Mtandao wa "YAS" Msipokuwa serious mtaanguka sokoni

Mtandao wa "YAS" Msipokuwa serious mtaanguka sokoni

Addons

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2023
Posts
393
Reaction score
571
Kwanza niwapongeze kwa kufanikiwa kweny manunuzi ya mtandao wa tigo na mkaubadilisha jina kuwa" YAS"

Mahali mnapofeli kwa sasa
1. Mmebweteka saana, kweny promotion mkiendelea kutegemea promo za zamani za tigo na mnachofanya ni kubadili jina tuu la promotion.

2. Kukosekana kwa ubunifu na kukosa tyming ya soko.

My take: unapoamua kuubadilisha mtandao jina ni sawa na kuanza biashara!
Hili gape/ombwe la kibiashara mliloliacha ukitokea mtandao wenye offa nzuri hakika watu watazitupa Laini zenu.

Biashara ya simu ina ushindani mkubwa saana. Inatakiwa unapoleta mtandao mpya sokoni uumbatane na offa za kutosha sana!

Ni vile kwasasa mnafanya kazi Kama Cartel ingekuwa enzi zile umngeshapotea zamn sana.

Kama mmeshiwa mbinu tumieni hata za zamani
1: internet kuanzia saa 6 usiku buree mpk asubuhi
2: vifurushi vya chuo vijazwe dk na sms
3: mtoe zawadi Live Kama pikipiki, trekta, gari!! Sio mnaishia kusema kuwa umeingia kweny droo.

Mkubali hasara ya muda mchache mpate faida ya muda mrefu..

Tumieni Tax Holiday hii ya sasa mpate faida ya muda mrefu....
Changamkeni
 
Kwa pamoja tunasonga mbele kuelekea kesho iliyobora zaidi kamwe atuache kuwa wabunifu na kuendelea kujijenga sisi ndiyo kizazi kinachobadilisha mchezo kila tunapounganishwa fursa mpya zinafunguka tunatengeneza kesho yetu kwa kufata matakwa yetu wenyewe tuna uhuru wa kubuni na uhuru wa kujieleza mchezo umebadilika sisi ndo wapindua meza tukiungana hakuna wa kutuzuia wakati umewadia muda ndio huu ni wakati wetu

Tigo sasa Ni Yas
 
Mtandao ni mkubwa sana na una malengo makubwa sana!! Focus yenu isije badilika maana mtu akiliona hili gape anaweza kutengeneza mtandao wake chap na akawatake over, msiache space kwa wapinza
 
ila sijui kwann walisema MIXX cjui Ina maana gan?
Labda waliona ni SWAGA ya huko darisalama. Ila huku vijijin tulipo kwanza walipoona tu jina limebadilika wengine walitupa line zao kwamba zimeharibika,wengine walihofia pesa zao kuwa zitaibiwa so wakatoa kwenye akaunti zao na kuachana na line.
Mawakala nao walizingua yaani ni vurugu tupu.
 
Kuna namna wanatakiwa kufanya followup ya soko lao hasa vijijn
 
Back
Top Bottom