SoC04 Mtandao wa Masoko Sahili: Tufufue Uchumi wa Tanzania kwa Soko la Bidhaa za Ndani

Tanzania Tuitakayo competition threads

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
3,644
Reaction score
4,315
Sio ujinga kweli kudhania kwamba, tuyakuza uchumi kwa kuzalisha tu, bila kujali tunauzaje kilichozalishwa? Kufikiri nusunusu ni ishara ya kutokomaa kiakili.

Nini hupelekea maonesho ya nanenane/sabababa na mengineyo kama ya viwanda na kilimo kufana sana? Ni mkusanyiko mkubwa wa wanunuzi, wauzaji na wabunifu wa bidhaa za ndani mahala pamoja. Ninaiita 'NANENANE EFFECT'. Naamini si lazima nane nane kudumu wiki moja tu maana kwa maendeleo ya sasa ya miundombinu na teknolojia jambo hilo laweza kufanyika si tu kila siku, bali hata masaa ishirini na manne! Kufikia lengo hili wala sio tata ni rahisi tu (sahili).

Mtandao wa Soko wa Sahili ni mfumo mpya unaolenga kuinua uchumi wa Tanzania kwa kukuza biashara ya bidhaa na huduma zinazozalishwa ndani ya nchi. Mfumo huu unajumuisha maduka makubwa kote nchini yanayouza bidhaa za ndani, pamoja na duka la mtandaoni linalofanya bidhaa hizi kupatikana kwa urahisi kwa Watanzania wote. Serikali ama kampuni binafsi inaweza kutenga soko maalumu (mall) linaloitwa SAHILI MARKETPLACE NETWORK. Maeneo ya nanenane yaliyopo yanaweza kutenga eneo dogo na kuliboresha kuwa nanenane ya kudumu.

shopping-mall-7340181_1280.jpg

Picha: Nguyên Trần kutoka Pixabay

Ni kama ilivyo 'mlimani city mall' lakini kwa hapa ni kila wilaya inakuwa na 'mall' yake inayouza bidhaa zote zinazozalishwa wilayani humo. Na ina vyumba vyenye bidhaa kutoka kila mikoa ya nchi nzima. Utakutana na viazi ulaya katika mkoa wa Mbeya, Wine za zabibu mahala ilipo Dodoma yaani kama nanenane vile. Nanenane effect.

Katika dunia ya leo, uchumi wa nchi yoyote unategemea sana uwezo wake wa kuzalisha na kuuza bidhaa na huduma. Tanzania, ikiwa na utajiri wa rasilimali na watu wenye vipaji, inahitaji jukwaa la kuonyesha bidhaa na huduma zake bora. Hapo ndipo Mtandao wa Soko la Sahili unapoingia kwenye nafasi yake sasa.

Maduka haya makubwa yatapatikana katika kila kona ya nchi, tunaweza tukaanza na kila wilaya na miji, yatatoa fursa kwa wajasiriamali wadogo na wakubwa kuuza bidhaa zao. Anzia na ubunifu, mavazi ya kiasili, vyakula vya kitamaduni, hadi vifaa vya kisasa, kila kitu kitatolewa kwa ubora wa hali ya juu na kwa bei zinanazomstahili muuzaji na mteja.

Faida za Mtandao wa Soko la Sahili

Kwanza kabisa, mfumo huu utaongeza ajira kwa Watanzania
. Kila duka litahitaji wafanyakazi wa ngazi mbalimbali, kutoka wahudumu wa maduka, mameneja, hadi wafanyakazi wa usafirishaji na usambazaji. Hii itapunguza tatizo la ukosefu wa ajira na kuinua hali ya maisha ya Watanzania wengi.

Pili, Mtandao wa Soko la Sahili utawezesha wajasiriamali wadogo kuonekana na kufikia soko pana zaidi. Kwa kawaida, wajasiriamali wadogo hukutana na changamoto nyingi wanapotaka kuuza bidhaa zao katika masoko ya ndani na nje. Mtandao huu utawapa jukwaa la moja kwa moja la kuuza bidhaa zao kwa wateja wa ndani na hata wa kimataifa kupitia duka la mtandaoni.

