Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 752
Na Mwandishi Wetu
Mtangazaji anayekuja kwa kasi kwenye field hiyo Zamaradi Nketema ambaye anapiga mzigo katika Kituo cha Radio Clouds Fm, naye ameamua kwa moyo mmoja kuingia kwenye siasa huku kiu yake ikiwa ni kutinga Bungeni baadaye Novemba mwaka huu.
Juzi, Jumanne Amani lilitumiwa ujumbe mfupi na chanzo chake makini, kikitonya kwamba: Oyaaa Zamaradi amechukua fomu ya kugombea Ubunge kupitia Viti Maalum CCM.
Kama kawa, bila kuchelewa Askari wa Amani alimvutia waya Zamaradi na kutaka kujua ukweli wa stori hiyo ambapo alitoa ushirikiano wa kutosha.
Ni kweli nimechukua fomu leo (Jumanne) na ninatarajia kurudisha kesho. Siwezi kuongea mengi kwasasa, labda hadi nitakaporudisha fomu. Nitafute kuanzia kesho (Jumatano) na kuendelea, ninaweza kuwa na mengi ya kuongea, alisema Zamaradi.
Zamaradi anakuwa Mtangazaji wa pili wa kituo hicho kurusha karata yake kwenye kinyanganyiro hicho baada ya marehemu Amina Chifupa kufanikiwa kuingia bungeni kwa uteuzi kama anaowania.
SOURCE: GBL