Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Vitu vilivyotolewa ni mchele kilo 100, unga wa ugali kilo 50, unga wa ngano kilo 50, mafuta ya kula lita 20, miswaki katoni 1, dawa ya meno katoni1, mafuta ya kupaka katoni 1, sabuni ya unga mifuko 2, miche boksi 2, mifagio 4, pampasi 7, sabuni ya maji lita10, majani ya chai dazeni 1, wembe dazeni1, sukari kilo 25, chumvi katoni 1, vifaa vya usafi brashi za chooni 4 pamoja na mopa 4
Akiongea katika tukio hilo, Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Kilimanjaro (SP) Asia Matauka ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa mtandao wa Polisi wanawake mkoani hapa, amewataka kudumisha upendo kwa kujitoa ili kuendelea kujenga ushirikiano katika jamii
Vivyo hivyo aliwashukuru askari polisi wanawake mkoani hapa kwa umoja wao kwa kutenga muda na kutembelea wazee hao, hii inaonyesha upendo na inajenga taswira nzuri kwa Jeshi la Polisi kushiriki shughuli za kijamii
Aliendelea kuwashukuru na kuwapongeza watendaji wote wa kituo hicho kwa upendo walionao kwa wazee hao kwani kujitolea kwao ni sadaka mbele za Mungu, huduma wanayotoa kuhakikisha wanawahudumia vyema siku zote wakiwa katika hali nzuri