Tatu, kwa kununua bidhaa za ndani, tutakuwa tunasaidia kuimarisha uchumi wa ndani. Fedha zitakazotumika katika ununuzi wa bidhaa hizi zitarudi kwa wazalishaji wa ndani na kusaidia katika kukuza biashara zao. Hii itasaidia kuleta mzunguko mzuri wa fedha ndani ya nchi na kuongeza pato la taifa.

Nne, mfumo huu utasaidia katika kuboresha ubora wa bidhaa za ndani. Kwa kuwa na jukwaa la kuuza bidhaa kwa wingi, wazalishaji watalazimika kuboresha viwango vyao vya ubora ili kushindana na bidhaa zingine kwenye soko. Hii itasaidia kuongeza thamani ya bidhaa za Tanzania na kuvutia wateja zaidi.

Tano, wateja wote watajipatia nafasi ya kuzielewa bidhaa zao maana wanapata uwezo wa kuzungumza na wajasiriamali wazalishaji moja kwa moja. Yaani ni kama kutembelea mabanda ya maonesho kila siku, au masaa ishirini na nne. Maana yapo mawasiliano ya wazalishaji katika kila banda na kila bidhaa. Pia kama tukiikuza na kutumia mfumo uliopo mkondoni wa maduka na mabanda ya maonesho basi itakuwa ni nanenane kila siku na kila saa!

Sita, ni rahisi kufuatilia taratibu mbalimbali za kibiashara mfano kodi TRA, usajili, TBS, Barcode, SIDO, TIRDO, COSTECH na leseni maana wahusika wanalo eneo moja la kuwakutanisha, watapeana taratibu ujuzi na mbinu bora kutekeleza kila kitu.

Duka la Mtandaoni la Sahili
Mbali na maduka halisia katika malls kila wilaya, Mtandao wa Soko la Sahili pia unajumuisha duka la mtandaoni ambalo litakuwa na bidhaa zote zinazopatikana kwenye maduka ya kimwili. Duka hili litakuwa na faida kubwa sana kwani litawawezesha Watanzania wote, popote walipo, kununua bidhaa kwa urahisi na haraka.
Screenshot_20240604-155026_Chrome.jpg

Picha kwa hisani ya mtandao wa Sahili Marketplace Network (Sahili – Bidhaa na huduma murua za kijasiriamali za wa – Tanzania)

Wateja wataweza kupitia bidhaa mbalimbali, kuzichagua, na kulipia mtandaoni. Baada ya hapo, bidhaa hizo zitawasilishwa kwenye milango yao. Hii itapunguza muda na gharama za kusafiri kwenda kwenye maduka ya kimwili, na kufanya ununuzi kuwa rahisi zaidi kwa watu wote, wakiwemo wale wa maeneo ya vijijini.

Tena kwa kuwa ni mtandao, kunakuwa hakuna mipaka ya mambo tunaweza kuboresha, mfano uwezekano wa kuwa na jukwaa la makala na machapisho yanayohusu ujasiriamali na bidhaa zenyewe. Hapa kila mtanzania anayo fursa ya kujifunza mbinu mpya kama uzalishaji sabuni, mashine mpya na maujanja ya kiubunifu, uandishi wa blogu na nafasi za mikopo.
Screenshot_20240604-155606_Chrome.jpg

Picha kwa hisani ya mtandao wa Sahili Marketplace Network

Mifumo ya mtandaoni inaweza 'kusevu' gharama kwa kuwezesha wanunuzi kuweka miadi na muuzaji/mbunifu kabla ya kutembeleana dukani. Mfano, jumanne nitakuja kuutizama mtambo wa utotoleshaji, tukutane nanenane saa tano unipatie maelekezo zaidi. Au muuzaji anaweza kusema mimi nitafungua banda langu kila jumatatu na alhamisi maana ndizo siku ninakuwa nimevuna mazao niwauzie ya shamba leoleo (fresh produce).

Kufanya Tanzania Kuwa na Soko la Kisasa la kudumu.

