstrean had 1080p?
 
Youtube 1080 ni 5mbps, Netflix pia ni 5mbps hivyo kwa Popular website ndio utastream kwa Full HD.

Adsl ni zile waya za simu za kizamani, inapatikana NChi nzima sehemu zenye Nguzo za simu unaweza kuwasiliana na Tawi la TTCL la karibu kama inapatikana eneo lako.

Sema angalia kama Fiber ipo kwanza kama haipo ndio nenda Adsl.
 
nimekupata mkuu,asante
 
Back
Top Bottom