Mtandao wa Starlink sasa unapatikana Burundi.

Mtandao wa Starlink sasa unapatikana Burundi.

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Mtandao wa Bwana Elon Musk wa Starlink sasa unapatikana Burundi.

Juzi rais wa Afrika Kusini alisema anamkaribisha na ameongea na Elon kutoa huduma ya Starlink hata kwa kuondoa vikwazo vya umiliki wa wazawa wa ndani.

Starlink inapatikana Afrika kusini ila kwa huduma ya Roaming kama ilivyo Uganda. Uganda inaruhusu huduma ya Starlink kutumika hata kama bado haijaruhusiwa rasmi nchini.

Starlink inakupa internet ya kasi sana kwa gharama nafuu sana. Wastani wa shilingi elfu 80 huku ukipewa GB 1,024 ama Terabyte 1 kwa mwezi na iwapo utamaliza hizo GB kabla ya mwezi kuisha basi utatozwa shilingi 400 za Kitanzania kwa GB moja. Hii ni kwa matumizi ya kawaida speed ya hadi megabytes 100 kwa sekunde.

Matumizi ya kibiashara unalipa kati ya shilingi laki 2 na laki 3 huku ukipewa terabyte 2 za data kwa speed ya hadi megabytes 220 kwa sekunde.

Wakati wenzetu wakitangulia kiteknolojia, sisi bado tuko nyuma kwa kutunga kanuni za ajabu ajabu zisizo na kichwa wala miguu.

View: https://x.com/Starlink/status/1838555166099808610?s=19
 
Back
Top Bottom