Mtandao wa Soko la Sahili ni hatua kubwa kuelekea katika kufanya Tanzania kuwa na soko la kisasa na lenye nguvu. Mfumo huu utasaidia kupambana na changamoto za soko la ndani, kutoa ajira, kuboresha bidhaa za ndani, na kuongeza pato la taifa. Hii ni fursa ya kipekee kwa Watanzania wote kuchangia katika kujenga taifa lenye uchumi imara na wenye uwezo wa kujitegemea.

Kwa kumalizia, ni jukumu letu sote kama Watanzania kuunga mkono Mtandao wa Soko la Sahili. Tunapokuwa na soko la ndani linaloimarika, tunaimarisha uchumi wetu na kuongeza fursa za maendeleo kwa kila mmoja wetu. Hivyo basi, tuunge mkono bidhaa za ndani, tuunge mkono Mtandao wa Soko la Sahili, na kwa pamoja, tujenge Tanzania yenye nguvu na ustawi.

Fikiria Tanzania ambayo kila mtu anao uwezo wa kuzalisha bidhaa yake nyumbani na kuitangaza kwa watu wa maeneo yake mara moja (kama kuwa na meza/banda nanenane vile). Lakini pia kulifikia soko la kitaifa na kimataifa kwa kuweka bidhaa yake mkondoni (online). Ni 'nanenane effect' duniya mzima! Ahsanteni sana.
 
Upvote 8
Sio ujinga kweli kudhania kwamba, tuyakuza uchumi kwa kuzalisha tu, bila kujali tunauzaje kilichozalishwa? Kufikiri nusunusu ni ishara ya kutokomaa kiakili.

Nini hupelekea maonesho ya nanenane/sabababa na mengineyo kama ya viwanda na kilimo kufana sana? Ni mkusanyiko mkubwa wa wanunuzi, wauzaji na wabunifu wa bidhaa za ndani mahala pamoja. Ninaiita 'NANENANE EFFECT'. Naamini si lazima nane nane kudumu wiki moja tu maana kwa maendeleo ya sasa ya miundombinu na teknolojia jambo hilo laweza kufanyika si tu kila siku, bali hata masaa ishirini na manne! Kufikia lengo hili wala sio tata ni rahisi tu (sahili).

Mtandao wa Soko wa Sahili ni mfumo mpya unaolenga kuinua uchumi wa Tanzania kwa kukuza biashara ya bidhaa na huduma zinazozalishwa ndani ya nchi. Mfumo huu unajumuisha maduka makubwa kote nchini yanayouza bidhaa za ndani, pamoja na duka la mtandaoni linalofanya bidhaa hizi kupatikana kwa urahisi kwa Watanzania wote. Serikali ama kampuni binafsi inaweza kutenga soko maalumu (mall) linaloitwa SAHILI MARKETPLACE NETWORK. Maeneo ya nanenane yaliyopo yanaweza kutenga eneo dogo na kuliboresha kuwa nanenane ya kudumu.
View attachment 3008341
Picha: Nguyên Trần kutoka Pixabay

Ni kama ilivyo 'mlimani city mall' lakini kwa hapa ni kila wilaya inakuwa na 'mall' yake inayouza bidhaa zote zinazozalishwa wilayani humo. Na ina vyumba vyenye bidhaa kutoka kila mikoa ya nchi nzima. Utakutana na viazi ulaya katika mkoa wa Mbeya, Wine za zabibu mahala ilipo Dodoma yaani kama nanenane vile. Nanenane effect.

Katika dunia ya leo, uchumi wa nchi yoyote unategemea sana uwezo wake wa kuzalisha na kuuza bidhaa na huduma. Tanzania, ikiwa na utajiri wa rasilimali na watu wenye vipaji, inahitaji jukwaa la kuonyesha bidhaa na huduma zake bora. Hapo ndipo Mtandao wa Soko la Sahili unapoingia kwenye nafasi yake sasa.

