Mtandao kusuasua siku mbili hizi ni njama ya kuzuia kampeni ya Tone Tone kuichangia CHADEMA?

Mtandao kusuasua siku mbili hizi ni njama ya kuzuia kampeni ya Tone Tone kuichangia CHADEMA?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Salaam Wakuu,

Toka kampeni ya Tone Tone izinduliwe kumekwa na changamoto ya mtandao ambao haieleweki eleweki.

Wakati wameshazindua na wakawa wanaitana mbele kila mmoja kuhamasisha watu wake, commentszilikuwa zinapita chini baadhi wakisema miamala inakataliwa, mara inakaa pending muda mrefu mpaka mtu anakata tamaa, nk.

Mtandao haujakaa vizuri mpaka leo, wakati mwingine unakuwa slow sana au fanyikazi kabisa mpaka uhamie kwenye VPN!

Ni hujuma kwa CHADEMA ndio ili raia wasiweze kuchangia na CHADEMA kufikia malengo yao?

CCM itakuwa imeshikwa pabaya sana kama wameona hii ndio solution iliyobaki kuwazima CHADEMA. Itakuwa wanapumulia mashine!

Aroo mnakwamisha mambo yetu bana, hamuoni kama hii inaathiri pia mapato ya serikali na taasisi nyingine?
 
Kulinda na Kuitetea amani yetu sio jambo la kuoneana huruma bali ni jambo la msingi kabisa, lenye uzito tofauti kabisa na mambo yenu ya katiba na uchaguzi
 
Kulinda na Kuitetea amani yetu sio jambo la kuoneana huruma bali ni jambo la msingi kabisa, lenye uzito tofauti kabisa na mambo yenu ya katiba na uchaguzi
🤣🤣🤣 amani ipo hiyo unazungumzia Mkuu? Ukute kuna maana nyingine ambayo hatuijui
 
Back
Top Bottom