Maduka haya makubwa yatapatikana katika kila kona ya nchi, tunaweza tukaanza na kila wilaya na miji, yatatoa fursa kwa wajasiriamali wadogo na wakubwa kuuza bidhaa zao. Anzia na ubunifu, mavazi ya kiasili, vyakula vya kitamaduni, hadi vifaa vya kisasa, kila kitu kitatolewa kwa ubora wa hali ya juu na kwa bei zinanazomstahili muuzaji na mteja.

Faida za Mtandao wa Soko la Sahili

Kwanza kabisa, mfumo huu utaongeza ajira kwa Watanzania. Kila duka litahitaji wafanyakazi wa ngazi mbalimbali, kutoka wahudumu wa maduka, mameneja, hadi wafanyakazi wa usafirishaji na usambazaji. Hii itapunguza tatizo la ukosefu wa ajira na kuinua hali ya maisha ya Watanzania wengi.

Pili, Mtandao wa Soko la Sahili utawezesha wajasiriamali wadogo kuonekana na kufikia soko pana zaidi. Kwa kawaida, wajasiriamali wadogo hukutana na changamoto nyingi wanapotaka kuuza bidhaa zao katika masoko ya ndani na nje. Mtandao huu utawapa jukwaa la moja kwa moja la kuuza bidhaa zao kwa wateja wa ndani na hata wa kimataifa kupitia duka la mtandaoni.

Tatu, kwa kununua bidhaa za ndani, tutakuwa tunasaidia kuimarisha uchumi wa ndani. Fedha zitakazotumika katika ununuzi wa bidhaa hizi zitarudi kwa wazalishaji wa ndani na kusaidia katika kukuza biashara zao. Hii itasaidia kuleta mzunguko mzuri wa fedha ndani ya nchi na kuongeza pato la taifa.

Nne, mfumo huu utasaidia katika kuboresha ubora wa bidhaa za ndani. Kwa kuwa na jukwaa la kuuza bidhaa kwa wingi, wazalishaji watalazimika kuboresha viwango vyao vya ubora ili kushindana na bidhaa zingine kwenye soko. Hii itasaidia kuongeza thamani ya bidhaa za Tanzania na kuvutia wateja zaidi.

Tano, wateja wote watajipatia nafasi ya kuzielewa bidhaa zao maana wanapata uwezo wa kuzungumza na wajasiriamali wazalishaji moja kwa moja. Yaani ni kama kutembelea mabanda ya maonesho kila siku, au masaa ishirini na nne. Maana yapo mawasiliano ya wazalishaji katika kila banda na kila bidhaa. Pia kama tukiikuza na kutumia mfumo uliopo mkondoni wa maduka na mabanda ya maonesho basi itakuwa ni nanenane kila siku na kila saa!

Sita, ni rahisi kufuatilia taratibu mbalimbali za kibiashara mfano kodi TRA, usajili, TBS, Barcode, SIDO, TIRDO, COSTECH na leseni maana wahusika wanalo eneo moja la kuwakutanisha, watapeana taratibu ujuzi na mbinu bora kutekeleza kila kitu.

Duka la Mtandaoni la Sahili
Mbali na maduka halisia katika malls kila wilaya, Mtandao wa Soko la Sahili pia unajumuisha duka la mtandaoni ambalo litakuwa na bidhaa zote zinazopatikana kwenye maduka ya kimwili. Duka hili litakuwa na faida kubwa sana kwani litawawezesha Watanzania wote, popote walipo, kununua bidhaa kwa urahisi na haraka.
View attachment 3008319
Picha kwa hisani ya mtandao wa Sahili Marketplace Network (https://sahili.net/wp/)

Wateja wataweza kupitia bidhaa mbalimbali, kuzichagua, na kulipia mtandaoni. Baada ya hapo, bidhaa hizo zitawasilishwa kwenye milango yao. Hii itapunguza muda na gharama za kusafiri kwenda kwenye maduka ya kimwili, na kufanya ununuzi kuwa rahisi zaidi kwa watu wote, wakiwemo wale wa maeneo ya vijijini.

Tena kwa kuwa ni mtandao, kunakuwa hakuna mipaka ya mambo tunaweza kuboresha, mfano uwezekano wa kuwa na jukwaa la makala na machapisho yanayohusu ujasiriamali na bidhaa zenyewe. Hapa kila mtanzania anayo fursa ya kujifunza mbinu mpya kama uzalishaji sabuni, mashine mpya na maujanja ya kiubunifu, uandishi wa blogu na nafasi za mikopo.
View attachment 3008322
Picha kwa hisani ya mtandao wa Sahili Marketplace Network

Mifumo ya mtandaoni inaweza 'kusevu' gharama kwa kuwezesha wanunuzi kuweka miadi na muuzaji/mbunifu kabla ya kutembeleana dukani. Mfano, jumanne nitakuja kuutizama mtambo wa utotoleshaji, tukutane nanenane saa tano unipatie maelekezo zaidi. Au muuzaji anaweza kusema mimi nitafungua banda langu kila jumatatu na alhamisi maana ndizo siku ninakuwa nimevuna mazao niwauzie ya shamba leoleo (fresh produce).

Kufanya Tanzania Kuwa na Soko la Kisasa la kudumu.

Mtandao wa Soko la Sahili ni hatua kubwa kuelekea katika kufanya Tanzania kuwa na soko la kisasa na lenye nguvu. Mfumo huu utasaidia kupambana na changamoto za soko la ndani, kutoa ajira, kuboresha bidhaa za ndani, na kuongeza pato la taifa. Hii ni fursa ya kipekee kwa Watanzania wote kuchangia katika kujenga taifa lenye uchumi imara na wenye uwezo wa kujitegemea.

Kwa kumalizia, ni jukumu letu sote kama Watanzania kuunga mkono Mtandao wa Soko la Sahili. Tunapokuwa na soko la ndani linaloimarika, tunaimarisha uchumi wetu na kuongeza fursa za maendeleo kwa kila mmoja wetu. Hivyo basi, tuunge mkono bidhaa za ndani, tuunge mkono Mtandao wa Soko la Sahili, na kwa pamoja, tujenge Tanzania yenye nguvu na ustawi.

Fikiria Tanzania ambayo kila mtu anao uwezo wa kuzalisha bidhaa yake nyumbani na kuitangaza kwa watu wa maeneo yake mara moja (kama kuwa na meza/banda nanenane vile). Lakini pia kulifikia soko la kitaifa na kimataifa kwa kuweka bidhaa yake mkondoni (online). Ni 'nanenane effect' duniya mzima! Ahsanteni sana.
Kwa hio hiz mall n sawa na Magulio/ minada?
 
Kwa kumalizia, ni jukumu letu sote kama Watanzania kuunga mkono Mtandao wa Soko la Sahili. Tunapokuwa na soko la ndani linaloimarika, tunaimarisha uchumi wetu na kuongeza fursa za maendeleo kwa kila mmoja wetu. Hivyo basi, tuunge mkono bidhaa za ndani, tuunge mkono Mtandao wa Soko la Sahili, na kwa pamoja, tujenge Tanzania yenye nguvu na ustawi.
NICE
 
Kwa hio hiz mall n sawa na Magulio/ minada?
Hakika, tunaweza kusema hivyo.

Sasa hapo itatakiwa kuweka kwa upana zaidi. Fikiria gulio la kijijini, mwanakijiji anazalisha bidhaa na kuhudumia watu wa kijiji chake tu. Akienda mbali ni kijiji jirani tu hapo.

Sasaa tumuongezee uwanda, auze kijijini kwake, vijiji jirani, wilaya hiyo nzima mkoa na Taifa kabisa kutokana na usafirishaji wa vifurushi haraka.

Lakini pia kutokana na intaneti aweze kujitangaza na kuhudumia dunia nzima kwa Sahili Marketplace Network!
Unajua ili mtu ajikimu atahudumoa mwisho familia yake, ili ajiweze anatakiwa kidogo aweze kuhudumia mtaa/kijiji/mji/wilaya yake..... lakini ili awe milionea basi awe na uwezo wa kuifikia nchi yake na kwa mantiki hiyo ni kwamba Tanzania tuitakayo haitaweza kutengeneza mabilionea na matilionea bila kuhudumia dunia mzima
 
Back
Top Bottom